Mkataba wa DP World umetufumbua macho

Mkataba wa DP World umetufumbua macho

Kenney

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2013
Posts
295
Reaction score
174
Habari za Mchana Wazalendo Mliomo jamvini,

Kuna vitu ambavyo usipo viangalia kwa makini au kuvipuuzia vinaweza kuleta matokeo ambayo yakawa ni majuto baadae sababu tu ya kudhani uwepo wa mambohayo ni mambo ya kawaida tu. Kuna hii mikataba inayo endelea huku mitaani kwetu ambayo tunaweza kuichukulia ni mambo ya kawaida kabisa katika maisha yetu ya kila siku ndiyo hiyo inakuja kukua kiwango cha Taifa na kuleta haya mambo kama ya DP World.

Naomba nilete mfano wa haya makusanyo (Niite Ushuru) wa Taka, imefika mahali umekuwa holela, haueleweki kila mhusika anafanya atakavyo> Huu ushuru wa Taka wengine wanaita wa Usafi inaonekana au pengine ndivyo ilivyo uatakiwa ukusanywe na Halmashauri ya mahali husika kwa sababu wao ndiyo wanao miliki na kusimamia shughuli zote zinazofanyika katka maeneo husika.

Kutokana pengine na kuzidiwa na majukumu kuna Halmashauri zinalazimika kubinafsiha shughuli zinazoendana na uzoaji taka, mpaka ukusanyaji wa ushuru husika, kwa mtizamo wango ubinafsishaji wa hizo shughuli siyo jambo baya, ila sasa huwa najiuliza inakuwaje Halmashauri (nadhani baadhi) zina binafsisha kila kitu kwa mkandarasi mmoja, mfano mtu huyo ndiye anaye zoa taka, halafu mtu huyohuyo ndiye anakusanya ushuru wa Usafi (Pengine hata Tenda imepatikana kwa mashaka nyingi zinasemekana ni deal za wakubwa) hapo sasa ndiyo haieleweki Halmashauri inafaidika na nini ikiwa Mkusanya Taka taka huyohuyo ndiye mkusanya ushuru na viwango anajipanga mwenyewe ambavyo hata vigezo vya viwango havina uwiano (unachajiwa labda kwa kuangaliwa usoni) na monitoring ya hawa makandarasi sijui ikoje. Kwa ujumla hao watu ni wababe, hawana ustaarab kabisa wakikukuta na wewe ni mnyonge imekula kwako.

katika hali hiyo nimeona niwashirikishe Wazalendo wenzangu wenye uelewa wa masuala haya tupate kusaidiana katika kukabiliana nayo.
 
Umefumbua macho ila kuna wanaojitia uziwi
Kwakweli Madaraka yanatia kiburi, lakini uwakute kwenye kuomba kura walivyo wanyenyekevu, wanapiga na magoti!
 
Back
Top Bottom