Mkataba wa kifisadi wa Lugumi kuwasilishwa mbele ya Kamati ya Bunge leo

Mkataba wa kifisadi wa Lugumi kuwasilishwa mbele ya Kamati ya Bunge leo

Hao wanaokabidhi hiyo ripoti wao hawakuona hayo madudu mapema?Matatizo yote hayo yanaendelea kukomaa kwasababu BUNGE ndio linachangia kulipua kwa kutotaka maazimio ya kamati teule za bunge yanapopelekwa kwao kuwa na mtazamo wa itikadi za tofauti za vyama.Laiti kama BUNGE lingekua moja matatizo yasingezidi kumea,kukua na kukomaa.Wabunge acheni kudharau mawazo mazuri kutoka kwa wengine hatakama mnazo itikadi tofauti.Raisi ninashauri aendelee kutumbua hayo MABUSHA bila kuangalia mtu usoni yeye ninani,nimtoto au mjukuu wa nani au baba wa watoto na wajukuu wangapi.Kwabunge tulilonalo haliwezi kutimiza ndoto zetu kwa kua watuhumiwa wapo ndani mle.Pia kwakua wanalinda unga wao(wabunge)JPM piga kazi hawezi kufikia hatua ya kukinzana na wewe hata kiasi cha uchaguzi kuitishwa upya ninao uhakika hawana uthubutu.Pia wakithubutu wanyonge walio wengi kuliko hayo majizi watakupigia kura
 
KAMATI gani ...hakuna issue kama hiyo ratiba ya vikao inaisha hivyo. ..
2.Issue ilivyo sio nzuri kabisa huwezi lipa hela ndefu hivyo in advance na kazi bado kabisa ..hili NI janga
 
Hakuna lolote hapo ni wivu, husda baina yao na watu wanatafuta kick tu hakuna lolote
 
kama upo sawa unataka waseme ni mbovu ili ufurahi ama? kwa staili hii ya kufurahishana sijui kama tutafika kweli.
Kwa hiyo wewe unataka waseme ni mzuri wakati ni mbaya ili wakufurahishe wewe na mafisadi mwenzako mlio zoea vya kunyonga sio?
 
Wataweka pingamizi mahakamani kama alivyofanya chenge wa escrow.
 
Waisha ifix tiyari utasikia mkataba upo sawa kabisa
Kitendo cha kupewa 99% halafu ameweka vituo 14 moja kwa moja mkataba umevunjwa duniani hakuna mkataba wa aina hiyo tena kazi yenyewe imefanyika miaka zaidi ya 2 iliyopita labda kama wabunge wa ccm wataamua kupotezea kama kawaida yao
 
Kwa kweli hii kesi ipo wazi sana
 
Mtakumbuka ule mkataba uliozua mjadala mkubwa kati ya jeshi la polisi na kampuni ya Lugumi ambayo mtoto wa rais mstaafu Ridhiwan Kikwete amekiri kuwa na urafiki na mmiliki wake. Leo mbivu na mbichi inajulikana baada ya kuwekwa hadharani mbele ya kamati ya bunge.

Kashfa hiyo inatarajiwa kukigawa Chama Cha Mapinduzi baada ya wabunge kudhamiria kutumia kashfa hiyo kuwaumbua vigogo kama hatua ya kulipiza kisasi baada ya wenzao kuburuzwa mahakamani kwa kashfa ya kuomba rushwa.

Stay tuned, mtoto wa mfalme maji yanakaribia shingo!
Mfalme na mwanaye walikua smart sana, ni vigumu sana kuikuta mikono yao moja kwa moja mahala ilipodokolewa mboga, walichokua wanakifanya ni kukuagiza Orally ukibisha huna kazi au matanga yaweza kukuhusu
 
Kipindi hiki hakuna wa kifuani na mgongoni wote ni watoto na kila goti litakwenda kupigwa
 
Wadau tupeni update ya huu mkataba wa lugumi umefikia wapi naona tumetolewa nje Bila kujua.
 
Mfalme na mwanaye walikua smart sana, ni vigumu sana kuikuta mikono yao moja kwa moja mahala ilipodokolewa mboga, walichokua wanakifanya ni kukuagiza Orally ukibisha huna kazi au matanga yaweza kukuhusu
Mhhh watu mna vijinenoneno
 
Back
Top Bottom