Kwa maana nyingine hao wahindi walitoa info za uwongo ili kuweza kuupata mkataba huo wa kuendesha shirika la Reli. Hivyo siri kali ina kila sababu ya kuuvunja kwa kuwa hao wahindi hawakuwa wakweli na hivyo kuepuka hayo malipo ya shilingi 18,000,000 kwa mwezi za hizo injini saba, malipo ambayo yanafanywa hata kama injini hazifanyi kazi. Pia inabidi siri kali iyasimamishe malipo hayo mara moja.
Augustoons,
Mshikaji siamini kuwa TRC ilikuwa mzigo mkubwa kwa serikali isipokuwa serikali (viongozi) ilitaka TRC ife kifo kama cha makampuni mengine yote makubwa kisha yapate kuuzwa kwa bei njugu wakikamata hizo 10%...All these things Tanesco, NBC, IPTL, City water na mashirika yote muhimu ni faida tupu kwa mabillioni ya fedha. Matajiri wote wakubwa duniani wameshika mashirika kama haya kama sio serikali zao..Na ndio ugonvi mkubwa wa IMF na nchi maskini kwani mataifa makubwa target yao ni hizi miundombinu ya uchumi wa nchi...Hivyo siwezi kuamini kwamba TRC ilikosa mwekeshaji kama walivyosema wakati tumeanza kuisikia Richmond.
Hizi habari za kufa ni hadithi tupu tusubiri hiyo Jumanne kisha utaona mwenyewe kuwa Wajerumani walikuwa tayari kuingia mkataba tena basi navyokumbuka mimi ilikuwa contracting ambayo serikali yetu ingeendelea kushika 100% share na wao kulipwa fedha za Kufufua na Uendeshaji wa reli hiyo tena navyosikia waliona heshima kubwa ( honoured) kuitumikia serikali yetu ktk vitu ambavyo wao walivijenga kwetu..
KOSA SIO LA WAHINDI HAPA!
Wakati tunapambana na Ufisadi, ni muhimu tukaeelewa mambo ya nchi yanavyo endeshwa kabla ya kurusha mikuki gizani, vinginevyo watatuzidi kete. Mkataba ni kati ya Serikali na Kampuni, kwa mujibu wa sheria, sio kwa mujibu wa Serikali. Serikali haina nguvu ya kuvunja mkataba inapotaka. Inabidi waende kwanza mahakamani.
Kawaida, mahakamani sio rahisi sana kuvunja mkataba. Ndio maana leo jioni tumelipa dola laki moja na nusu kwa dili la Richmond na warithi wake, na kesho asubuhi tutalipa tena.
Ina maana tudai uwajibikaji katika kuingia, sii kujitoa, katika hii mikataba. Wahindi wamekudanganyeni, kwani waliongea kikwao? Mkataba wa kibiashara una vipengele vinavyosema nini la kufanya kama mmoja akishindwa kutimiza wajibu wake. Haiendi kwa kutegemea kauli mtu.
Kosa sio ka wahindi. Ni sisi ndio tatizo (kama hizi habari ni kweli, manake hatujapata details zozote bado.
..HAPANA HUO MSHAHARA WALIAHIDI RITES WENYEWE BILA KUSHINIKIZWA NA SERIKALIO........SASA KUMBE NAO WALIKUWA WANAFANYA USANIII.NADHANI WAMEGUNDUA USANII SI KOSA TANZANIA...INGEKUWA NCHI NYINGINE HIYO TU [KUTOA AHADI YA UWONGO]..INGETOSHA KUWAFUKUZISHA..NA KUNYANGANYWA LESENI....
Ndugu Watanzania kwa mara Nyingine Tena Tunaona Serekali yetu ina vyo tufanyia Usanii.
Mimi ninaomba kumuuliza Huyo Pinda na Bot , mkopo huo umetoka kwenye fungu gani au Bank Ipi? na nini ni Dhamana ya Huo Mkopo?
vip lakn ww si kanjanja?
Ungekuja na hoja pia unafikiri Serikali ingefanya nini!!! wakati wananchi wake wa Mikoa ya Tabora,Kigoma, Shinyanga, Mwanza wakiteseka kwa usafiri?
Assuming hizo hela zimetoka kwenye fungu la maafa? reallocation ya fund is operational issues... by the way it is just mkopo... Watanzania tuna matatizo... tuna muda mwingi wakupiga porojo... is this a issue real?
Kama wamefanya re-allocation au kutoka funga la maafa si waseme kwa uwazi, na huo mkataba wa mkopo kama ni interest free au sivyo kwa nini wasiweke mambo wazi?
Mawazo mazuri but you can not do this when you already have crisis... kama ungewahi kuongoza... ungeona hili ni jambo la kawaida.Maana tumeona mikopo kwa akina Mzindakaya, fedha zilizokuwa zikitolewa na ATC wakati wa Mkataba na SA, ikumbukwe pia ilikuwepo Alliance Air.
Tatu hii kampuni ni ya kibiashara na kila upande una majukumu yake na Contribution yake katika Share capital, sasa kama hiyo project au hiyo biashara ya RITEs inalipa kwanini wasiende kukopa Bank.
Kweli kabisa kama wananchi wa Kigoma, Tabora, Shinyanga, Bukoba, Mwanza wangekuwa na usafiri mbadala... na wa rahisi... au kungekuwa na ushindani wa uendeshaji shughuli za Treni serikali isingeingilia.... angalia hali ilivyo sasa forget about the books you read.Nne ujue mambo ya kibiashara na kiuchumi haya endeshwi kisiasa, ndio maana wakati mwingine viongozi wanatoa maamuzi , ambayo unakuta yanapingana na Sheria au taratibu za kifedha na za kiuchumi.
Juzi juzi tu hapa Fedha zilitolewa wakati wa Issue ya Mahujaji, nayo ilitolewa kwenye Maafa? na Hata zikiwa zimetolewa kwenye maafa hivyo ndio jinsi ya kufanya biashara , ndugu yangu Kasheshe.
Ndugu Watanzania kwa mara Nyingine Tena Tunaona Serekali yetu ina vyo tufanyia Usanii.
Mimi ninaomba kumuuliza Huyo Pinda na Bot , mkopo huo umetoka kwenye fungu gani au Bank Ipi? na nini ni Dhamana ya Huo Mkopo?
Pili hizo Fedha zilizo letwa na Muwekezaji ili kupata 51% share zipo wapi?
Ndio yananza yale yale ya ATC na SA, ambapo serekali iliingia mkataba wa namna hii , mwisho wa siku tukawa tunatoa fedha za uendeshaji.
Haya ndio matatizo ya kusaini mikataba na matapeli ambao walidanganya uwezo wao ili tu wapate huo mkataba. Sasa sijui wanatakiwa warudishe mkopo huo kwa muda gani na riba ni kiasi gani. Haitakuwa ajabu kusikia jamaa hawana uwezo wa kuulipa na kuingia mitini huku TRL ikabaki hoi bin taabani.