ZOMBA WEKA HUO MKATABA HAPA TUKAUCHAMBUE
Zomba, kuna vijiba gani tena hapo?
Rais anposaini mkataba hufanya hivyo kwa niaba ya sisi sote kama taifa na wala hafanyi hivyo kwa manufaa ya familia yake kiasi cha kukufanya uone ya kwamba akifanya hivyo basi waraka huo UBAKIE SIRI UVUNGUNI MWA KITANDA mpaka siku itakapozunda kama ya Dowans ndio mnahaha nayo kuileta mezani ili tukawalipe wamiliki majini babari fedha zetu.
Acha kujizungusha bure, weka huo mkataba hapa jamvini tukausome tuone vipengele vyake vimekaeje maana viongozi wetu hawaaminiki tena kwa lolote lile.
Kujaribu tukupeleka macho yetu kwenye umeme Megawatts 600 utakaopatikana utakaopatikana haitoshi, sharti Watanzani tangu sasa na tukapekue kila mkataba unasemaje na ulitayarishwa na wanasheria gani tofauti na wale waliowahi kututumbukiza kwenye janga kubwa kama taifa kufanya bisahara na Majini wasiojulikana sura wala nchi wanakotoka mle ndani ya Dowans.
Zomba najua sana unavyojuta kilichokufanya uanze kujitambisha na mkataba huo wa Mhe Kikwete hapa jf. Kama wewe si mtaalam wa kutundika ovyo threads zisizokuwa na kichwa wala miguu, tundika na huo mkataba hapa, laa sivyo uondoe kabisa kauli za mijigambo hewa hapa na kutuomba msamaha endapo bado chembe cha ustaarabu na ukomavu unanukia kwako.
Karibu kwa mtihani huu.