Mkate wa Siha

Mkate wa Siha

Mikate ile mitami klikuwa inazalishwa na Shirika la umma NMC. Mashirika ya umma mengi ilifika wakati yalidorora au kufa. Utengenezaji wa huo mate nadhani uliathiriwa na hali hii.
Dah tumejikosea kitu kizuri, inabidi nifuatilie why na nikipata jibu kama nawza pata recipe , itabidi nifanyie kazi.
 
Kwa wale wahenga wenzangu wa Oysterbay na Masaki, mnakumbuka kipindi cha miaka ya 80, pale Morogoro stores, kulikuwa na duka lina uza Mikate ya Siha, kipindi hicho niko mdogo sana sikumbuki vizuri ila ninachokumbuka kama vile ilikuwa inapaikana mara moja kwa week na kulikua kama inagombewa.

Sijui sababu haswa ilikuwa ni nini kugombewa kihivyo na kwanini ilipatikana mara moja kwa weeki na je, Mkate wa Siha ulikuwa mkate unatengenezwa kwa nini haswa, sababu ulikuwana utamu a aina yake.
Maziwa na siagi.
Moshi arusha kipindi hiko wanafunzi wa sec wale walokua na uwezo wakofika mjini ni mkate wa Siha kwa kwenda mbere
 
Maziwa na siagi.
Moshi arusha kipindi hiko wanafunzi wa sec wale walokua na uwezo wakofika mjini ni mkate wa Siha kwa kwenda mbere
Sikujua kabisa Mkate huo ulikua popular hivyo , nilidhani ni maeneo ya Obay na Masaki , nilidhani duka liliku hapo tuu moja na nikadhani ulitengenezwa na bakery ndogo iliyopo hapo eneo la Morogoro Stores in Oysterbay, kumbe ni kitu kilikuwa kikubwa hivyo
 
Nimewaza labda ulikuwa unatengenezwa na mchaga mmoja huko wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,anyway kama ulikuwa unatengenezwa Tazara dasalama kwann ulitoka mara Moja Kwa wiki?
Hata NMC ARUSHA walitengeneza pia kwa ajili ya Arusha na Moshi
 
Sikujua kabisa Mkate huo ulikua popular hivyo , nilidhani ni maeneo ya Obay na Masaki , nilidhani duka liliku hapo tuu moja na nikadhani ulitengenezwa na bakery ndogo iliyopo hapo eneo la Morogoro Stores in Oysterbay, kumbe ni kitu kilikuwa kikubwa hivyo
YES,
Arusha -Moshi ilikuwepo
 
Duh umenikumbusha mbali sana miaka 1987,88 nilikuwa nauza hiyo mikate maeneo ya Buguruni Relini nilikuwa na brother mmoja anaitwa Koba ( jina la utani Wamizoga)
Huyo brother alikuwa anapenda sana kununua mikate ya jana (ndaza) au ile iliotoka na sura mbaya ni nadra sana sisi kununua ya leo leo maana hiyo tulikuwa tunapata kwa bei ndogo

Mikate hiyo tulikuwa tunanunua hapo kiwandani NMC panatizamana na Tazara na tunauza hapo Buguruni Relini kwa bei ya jumla na rejareja
 
Kumbe ilikua popular sehemu nyingi, ila najiuliza kma ilikuwa mitamu kwanini hajaendelea kuwepo wakati uhitaji upo ? au ilikuwa ni ladha tamu ya kawaida tuu kama mikate mingi iliyo kuwepo sasa, ila tuu labda kwa wakati huyo tulikuwa hatuna choice nyingi na mitamu ilikua ni hiyo tuu kwa kipindi hicho na tunaimani kwamba ilikua mitamu sana kwa sisi ulio kula kipindi hicho?
Ile mikati ya siha na ya Arusha ilikuwa mitamu kipindi kile kwa kuwa hali ya uchumi ilikuwa mbaya. Ni kama pilau la enzi zile au wali ndondo vilikuwa vitamu kwa kuwa upatikanaji ulikuwa mbinde. Uchumi umekuwa kwa sasa mikate yote ina viwango tunajionea kawaida
 
Nani anakumbuka wale samaki wa kwenye mkebe kutoka China unapasha kidogo unakula na ugali pia na Tanganyika Beef kutoka Tanganyika Packers zile za kwenye mikebe
 
Hii mikate ilikuwa mitamu😂, ilikuwa inafungwa kwenye kifuko kina maandishi mekundu hivi
 
Hii mikate ilikuwa mitamu😂, ilikuwa inafungwa kwenye kifuko kina maandishi mekundu hivi
Nakumbuka ilikua mitamu sana a ilipo kuwa ikija the whole neigbohood ina jua na foleni na ukichelewa ina kuwa ime kiwisha .
 
Nakumbuka ilikua mitamu sana a ilipo kuwa ikija the whole neigbohood ina jua na foleni na ukichelewa ina kuwa ime kiwisha .
Ndio😂😂, Mimi nilikuwa nakunywa na chai kwa style ya kuiloweka kwenye chai 😂😂😂
 
Nani anakumbuka wale samaki wa kwenye mkebe kutoka China unapasha kidogo unakula na ugali pia na Tanganyika Beef kutoka Tanganyika Packers zile za kwenye mikebe
Samaki sikumbuki , ila Tanganyika Packers numbuka , Baba yangu alikuwa ana nunua Cane beef zilikuwa kwa ajili ya mbwa na paka , zilikuwa zinanukia vizuri sana kiasi unatamani kuonja ila wakasema ni kwa wanyama tuu , ina wezekana ilikuwa ni mabaki ya nyuma za ng'ombe za pale kiwandani .
 
Ile mikati ya siha na ya Arusha ilikuwa mitamu kipindi kile kwa kuwa hali ya uchumi ilikuwa mbaya. Ni kama pilau la enzi zile au wali ndondo vilikuwa vitamu kwa kuwa upatikanaji ulikuwa mbinde. Uchumi umekuwa kwa sasa mikate yote ina viwango tunajionea kawaida
Asante , hilo ndio nilikuwa nina hisi, inawezekana sio kwamba ilikuwa ya ajabu sana ila tuu choices ya different dreads tulikuwa hatuna , ina wezekana ni kama hii hii ya sasa ila tuu kipindi hicho kama unavyosema ni hali ya kiuchumi,sababu najiuliza kama ilikuwa mitamu kihivyo kwanini haikuendelezwa ?
 
Asante

, nilikuwa najiuliza ilitokea wapi ? na je kwanini kwa sasa haipo?
Kipindi hicho mikate ilikuwa adimu sana kama zilivyokuwa bidhaa nyingi. Mikate mingi ilikuwa inaokwa kwenye bakery ndogo ndogo za mtaani ila mikate ya siha ilikuwa inaongoza kwa ubora. Kwa sasa hivi bila shaka itaonekana ni mikate ya kwaidia tu kwani kuna mikate mingi yene ubora.
 
Back
Top Bottom