Napenda kushare nanyi hiki kisa kwani kimetokea eneo lililopo kwa sasa.
Kwanza, hiyo picha si ya tukio husika, pili huyo alikuwa ni mlinzi wa shule ya kanisa ( Likonde minor seminary).
Je silaha aina ya Gobole ilikuwa mali ya nani? Kwa taarifa ni kuwa marehemu alikuwa muwindaji tangu awali hivyo alikuwa anamiliki silaha hiyo kwa utaratibu wa kisheria.
Je kwa nini kajiua? Taarifa zilizopo mtaani ni kuwa marehemu alikuwa na ushirikina katika kazi yake ya uwindaji, sharti ilikuwa ili awe anapata wanyama lazima alale na mabinti zake, tabia hiyo ameifanya siku nyingi na mabinti zake wengine wawili tayari wameolewa. Hivi karibuni alitaka kufanya kwa binti yake mwanafunzi kati ya darasa la nne ama tano, mke wake akapokea malalamiko toka kwa mtoto, akamshtaki serikali ya kijiji, na mmoja wao kwenye baraza la migogoro ni kaka yake na marehemu, mke akaona anazungushwa akaenda mahakamani ( Kigonsera) huko kesi ilikuwa isomwe jana tarehe 2 July, jamaa akaamua kujiua shambani kwake kabla ya kufika mahakamani.