Nikushauri tu,nenda mwenyewe mpaka hapo,fika elezea jambo lako,utapata wahusika utaelekezwa na utakuwa umejionea kwa usahihi,Kilimo hakifanywi kwa Blue tooth,wengi wamelia kwa kufanya kilimo kwa njia ya simu.Ruaha Mbuyuni kumeinua wengi na KUMEWALIZA wengi,kuna watu walikuwa wanaishia gesti tu mashambani hawafiki wanawauliza vijana wao vipi huko,vijana wanawaambia safi kabisa,mtu anaona taabu kuingia kwenye vitalu,mwishowe walilia,Ni vyema ukaenda mwenyewe.