TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linamtafuta mwanamke anayefahamika kwa jina la Queen Mbuba kwa tuhuma za mauaji ya mume wake, Shizya Mwangwale (35), mkazi wa Kijiji cha Igunda, Wilaya ya Mbozi.
Inadaiwa kuwa Shizya alichomwa sindano inayodhaniwa kuwa na sumu begani upande wa kushoto, kisha baadaye kuchomwa kisu tumboni upande wa kulia na mke wake, ambaye alitoroka mara baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, SACP Augustino Senga, tukio hilo limetokea Mei 22, 2026 majira ya saa saa tisa za usiku.
Inaelezwa kuwa pindi Shizya alipomuuliza mkewe kuhusu sindano hiyo, mtuhumiwa alidai kuwa ilikuwa ni dawa kwa ajili ya tatizo la miguu lililokuwa linamsumbua marehemu.
Baada ya tukio hilo, Shizya alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kwa ajili ya matibabu na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya, ambapo amefariki dunia leo Mei 26, 2026 akiwa anapatiwa matibabu.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu Shizya kuwa na mahusiano na wanawake wengine.
Polisi wanaendelea na msako wa kumkamata mtuhumiwa huyo ili hatua za kisheria zichukuliwe.