Afu usiwe unapoteaga hivo kipenzi mama mtumishi.Hapo Mwamposa ametoa "opinions" zake, kadri anavyojisikia au kuona inamfaa yeye. Alichokiongea sio sheria, tena sio neno la Mungu; na sio SI UNIT ya ndoa zote ulimwenguni. Whatever suits him...
Nilitegemea Watumishi wa Mungu wawakumbushe waumini wao juu ya umuhimu wa kutunza viapo vyao vya ndoa na kuwa waaminifu kwa wenzi wao; na sio kukimbilia kuwaambia wanawake wasishike simu za waume wao. Hivi kati ya simu na sehemu za siri ni kipi kinatakiwa kitunzwe na kufichwa zaidi? Sehemu zako za siri unaziweka wazi kama public pizza afu simu ndiyo unajifanya Ina umuhimuuuu.
Tunalea kizazi cha hovyo kwelikweli cha watoto wa kiume ambao definitely watakuja kuwatreat wake zao kama options. Waume wafanye tu wanavyojisikia, na wake hawana options nyingine zaidi ya kuvumilia. Ndiyo maana uzeeni wanaume wengi wana -suffer kwelikweli ilihali wake zao wananawiri tu. What you sow in your wife in your youth; you shall reap it in your old age.
Afu sielewi kwa nini mnataka mwanamke aliyeachwa (divorcee) aone aibu kwa kuachwa/kuacha. Yes ni aibu kama ulifanya ujinga ukaachwa au ulitafuta sababu ya kijinga ili kuvunja ndoa yako; ila kwa mwanamke mwenye akili zake timamu; aliyekaa chini akatafakari na kuona kuwa hiyo ndoa ni threat kwa afya yake ya kiroho, kimwili, kihisia na hata kiuchumi; basi divorce ni uamuzi sahihi kwake.
Afu tusitake ionekane as if kila divorce ikitokea mwanamke ndiye ana-lose; wanaume kibao wameishia kupata depression pia kwa sababu ya kuachwa. Ingawa mbele za watu wanajifanya kujitutumua kuwa hawaumii na wamemove wamevuta vifaa vipya; deep down wanateketea. Tafuta wanawake walioolewa na divorcees afu wakusimulie maisha wanayoishi nao; majority are very very bitter; utalipia uchungu wake wa kuachwa as if wewe ndiyo ulimuacha.
Zamaradi Mketema alipambana weeh na wake wenzie kwa Marehemu Ruge; mwisho akanyoosha mikono juu. Leo yupo zake na Mzee wa "ulisi" na ndoa yao, wanalea watoto wao kwa amani. Kaheshimika from baby momma of father Abraham to a married woman.
Queen Masanja huyo kalilia talaka yake, sasa hivi maisha yake yanamuendea kwa amani. Anafanya vitu, anaishi maono na ndoto zake ambazo asingeweza kuziishi kama angeendelea na ndoa yake na Dr Mwaka. So inategemea na utashi wa mwanamke husika; sio kila mtu anapoteza akidivorce. Wengine wanang'ang'ana kwelikweli wanaishia kufia ndoa; hasara kwa watoto na wazazi wao.
Halafu mlivyo na uchungu mnaonaga kumnyima mwanamke mali ndiyo kumkomesha. Kuna wanawake ambao wapo willing kuacha kila kitu; anasonga mbele kwa ajili ya amani yake ya moyo; naki hapo na mali zako. Peace of mind is all that matters.. .Msiishi na wake zenu kiubabe ubabe as if their lives revolve around marriage.
Hili andiko limenibariki sana.
Wanaume wanataka wao ndio wafiche simu zao, mwanamke akificha ni Malaya🤣🤣🤣