Mke akinunua gari/kiwanja, mkiachana inatakiwa kugawanywa kama wanaume?

Sheria imeeleza wazi kuwa mwanaume ndio ana wajibu wa kummeintain mke wake na watoto na c mwanamke except in exceptional circumstances... So pambana baba..!!

Unajuaje kuwa mimi ni mwanaume!? Nimeuliza swali kutaka kuelimishwa, kama unajua ulitakiwa kutoa elimu kwa sheria zilivyo ila badala yake unajibu kipashkunaku na kisukununu, eti nitafute vyangu, haya Unajuaje kuwa sina vyangu!? Jibu swali la msingi
 
Hio itakuwa matrimonial Property ndugu muuliza swali kwakuwa ni Mali iliyochumwa mkiwa ndani ya ndoa

OK mkuu, mafundi wa sheria mkitusaidia hivi ni ahueni kwetu
 
swali zuri ila lianjibiwa kihuni.Mwenye anajua sheria aseme maana siku zote sheria huwa ni ujanjaujanja tu.Mfano kama mama wa miaka 30 akijihusisha kimapenzi na mvulana wa miaka 14,je huu utaitwa ubakaji ama!?

Asante mkuu kwa kutambua umuhimu wa swali langu, nilitegemea wajuzi wa mambo haya waje kutujibu
 
Inauma sana, mnatafuta unamsaidia anaongeza elimu akirudi ns kupata pesa mara mkopo akinunua gari lake hata kulipanda maneno. Akibahatika na akajenga utaona anahangaika kubadili majina. Wanawake wengi wachoyo wabinafsi
 
Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inasema mali zote zilizopatikana watu wakiwa ndani ya ndoa basi ni mali zao wote isipokuwa kama kuna makubaliano maalumu na wahusika kuwa mali fulani inabaki binafsi kwa mwenza mmoja. Hii sheria ilipata tafsiri nzuri kwenye kesi maarufu miaka ya themanini mwanzoni ya Hawa Mohamed ambapo mahakama ya rufaa ilisema hata kama mwenza hajachangia fedha bado anastahili mgao siku ndoa ikivunjika. Ila bahati mbaya mahakama iliacha fumbo kuwa mgao sio lazima uwe 50/50, bali kila kesi itaangaliwa kwa mazingara yake.
 
Nchi za wanzetu mambo ni shwari, hukuna ubaguzi wa kijinsia, sheria ni msumeno. Huku kwetu mentality ya jamii na mahakimu wengi ni kuwa cha mwanamke ni cha mwanamke, ila cha mwanamme ndio cha ndoa, lakini ukweli sheria haipo hivyo. Sema wanaume wenye kipato duni kwenye ndoa huwa wanaona aibu kupambana mgao wa mali pale ndoa inapovunjika. Kuna mifano, Jide alimtosa mme wake hutusikia mme/mtalaka akikomaa mgao wa mali, tetesi ni kuwa alikubali yaishe kishikaji kwa kupewa kiduchu. Kuna mme wa jaji fulani ndoa imeangukia pua, hana hela anatia tu aibu mjini. Ingekuwa amekomaa mgao mpaka pensheni ya jaji angegawiwa tu.
 
Sheria imeeleza wazi kuwa mwanaume ndio ana wajibu wa kummeintain mke wake na watoto na c mwanamke except in exceptional circumstances... So pambana baba..!!

Gurunyembe detected........
 
Kwa hiyo hutaki kupambana...subir mkeo achume tukuone kifua mbele ukienda kudai mgao wa mali za mkeo..mke akuzalie na bado akutafutie Mali shame on u..!!
Mwenye uzi kauliza kama mke akichuma mali ndani ya ndoa ikitokea wakaachana je na mume nayw ana haki ya kudai mgao ??kama ilivozoeleka kwa wanaume, wanawake kudai mgao pale ambapo mambo yanaenda kombo.........Yawezekana na mimi nikiwa na mali pia nilizochuma pamoja na mke wangu ila docs zinasoma jina langu vivo hivyo kwa mama pia anaweza akawa na mali tulizochuma pamoja ila docs zinasoma jina lake.......Sasa hapo mwenye uzi akawa anauliza je na mwanaume ume ana haki ya kudai kama iwavyo kwa mwanamke???...Afu swali langu kwako kulingana na quote yako hapo juu je wajibu wa mwanamke ktk ndoa ni kuzaa watoto pekee?????
 

Well, mummito ajibu sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…