Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

W
Hata Mimi wangu alikuwa na hiyo tabia ugomvi kidogo tuachane na tugawane mali, ili kuepusha kelele na ujuaji mwingi toka hapo sijawahi mshirikisha kitu tena, nimenunua ardhi sana na kuna kiasi kizuri sana benki hajui na nilishaapa na kuweka nadhiri kuwa hatajua kitu chochote zaidi ya vile alivyokuwa ananiimbia wimbo tugawane, yeye siku pekee ambayo anakuja kujua ni siku ambayo mm nimetangulia mbele ya haki/kufa ndo hapo atapojua maana nategemea kuandika wosia alafu yeye hataridhi kitu toka kwangu zaidi ya vile alivyokuwa ananiimbia wimbo.
WAtoto sasa ndio changamoto au huna watoto wadogo mkuu
 
MZOZO UKAENDELEA,
Watu wakinisihi tuyamalize pembeni Hapa mjini tunawafaidisha Watu, nikawambia Sina MDA wa kupoteza kwenda mahakamani. Na Hilo pagale analodai tugawane Kama Kuna mtu anapesa Hapa aseme naliuza cash pesa yote mpeni huyu Mwanamke akaanze maisha yake. Kama hamna Basi niitieni dalali liuzwe leo leo silazi damu Mimi. Watu wakamsihi wife ashuke pale aombe radhi anadhalilika yeye. Wife akaanza kujishusha nimsamehe Lile neno lilimponyoka TU bahati mbaya. Nikasema maamuzi yangu Ni hayo hayo. Sirudi nyuma. Kazi iendelee.

Hatujakaa Sana,
CANTER tupu ikaingia, nikawaambia vijana wapande twende nyumbani nako tukapakie kila kitu vitu vya ndani navyo vipelekwe Magomeni. Vijana wakasema utatuongezea hela, nkwambia hamna shida ntawaongezea. Vijana wakapanda, CANTER ikang'oa tukaelekea nyumbani. Tulipofika hatukua na muda wa kupoteza vijana wakaingia ndani haraka na kuanza kusomba vitu kuingiza kwny Gari.

Ghafla wife na baadhi ya wafanyabiashara wenzangu wakafika pale nyumbani kunisihi niache vile nilikuWa nakifanya, namdhalilisha wife.

Wife akawa analia na kuwazuia vijana wasitoe vitu kwenye Gari. Vijana wanaingiza, kwenye Gari wife anatoa anarudisha ndani. Vijana wanamsukuma pembeni kuwa wao wako kazini asiwaingilie.

Mzozo ukawa mzozo majirani mtaani pale wakajaa, nikawaambia pale,
"Wote Mmemuona huyu shemej yenu, tumegombana tu anasema tugawane mali. Sasa Mimi Sina MDA mchafu wa kwenda kukaa mahakamani kupotezea ili kugawana mali,Nampa kila kitu Hadi kijiko nisikione ndani kwangu, Leo rasmi naanza upya. Kule dukan, fuso tayar lishapakia mzigo wote wa Dukani linaelekea kwao magomeni Kwenda Kufungua duka ukweni.Na Hapa Hii canter mnayoiona itasomba mzigo wote wa vitu vya ndani na kuelekea kwao kule kule magomeni. Kwaiyo Nataka Akafungua duka lake magomeni na akaanze yake maisha mapya magomeni. Sina Muda mchafu wa kugawana Mali na mwanamke Mimi" wote wakabaki na mshangao.

Hatukukawia Sana mwenyekiti wa mtaa akafika na kunisihi tukayaongee ofisini ya mtaa, nikamwambia mzee nakuheshimu Sana Ila tutayaongea tayari nishampatia huyu mwanamke anachokitaka. Hapa niache tu nimalizie hili zoezi langu afu ntakuja uko ofsini tuyaongee.

Mwenyekiti akaanza kuniletea habar za kuniitia polisi nakaidi agizo lake. Basi nae mwenyekiti Tukajibizana mbovu sana, ugomvi karibu uibuke nimchape ngumi maana alianza kuminyooshe vidole. Baadhi ya Watu wakaamulia na kumtoa mwenyekiti eneo Lile akaondoka.

Wife akazidi kububujikwa na machozi anaomba yaishe, kelele zile Ikawa Kama nmeufunga mtaa sasa maana zilikuwa kelele kibao Sana pale. Sijakaa sawa nikaona ile fuso yenye mzigo wa duka inarudi na kusimama pale nyumbani. Kwenye fuso anatoka kijana wa dukani na baba mkwe. Sijakaa sawa taxi nyeupe nayo inafika iko na wale shangazi zake na wife wale walionitukana sana kipindi kile.

Baba mkwe kanifata na kuniomba radhi yaishe, chonde chonde nitulize jazba. Nikamwambia mzee kuwa unawaona hawa walokuja na taxi, walionitukana Sana nilivyokuja ukweni kusuluhishwa. Wakanitusi sifai na kusema niwarudishie binti yenu,Sina msimamo,mzee wa kusemelea nna kiherehere , najipendekeza kwenye ukoo wenu, binti yenu mzuri sana na matusi mengine lukuki.

Sasa mzee wangu nmeamua kutimiza haja yenu, nmemuacha rasmi binti yako na kila kitu hapa nampa Kama unavyoona ili akaishi kwa amani. Tena nampa mbele ya umati huu mtaa mzima unashuhudia Ili mbeleni uko Asije Sema nimemtelekeza, mimi ni katili Sana Kama shangaz zake walivodai.

Umati wote ule ukawageukia wale shangazi zake na mzee wao waliulizia ilikuaje. Ikabidi kuwasimulia matus yote na kejeli zote nilizotukanwa ukweli siku ile nilipofata suluhu.

Umati ule ukawa unawashangaa na kuwanyooshea vidole wale wakwe zangu, inakuaje mkwe wao anakuja wayazungumze kistaarabu mnamtukana matusi, kinachotokea Hapa mkwe wenu msimlaumu, mmeyataka weyewe na mmejidhalilisha Kama familia.

Baba mkwe akasema chonde chonde yeye hakuepo siku ya matusi, nisimjumlishe tuyaongee. Nikamwambia mzee Mimi hatuwezi kuongea chochote kama nawaona Hawa hapa walonitusi matusi ya nguoni mbele yangu. Ikabidi waambiwe warudi kwenye Taxi yao na kuondoka eneo Lile. Maana Hali ya hewa ishachafuka.

Wife akabaki analia machozi Hadi kamasi, kapiga magoti mbele ya umati kumuomba baba ake msamaha kakosea yaishe. Baba ake kwambia hajamkosea yeye kanisekosea Mimi.
Kaja anatambaa anaomba msamaha yaishe nnachofanya namdhalilisha yeye na familia yake pale. Amekiri makosa yake yote tuanze upya. Nikasema HAPANA Hapa mpk kieleweke.
super story
 
IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.

Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.

Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.

Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.

Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.

Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .

Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.

Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.

Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.

Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.

Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.

Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.

Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.

TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.

Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani na Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai tena kuuza duka langu lolote.

Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake, Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU. wengine ni salamu TU,kila mtu kivyake.

Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatulia akawa mcha mungu na MKE mzur Sana.[emoji1431]

Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material mama wa watoto wangu[emoji4]

Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. Michepuko wote nilonao, vichwa maji tupu, mamaJ inclusive.

KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae, Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na alisaisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]

SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA kingine KILICHONIFANYA NIJIVUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]

ASANTENI SANA WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######

NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai talaka wagawane Mali.

NAWASILISHA[emoji1431]
Mimi siku mke wangu naye akidai tuachane na tugawane hii biashara yangu ya majeneza ntamuachia yote tena nakodi fuso kupeleka mzigo wote kwa mshua wake !(sipendagi ujinga)
 
 Masikini...
Huyo dada atajuta maisha yake uote!!

Au labda kuna wake ambao huhisi hela zitaishia kwa michepuko ndio maana huamua kuzifuja.
Acha kabisa omba yasikukute yanauma Sana
Ni upuuzi tu wa mke kaua Mme kirahisi tu Kwa tamaa
 
Mkeo mpuuzi sana kwanza alikukuta tayari una mali hivyo kuzaa nae mtoto mmoja haikua tiketi ya kutaka kugawana mali pasu kwa pasu. Aliziogopa mali zote ulizompa ghafla sababu hakua na akili ya kuziendekeza zaidi ya kushikiwa na ndugu tu
 
Hakika nimejifunza sana,Ahsante kwa ku share story inafundisha,kuelimisha na kukumbushana.
 
Sio kila kitu cha kumshirikisha mkeo, utaumia.
 
IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.

Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.

Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.

Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.

Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.

Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .

Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.

Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.

Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.

Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.

Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.

Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.

Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.

TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.

Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani na Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai tena kuuza duka langu lolote.

Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake, Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU. wengine ni salamu TU,kila mtu kivyake.

Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatulia akawa mcha mungu na MKE mzur Sana.[emoji1431]

Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material mama wa watoto wangu[emoji4]

Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. Michepuko wote nilonao, vichwa maji tupu, mamaJ inclusive.

KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae, Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na alisaisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]

SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA kingine KILICHONIFANYA NIJIVUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]

ASANTENI SANA WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######

NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai talaka wagawane Mali.

NAWASILISHA[emoji1431]
Wewe jamaa ni MUONGO SANA.
 
Yaan unasoma kama unaangalia [emoji327] movie kuna sehem unakaza meno kwa nguvu kuna sehem unajitingisha yaan kasheshe tupu.

Yaan ni taahira au bwege pekee ndio anaweza kupokea mali zile. Ila najiuliza wakat kaka mdg wa mke alipokuwa anatajirishwa na dadake yeye baba mkwe alikuwa haoni? Maana vitu vingine kama Mungu anapanga na anawapiga wengine upofu kwa muda wasilione ili somo lake litimie.. Pokea high 5 DP..!
You blew it...
 
Kumbe ule ugomvi uliozuka kipindi kile nikiwa chaliii ulikuwa wa kwenu...,

Kusema ukweli mm nilipewa baadhi ya vituu na jamaa mmoja hivi alikuwa anapakia mizigo nivifiche alivyokuja kuchukua akinipa buku kila mtu akafa kivyake[emoji23][emoji23][emoji23]
 
NIMEIOENDA SANA HII...BORA KUIAMBIA NA JAMII IKAJUA. KWAMBA NAANZA UPYA MAISHA YA SONGE ILA BEBA KILA KITU
 
Hahahah kumbe ndomana una mchepuko mama j,huyo mama H ni kimeo na nusu😅😅atakuzalia majike yenye tabia zake
 
Kwa sisi Vijana ambao bado hatujafunga ndoa Unatufundisha vitu Muhimu sana Mzee . Ubarikiwe kaka endelea kushusha nyuzi za kuelimisha kama hizi mzee wa posho ya meza Nakubali sana
 
Habar wakuu,

Kwanza niseme TU kisa hiki ni Cha miaka mingi ya nyuma sn ilopita ya ndoa yangu na MKE wangu MAMA G.
Kiukweli miongoni mwa ndoa zilizopita misukosuko mingi miaka 5 ya kwanza ya kwangu naweza kusema ilikua mojawapo.

Misukosuko hii nashkuru iliweza kutujenga imara mpk Sasa naweza kusema sijutii kuoa na naweza kusema nmebahatika kupata MKE Bora kabisa maishani, yaliyopita Si ndwele. Tugange yaliyopo na yajayo.

Anyway,
Nawaletea kisa Cha misukosuko ya ndoa yangu ambapo MKE wangu baada ya ugomvi mkubwa alidai talaka na kutaka tufuate sheria ili tugawane Mali, sema nilichomfanyia nilimnyoosha alijuta na hatosahau maishani mwake na mpk leo Hata tugombane vipi.

Kauli ya "TUGAWANE MALI" ilikoma na hawezi Tena kurudia kuitamka Tena.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]Nitarudi
 
Back
Top Bottom