Mke ametoroka, nami sitaki kuishi naye tena. Sheria inasemaje?

navache

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
499
Reaction score
368
Kama mada ilivyo hapo juu. Ameondoka huku akiacha maneno mengi kama vile kutishia kuniua na kwamba hanihitaji tena. Kwa hatua aliyoifikia nami sihitaji kuwa naye tena. Ikiwa nitahitaji talaka rasmi, sheria inasemaje? Naomba msaada kwa wajuzi wa sheria maana nitahitaji kutafuta mke mwingine na sitaki migogoro isiyo ya lazima huko mbeleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
waambie wazazi wake kwamba mtoto wao kakimbia akipata matatizo unakuwa sehemu salama zaidi maana bila hivyo wao wanajua yupo kwako ila lazima uweke wazi hayo matatizo mliyokuwa nayo.
 
Dah watu wanabadilika sana, Mliwahi kuitana Sweetheart, Dear, Bae xoxoxoxoxoo halafu ghafla mnafikia kutaka kutoana Uhai?? MUNGU awabariki
 
Pole sana mkuu hii ndo dunia ilivyo. nakushauri tumia busara sana katika utatuzi wa suala linalokukabili kwa wakati huu.
 
Sheria ya ndoa ya mwaka71 na vifungu vyake vinaeleza kuwa talaka inaweza kutolewa na ndoa kutangazwa kuwa imevunjika endapo mmoja wenu atakuwa eidha amefumaniwa bila kificho au kumuambukiza mwenzie magonjwa ya zinaa kwa makusudi au kumfanyia mwenzako vitendo vingine vya ukatili visivyovumilika. Nakushauri fanya utaratibu umtafute halafu kati ya hayo niliyotaja kama kuna mojawapo kalifanya basi unaweza kutoa talaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

 
waambie wazazi wake kwamba mtoto wao kakimbia akipata matatizo unakuwa sehemu salama zaidi maana bila hivyo wao wanajua yupo kwako ila lazima uweke wazi hayo matatizo mliyokuwa nayo.
Nashukuru. Nilitoa taarifa kwa serikali ya mtaa na waliwataarifu wazazi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah watu wanabadilika sana, Mliwahi kuitana Sweetheart, Dear, Bae xoxoxoxoxoo halafu ghafla mnafikia kutaka kutoana Uhai?? MUNGU awabariki
Ni kweli tunabadilika sana. Tena siyo uhai wangu tu, bali pia katishia wa watoto na kwamba akifanikisha, atajiua na yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru sana mkuu kwa kunifumbua macho kiasi chake. Kama ungeniruhusu nikutembelee pm ningebarikiwa zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole mkuu jitahidi upate ushahidi wa kutishiwa maisha iwe kama ushahidi .......ila kuwa makini inawekuwa amamemaanisha mkuu narudia tena kuwa makini
 
Pole kwa kutishiwa kuuwawa Ww katoe taarifa police baadae katoe taarifa kwao ikiwezekana toa na taraka mbele ya wazazi wake na viongozi baadae fanya unavyotaka kuoa au kuijpangakwanza ila ukianza kuhangaika kutafta kumbuka huyo sio mbuzi ni mtu mzima anaejielewa ukihangaika kutafta utapoteza pesa bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…