MKE AMUUA MUMEWE

MKE AMUUA MUMEWE

luangalila

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
6,346
Reaction score
6,928
Ni huko Murang'a mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 47 anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumuua mume wake kwa kucharaza mapanga mpaka mauti ukamfika. HII ni mwendelezo wa vitendo vya mauaji baina ya wapenzi au wana ndoa huko nchini Kenya.
Majirani mmjenge gereza mupya maana watu wanazidi kuuana tu last week tulisikia ya ivy, mara kule pwani university, mara akina wangui, hatuja kaa vizuri tunasikia na hiki kisa cha murang'a

source:
 
Tutakusaidia pia kuangaza ya Tanzania japo huko media zenu huwa kwenye usingizi hawaripoti mambo kama haya, wao wamekomalia kuonyesha mambo ya Diamond na Wasafi.

Bibi Anayetuhumiwa Kuua Mwanafunzi Auawa na Wanachi Wenye Hasira
Tukio lisilo la kawaida limetokea Wilayani Muleba Kata ya Kishanda Mkoani Kagera ambapo mtoto mwenye miaka saba Ismail Hamisi ambaye alipotea tangu April 5 akitokea shule na jana usiku amekutwa kwenye shamba la bibi mmoja akiwa amefukiwa kwenye shimo tayari ameshapoteza maisha.Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchomo moto akiwa ndani ya nyumba yakeKamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mtoto huyo alitoweka April 5 mwaka huu alipoondoka nyumbani kwenda shule, lakini hakuonekana tena hadi mwili wake...


http://www.magazetini.co.tz/news/bibi-anayetuhumiwa-kuua-mwanafunzi-auawa-na-wanachi-wenye-hasira
 

MWANACHUO AUAWA KILIMANJARO Mwanafunzi wa utabibu katika Chuo Faraja, ameuawa na mfanyabiashara ndogondogo wa kimasai baada ya kuibuka ugomvi kwenye manunuzi ya pete. Video Kamili utaipata kwenye chaneli yetu ya YouTube | @AzamTv #AzamTVApp #AzamTVUpdates

The media could not be played.
 
Mgogoro wa Wakulima na Wafugaji, Mzee Auawa kwa Mkuki!
PWANI.jpg

Mgogoro wa Wakulima na Wafugaji, Mzee Auawa kwa Mkuki!
March 27, 2019 by Global Publishers
MZEE mmoja aliyetambulika kwa jina la Visu Urembo (80), amefariki dunia baada ya kuchomwa mkuki kwenye sehemu ya ubavuni mwa mwili wake, katika mgogoro wa wakulima na wafugaji, uliotokea Lukenge, tarafa ya Ruvu, Kibaha Vijijini, mkoani Pwani.
Akithibitisha kutokea kwa tafrani hiyo, kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP, Wankyo Nyigesa alisema tukio limetokea jana, Jumann, Machi 26.
Alieleza, mzee Urembo kabla ya kufikwa na umauti alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi, ambapo baadae alikimbizwa hospital ya Tumbi kwa matibabu zaidi lakini kabla ya kupatiwa matibabu madaktari waligundua kuwa umati umeshamfika.
Hata hivyo, Wankyo alibainisha, wafugaji hao waliingiza mifugo yao (ng’ombe) kwenye bwawa linalotumika katika shughuli za binadamu ikiwemo kunywa, kufulia, kupikia na kadhalika.
“Kwa kuona hivyo ndipo wakulima wakaenda kwa mhemko kuwazuia watoe ng ‘ombe wao lakini wafugaji walianzisha tafrani, ambapo walianza kurusha mikuki ,vitu vyenye ncha kali na kusababisha kifo cha mzee huyo na kujeruhi watu watatu,“ alifafanua Wankyo.
“Polisi tulifika eneo la tukio alfajir March 27 ,na kutuliza tafrani hiyo na sasa hali ni shwarii”.
Wankyo aliwataja waliojeruhiwa ,kuwa ni pamoja na John Kisukari Urembo (50) ambae ni mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Lukenge.
Wengine ni mtendaji wa kijiji cha Lukenge Maximillian Evarist (34) na Adam Onesha ambae ni mwenyekiti wa kamati ya maji kijijini hapo. Kamanda huyo alitoa wito, jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepukana na madhara kama hayo yaliyojitokeza.
Wankyo,alisema kila mtu katika nchi hii ana haki ya kuishi, kutumia ardhi hii, na hakuna mwenye mamlaka juu ya mwenzie ila inabidi kuacha kuingiliana mipaka iliyotengwa kwa ajili ya kundi jingine ili hali kukabiliana na migogoro hasa ya wakulima na wafugaji”alisisitiza Wankyo.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyataka makundi hayo yaheshimiane na kujenga upendo badala ya kujiona kundi moja ni zaidi ya kundi jingine.
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

https://theworldnews.net/tz-news/mgogoro-wa-wakulima-na-wafugaji-mzee-auawa-kwa-mkuki
 
Kenya watu wanauana sababu ya MAPENZI that is my point of view .....ushawahi sikia bongo land watu wanaua sababu ya PENZI kama mmechokana mnaachana tu kimya kimya alafu usisomeshe mtoto wa mtu wakati ww sio baba yake WAKE UP Young men in Kenya
 
Asilimia 70 ya madem wa kenya Wana ruka ukuta kutokana na tamaaa

Ova
 
Back
Top Bottom