huwa kuna taratibu ndefu sana na sasa serikali inataka ipunguze talaka kwa kutotota talaka
Kukaa na mtu anaetaka kuondoka ni mtihani mkubwa sana,na ni hatari sana,
Kukubali kuingia mtegoni na kumuacha bila utaratibu ni Bomu linaloweza kulipuka muda wowote mbeleni,
Kufuata utaratibu kisheria pia ni kazi sana kuishawishi mahakama ikuamini unachoomba,
Nimepitia maisha haya kwa matendo,najua mzigo uliopo,
Imenisumbua kiasi kila nilichokuwa nafanya kilikuwa gunia la miiba,
Lkn siraha pekee iliyoniokoa ni kuikubali hali maana anaetaka kuondoka huwa anafanya visa kusudi ili aachike,ukikosa utulivu unaishia jela,
Inataka utulivu sana,na umakini sana,bila kusahau kukusanya kila aina ya ushahidi,kitachokunusiru ni Mungu akuwezeshe utulivu ndo utapata hata nafasi ya kksanya ushahidi,
Lkn kuondoka na kuacha kila kitu siyo suruhu japo watu hudanganyana kuwa ndo njia sahihi,unaweza dhani unakimbia tatizo ukawa unaliahirisha tu,na ukitaka kupata amani usiweke kisasi,msamehe,muone siyo adui,mtakie mema,usiwaze kuacha watoto na usimdhurumu kitu halafua acha sheria iamue na uwe tayari kupokea matokeo yyte,
Nina mwaka sasa tangu linikute na nikapita,ninaishi na wanangu japo ni mzigo lkn kuna nafuu