Mke anataka kuondoka, bila kufukuzwa..kuna umuhimu wakugawana mali

Mke anataka kuondoka, bila kufukuzwa..kuna umuhimu wakugawana mali

huwa kuna taratibu ndefu sana na sasa serikali inataka ipunguze talaka kwa kutotota talaka
kivip mkuu,lakini kuna sabb zile ambazo hakuna jinsi, mfano magonjwa yà zinaa HIV ,Uhanisi nk hapo pakoje?
 
Kukaa na mtu anaetaka kuondoka ni mtihani mkubwa sana,na ni hatari sana,
Kukubali kuingia mtegoni na kumuacha bila utaratibu ni Bomu linaloweza kulipuka muda wowote mbeleni,
Kufuata utaratibu kisheria pia ni kazi sana kuishawishi mahakama ikuamini unachoomba,
Nimepitia maisha haya kwa matendo,najua mzigo uliopo,
Imenisumbua kiasi kila nilichokuwa nafanya kilikuwa gunia la miiba,
Lkn siraha pekee iliyoniokoa ni kuikubali hali maana anaetaka kuondoka huwa anafanya visa kusudi ili aachike,ukikosa utulivu unaishia jela,
Inataka utulivu sana,na umakini sana,bila kusahau kukusanya kila aina ya ushahidi,kitachokunusiru ni Mungu akuwezeshe utulivu ndo utapata hata nafasi ya kksanya ushahidi,
Lkn kuondoka na kuacha kila kitu siyo suruhu japo watu hudanganyana kuwa ndo njia sahihi,unaweza dhani unakimbia tatizo ukawa unaliahirisha tu,na ukitaka kupata amani usiweke kisasi,msamehe,muone siyo adui,mtakie mema,usiwaze kuacha watoto na usimdhurumu kitu halafua acha sheria iamue na uwe tayari kupokea matokeo yyte,
Nina mwaka sasa tangu linikute na nikapita,ninaishi na wanangu japo ni mzigo lkn kuna nafuu
Ndugu pole mimi nna mwaka wa pili huu bado naangaika na ustwi ni shida kweli kweli ustawi wa jamii ni wasubufu mno alafu mwisho wa siku bado mahakama ndio jibu la mwisho kikubwa ni kutokukata tamaa tu
 
hata akienda huko ustawi wa jamii hakuna watakachoweza kulazimisha ufanye na una uwezo wa kukataa maana huwezi fungwa
 
Kuna bwana ilimfika hali kama hiyo, aliondoka na begi lake la nguo tu na pesa kidogo mfukoni. Alimuachia mke watoto, nyumba na kila kitu. Kitu ambacho mke hakufahamu ni kuwa rizki aliondoka nayo mwanaume.

Baada ya miaka miwili alikuwa na biashara iliyoshamiri katika mkoa aliohamia. Mali inatafutwa lakini amani na upendo haviwezi kununuliwa.
Umetoa point nzuri sana mkuu,barikiwa sana
 
Hata aking'ang'ania we lazimisha muorodheshe mali zote anazotaka. Mpe aende zake. Mali zote hizo mahakama itaitisha ili kuzigawa na utapata kilicho chako. Mwache asepe zake.
 
Back
Top Bottom