Mke anayedaiwa kupanga kumuua mumewe kortini.

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
janeth-2.jpg

Janeth Jackson anayedaiwa kula njama za kumuua mume wake, Simon Jakson na mtoto wake wa kambo.

index.html

Kwa ufupi
"Ni mke wa mfanyabiashara maarufuwa Tanzanite Arusha, anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe na mtoto wa kambo wa kiume anayeishi Bukoba."

Arusha. Mwanamke anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wa mume huyo, amepandishwa mahakamani akiwa na mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo.
Janeth Jackson (32), mkazi wa Moshono, Arusha na Novatus Elias, walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha /Arumeru, DevothaKamuzora, wakisomewa makosa mawili ya kula njama ya kutaka kumuua Simon Jackson ambaye ndiye mume wa Janeth.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Edna Kasala, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wote walitenda kosa la pili la kula njama na kutaka kumuua Desderi Sabas, ambaye ni mtoto wa mke mwingine kwa mume huyo anayeishi Bukoba, mkoani Kagera.
Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu Mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kasala iliomba mahakama kuwanyima dhamana washtakiwa, kwa sababu watuhumiwa wengine wawili wanatafutwa hivyo na upelelezi haujakamilika.
Alidai kutokana na uzito wa tuhumahizo, maombi hayo ya kuwanyima dhamana washtakiwa yameambatana na hati ya kiapo ya Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha.
“Mheshimiwa tunafahamu kwamba dhamana ni haki ya washtakiwa kikatiba, lakini kutokana na mazingira ya kesi hii kuwa magumu,tunaomba dhamana isitolewe ili kuwatafuta watuhumiwa wengine wa kesi hii,” alidai Kasala.
Kwa upande wake,Wakili wa utetezi, Fidelis Peter, alipinga maombi hayo na kutaka mahakama itoe dhamana kwa washtakiwa kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kwamba hilo ni kosa lao la kwanza.
Sababu nyingine ya kupinga maombi ya upande wa mashtaka, ni kwamba washtakiwa wanaweza kuvuruga upepelezi wakiachiwa siyo za msingi kwani ni watu wanaoaminika katika jamii.
“Mheshimiwa sababu za kuwanyima dhamana washtakiwa hazina uzito wowote, pia mshtakiwa wa kwanza (Janeth) anamtoto wa miezi sita na tangu akamatwe alhamisi iliyopita hajamwona wala kumnyonyesha hivyo anastahili kupewa dhamana,”alidai Wakili Peter.
Hata hivyo, baada ya kusikiliza maombi ya pande zote mbili, Hakimu Kamuzora, alikubaliana na maombi ya upande wa mashtaka nakuamuru watuhumiwa wapelekwe mahabusu hadi Agosti 5, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Katika kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi jijini hapa, inadaiwa Janeth alitaka kumuua mumewe ambaye ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite na mwanaye wa kiume, ili arithi mali na utajiri alionao mfanyabiashara huyo.
Akiwa amejifunika uso muda wote alipokuwa mahakamani, Janeth alionekana kuwa na mawazo mengina macho mekundu kwa sababu ya kulia baada ya njama hizo kugonga mwamba.
Awali kabla ya kukamatwa kwa mwanamke huyo, taarifa zilieleza kuwa, mwanamke huyo alitumia fedha nyingi kulipa majambazi waliotakiwa kutekeleza tukio hilo lakini mmoja wa majambazi hao aliamua kuvujisha siri hiyo polisi iliyofanikisha kukamatwa kwa wahusika kabla ya kutenda mauaji hayo.
Mume wa mwanamke huyo alinukuliwa awali akisikitika na kuhoji kwa nini mke huyo alifikia kupanga hilo.

© 2013 MCL
 
aka kakabila ka wake watoa roho kwa ajiri ya mali katasababisha mabinti zao kukimbiwa na wachumba wao kimya kimya
 
Watu wanasema wenye Tabia hizi ni wale wa zamani siyo wa sasa hivi, Kumbe Tabia hii ipo Damuni wacha waoane wenyewe kwa wenyewe, wauane. Ndiyo maana siku hizi kaka zao wanakimbilia kuwaoa waruguru, wahehe na wanyakyusa, wanawaogopa dada zao .
 
Jamani Dada mzuri anamuua mumewe kweli hii dunia noma,tena noma sana
 
Wito kwenu mliooa lile kabila kama mna vijisenti muwe macho
 
Tulishajadili juzi hapa wachaga hasa hasa wamachame a.k.a waPalestina ndo michezo yao wakawa wanabisha...kuoa mchaga ni kifo cha kujitakia kabisa.
 
Mume angekufa, angejishaua kulia na kuomboleza usiku kucha! shetani mkubwa! Baada ya kumaliza msiba angeanza kutesa na viserengeti boys, pepo kabisa huyu!
 
sasa shida yake ni nini mtu kama huyu jamani. kama mume ana mali si yake pia?
 
janeth-2.jpg

Janeth Jackson anayedaiwa kula njama za kumuua mume wake, Simon Jakson na mtoto wake wa kambo.

index.html

Kwa ufupi
"Ni mke wa mfanyabiashara maarufuwa Tanzanite Arusha, anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe na mtoto wa kambo wa kiume anayeishi Bukoba."

Arusha. Mwanamke anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wa mume huyo, amepandishwa mahakamani akiwa na mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo.
Janeth Jackson (32), mkazi wa Moshono, Arusha na Novatus Elias, walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha /Arumeru, DevothaKamuzora, wakisomewa makosa mawili ya kula njama ya kutaka kumuua Simon Jackson ambaye ndiye mume wa Janeth.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Edna Kasala, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa wote walitenda kosa la pili la kula njama na kutaka kumuua Desderi Sabas, ambaye ni mtoto wa mke mwingine kwa mume huyo anayeishi Bukoba, mkoani Kagera.
Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu Mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kasala iliomba mahakama kuwanyima dhamana washtakiwa, kwa sababu watuhumiwa wengine wawili wanatafutwa hivyo na upelelezi haujakamilika.
Alidai kutokana na uzito wa tuhumahizo, maombi hayo ya kuwanyima dhamana washtakiwa yameambatana na hati ya kiapo ya Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha.
"Mheshimiwa tunafahamu kwamba dhamana ni haki ya washtakiwa kikatiba, lakini kutokana na mazingira ya kesi hii kuwa magumu,tunaomba dhamana isitolewe ili kuwatafuta watuhumiwa wengine wa kesi hii," alidai Kasala.
Kwa upande wake,Wakili wa utetezi, Fidelis Peter, alipinga maombi hayo na kutaka mahakama itoe dhamana kwa washtakiwa kwa sababu ni haki yao ya kikatiba na kwamba hilo ni kosa lao la kwanza.
Sababu nyingine ya kupinga maombi ya upande wa mashtaka, ni kwamba washtakiwa wanaweza kuvuruga upepelezi wakiachiwa siyo za msingi kwani ni watu wanaoaminika katika jamii.
"Mheshimiwa sababu za kuwanyima dhamana washtakiwa hazina uzito wowote, pia mshtakiwa wa kwanza (Janeth) anamtoto wa miezi sita na tangu akamatwe alhamisi iliyopita hajamwona wala kumnyonyesha hivyo anastahili kupewa dhamana,"alidai Wakili Peter.
Hata hivyo, baada ya kusikiliza maombi ya pande zote mbili, Hakimu Kamuzora, alikubaliana na maombi ya upande wa mashtaka nakuamuru watuhumiwa wapelekwe mahabusu hadi Agosti 5, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Katika kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi jijini hapa, inadaiwa Janeth alitaka kumuua mumewe ambaye ni mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite na mwanaye wa kiume, ili arithi mali na utajiri alionao mfanyabiashara huyo.
Akiwa amejifunika uso muda wote alipokuwa mahakamani, Janeth alionekana kuwa na mawazo mengina macho mekundu kwa sababu ya kulia baada ya njama hizo kugonga mwamba.
Awali kabla ya kukamatwa kwa mwanamke huyo, taarifa zilieleza kuwa, mwanamke huyo alitumia fedha nyingi kulipa majambazi waliotakiwa kutekeleza tukio hilo lakini mmoja wa majambazi hao aliamua kuvujisha siri hiyo polisi iliyofanikisha kukamatwa kwa wahusika kabla ya kutenda mauaji hayo.
Mume wa mwanamke huyo alinukuliwa awali akisikitika na kuhoji kwa nini mke huyo alifikia kupanga hilo.

© 2013 MCL
Chezea Mchagga weye! Kwake pesa ni bora kuliko uhai wa mtu. Tupilia lupango huyo kwni kama ni mtoto Jackson tafuta mtu wa kumtunza. na huyo jambazi aliyetoa siri asamehewe madhambi yake yote apewe heshima yake.
 
Back
Top Bottom