Mke au mume wako anapojenga kwa siri bila wewe kujua tafsiri yake ni kwamba anajiandaa kuishi bila wewe

Mke au mume wako anapojenga kwa siri bila wewe kujua tafsiri yake ni kwamba anajiandaa kuishi bila wewe

Wanaume wengi wasio na uwezo wa kutafuta mali ndo wana hii kasumba ya kila kitu mke ajue.
Si lazima kila kitu mkeo afahamu. Yule ni mkeo si damu yako. Wakati wowote anaweza kuwa mke wa mwimgine. Tengeneza utaratibu mali zako zisipotee ukifa, watoto wako wazipate.
 
Habari wanandoa na wanauchumba.

Hivi unajua kuwa mwenzi wako anapoamua kujenga nyumba au kufanya jambo la kimaendeleo bila wewe kujua hapo anajiandaa kuishi bila wewe?

Hii dunia ina mambo sana. Unaweza kuona watu wakiishi pamoja wakicheka pamoja na kula pamoja ila mmoja au wote wakaingiwa na ibilisi wa ujinga, tamaa na ufedhuli.

Mtu anaamua ajenge kimyakimya. Tena wengine huwaibia wenzi wao (hujiibia wenywewe) na kwenda kujenga nyumba kwao.
Hii roho ni mbaya kuliko ile roho ya kuchepuka.

Kuna jirani yangu mmoja Mchaga hapa mjini Dar es Salaam ana viwanja 9, huku mke anakijua kimoja tu kati ya hivyo viwanja 9.
Ni ushetani flani hivi,hakuna dhambi yenye malipo mazuri hapa duniani...
 
Habari wanandoa na wanauchumba.

Hivi unajua kuwa mwenzi wako anapoamua kujenga nyumba au kufanya jambo la kimaendeleo bila wewe kujua hapo anajiandaa kuishi bila wewe?

Hii dunia ina mambo sana. Unaweza kuona watu wakiishi pamoja wakicheka pamoja na kula pamoja ila mmoja au wote wakaingiwa na ibilisi wa ujinga, tamaa na ufedhuli.

Mtu anaamua ajenge kimyakimya. Tena wengine huwaibia wenzi wao (hujiibia wenywewe) na kwenda kujenga nyumba kwao.
Hii roho ni mbaya kuliko ile roho ya kuchepuka.

Kuna jirani yangu mmoja Mchaga hapa mjini Dar es Salaam ana viwanja 9, huku mke anakijua kimoja tu kati ya hivyo viwanja 9.

Kama unajua siri za jamaa kiasi hicho basi wewe utakuwa mke mkubwa
 
Sasa huoni kuwa hiyo ni akili[emoji849]
'
JamiiForums-1851747025.jpg
 
unamficha mke au mume ili iweje ilhali mna watoto.
Mke atapata haki yake na watoto haki zao. Si lazima haki za watoto mke azijue wakati unazitengeneza. Utaratibu wa kuhakikisha mali zinawafikia wanao ukifariki ghafla ni wa muhimu.
 
Wanaume wengi wasio na uwezo wa kutafuta mali ndo wana hii kasumba ya kila kitu mke ajue.
Si lazima kila kitu mkeo afahamu. Yule ni mkeo si damu yako. Wakati wowote anaweza kuwa mke wa mwimgine. Tengeneza utaratibu mali zako zisipotee ukifa, watoto wako wazipate.
Hahahaha sasa watoto zako watazipataje bila mama yao kujua? Mama kujua ina maana watoto pia watajua, watoto kujua ina maana pia mama lazima ajue....! Ukiamua kumficha mama ina maana na watoto umewaficha
 
Mwanadamu hujisahau sana kuwa maisha ya duniani hapa ni mapito. Fahari zote zinapita. Ikimaanisha mwanadam ndiye anayepita. Ni kitambo kidogo tu cha miaka isiyozidi 70 lakini binadamu hujihangaisha na hila kama vile vitu anavyopata kwa hila ataambatana navyo akiondoka. Ni roho mbaya ya uchoyo na urafi tu usio na maana.

Unaweza kuona kuna majumba mengine yamejengwa hayakukamilika na yanabaki hivyo hivyo miaka mingi unashangaa, mmiliki huwa haji kuangalia jengo lake? Kumbe alishakufa na mke au familia haikujua kuwa ana jengo. Linabaki hivyo.

Maisha mapito, hila hazina maana.
 
kuna nyumba ya familia, nyumba yako na nyumba yake, yote yanawezekana
 
Ndo ivo,hakuna namna.Ila kuna uncle wangu kapata nyumba ya buree...kutokana na mjeshi kumficha mkewe Mali zake na kumthamini rafiki yake.Kafa na kende zake mke hajui kama mume alikuwa na jumba huko.
Nimewahi kusikia hii pia

Jamaa alimficha mkewe akamjulisha rafiki, alipokufa jamaa kajimilikisha nyumba na hajui ndugu za jamaa yake ikabidi aifanye yake
 
Wanaume wengi wasio na uwezo wa kutafuta mali ndo wana hii kasumba ya kila kitu mke ajue.
Si lazima kila kitu mkeo afahamu. Yule ni mkeo si damu yako. Wakati wowote anaweza kuwa mke wa mwimgine. Tengeneza utaratibu mali zako zisipotee ukifa, watoto wako wazipate.
Labda uweke mazingira ndugu unaowaamini wazijue

Lakini hebu tuwe na ubinadamu, mke kukupa haki ya ndoa, kukufulia, kukupikia, kukuuguza ukiumwa, saa zingine ni mlevi mbwa unarudi na matapishi anafua nguo, au unapenda totozi unapiga mambo huko mtaani dada wa watu hajui anakuja kufua janaba zako

Mimi huwa nafikiria mengi nahitimisha kwamba acha aje afaidi tu mwenyewe

Kuona mwanamke si nduguyo eti atafaidi nafikiri ni roho ya kibinafsi
 
Nimewahi kusikia hii pia

Jamaa alimficha mkewe akamjulisha rafiki, alipokufa jamaa kajimilikisha nyumba na hajui ndugu za jamaa yake ikabidi aifanye yake
Hadi huruma naionea hiyo familia
Watoto waishi maisha ya gheto huku mzazi umeacha nyumba.
Huyo rafiki angekuwa mwema angeijulisha familia yake baada ya kifo
 
Labda uweke mazingira ndugu unaowaamini wazijue

Lakini hebu tuwe na ubinadamu, mke kukupa haki ya ndoa, kukufulia, kukupikia, kukuuguza ukiumwa, saa zingine ni mlevi mbwa unarudi na matapishi anafua nguo, au unapenda totozi unapiga mambo huko mtaani dada wa watu hajui anakuja kufua janaba zako

Mimi huwa nafikiria mengi nahitimisha kwamba acha aje afaidi tu mwenyewe

Kuona mwanamke si nduguyo eti atafaidi nafikiri ni roho ya kibinafsi
Mwanaume mwenye tabia hizo hana mali za kumficha mke.
 
Mkuu ndoa zina mengi,,, usione watu wanfanya hvo..

Kuna wengine wanafanya hvo kwasababu wakishirikisha wenzi wao wanakuwa kama kikwazo..
Kwenye maendeleo huwa kuna migogoro mingi sana kwasabu kila mmoja anaweza kuwa na ndoto zake tofauti na interest... So mnaweza ishia kwenye mjadala na msifanye lolote so ni bora wakati mwingine uanze then mwenzako akija kujua akute Gari imeshawaka.....
 
Mimi najaribu kufikiria mazingira wezeshi kufanya hayo bila mmoja kujua

Najua kwa namna yoyote iwe mleta ugali nyumbani ni mume, mke au wote wawili inawezekanaje kufanya jambo mwingine asijue?
Najua panaweza kuwa na pato la ziada ambalo mmoja hajui lakini ugumu utamuwia penye kufanya hilo jambo lake na mwingine akitaka mfanye la familia

Yaani kama mume anajenga kwa siri na wewe mwanamke ukikomaa mjenge ya familia hapo ndio utajua kuna kitu, atabishaje? Akibisha utambana, akikubali jambo lake litafeli

Najaribu ku-imagine mko kwenye ndoa na huwa hamzungumzii kabisa maendeleo ya familia, hapo mtu atajenga kwa siri lakini kama mna plan za pamoja mtu anajengaje?
Au tuseme labda mlishajenga mnayoishi kwahiyo hamzungumzii mambo makubwa tena hali inayompa mtu mwanya wa kujenga kwa siri? Nyie mtakuwa wafu? Hata kama mmeshajenga bado kuna plan zaidi

Maswali yote haya najaribu kuelewa inawezekanaje mmoja akajenga bila mwingine kujua
Inawezekana kabisaaa na sio kujenga tu na mambo mengine yanafanyika bila kushirikishana uku mkishirikishana vichaaaache
 
  • Thanks
Reactions: T11
Mwanaume mwenye tabia hizo hana mali za kumficha mke.
Wapo wana mimali na kila umiliki wake kaandika jina la mke....tena matajiri kabisa.....mwanaume anayemilikisha ndugu mali badala ya mama wa watoto wake aiseee hayajamkuta
 
Wapo wana mimali na kila umiliki wake kaandika jina la mke....tena matajiri kabisa.....mwanaume anayemilikisha ndugu mali badala ya mama wa watoto wake aiseee hayajamkuta
1 katika 1000. Halafu kupata mke wa hivyo ni 1 katika 10000
 
Hahahaha sasa watoto zako watazipataje bila mama yao kujua? Mama kujua ina maana watoto pia watajua, watoto kujua ina maana pia mama lazima ajue....! Ukiamua kumficha mama ina maana na watoto umewaficha
Inawezekana vizuri tu watoto wako warithi mali zako ambazo ata mke wako alikuwa hazijui.
Ukiwa serious kutafuta mali za kurithisha vizazi na vizazi basi ni muhimu na wewe ukajielimisha njia ya kuzilinda hizo mali.
 
Back
Top Bottom