Mke bora na heshima kwa mwanaume

Mke bora na heshima kwa mwanaume

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Ni ukweli usiopingika mwanamke mzuri wa sura na umbile ni ndoto ya kila mwanaume,tena akiwa smart kichwani na elimu kwa mbali ndiyo kabisa.

1. Unajiamini kumtambulisha popote na kwa yeyote huku ukikenua meno yote na kujipiga kifua kwakuwa upo na mtu unayempenda kwa dhati na unaweza kuambatana naye popote.yaani CV yake imeshiba mno

2.Majukumu ya familia yanapungua kwasababu,anakuwa na kazi yake hivyo Kuna asilimia mambo mengi anarekebisha na salary yako Ina balance.(Bills za maji,umeme na ada kwa watoto anaweza kutatua bila wasiwasi

3.Uelewa wa mambo,hakuna kitu kizuri kuwa na mke ambaye anajua Dunia ,siasa na mambo yanaendaje.

Siyo mko sebuleni mnaangalia taarifa ya habari namna treni ya SGR ilivyokwama baada ya bundi na ngedere kufanya yao, halafu anakuuliza,
Kwani hii treni ni ya lini?
Iliishiwa mafuta?
Na kwanini waweke mafuta kidogo hawakujua KM na umbali waendako?

Mke hamjui mkuu wa wilaya yenu,huko ni mbali mno mkuu wa kituo wenu wa polisi hamjui,asalaaalee!!!

4R za Rais hajawahi kusikia,anachojua yeye Rais Samia ni Rais ila anashindwa kutofautisha vyeo Cha Philip Mpango na Kassim Majaliwa,
Haujui mradi wowote nchini ,anachojua ni kupanda mwendokasi na kufika alikokusudia

Halafu kabatini kwake kajaza mafulana yameandikwa "Mama anaupiga mwingi"

4. Mama bora atakayeheshimika na watoto wake, alooooh hakuna mtoto anayemdharau mzazi , baba au mama waziwazi,ila Kuna namna kimoyomoyo watoto wetu wanadharau sana haswa kwa wamama golikipa.

5. Mshauri wa mambo pindi yakienda mrama.
Baba ni kichwa cha familia lakini Kuna muda utakwama tu ,kichwa kinauma na huhitaji ushauri toka mbali,
Mikopo, insurance,madeni TRA,ada za watoto na mengine mengi,hapa mwanaume unahitaji tulizo.

Siyo sauti nzuri ,mahaba kitandani na uzuri wa shanga kiunoni na viuno sita vya juu na chini la hasha .

Hapa unatakiwa ushauri wa mtu mmoja naye ni mke anayetambua changamoto anazopitia mume wake ili kuijenga familia ,huku akiwa na ushauri chanya kiasi cha mtu presha inashuka.

6.Mwanamke anayekusikiliza na kukuheshimu,tena kwa mbaali awe kama anakuogopa licha ya wadhifa aliokuwa nao kazini kwake,
Sikatai anaweza kuwa anakucheat lakini iwe kwa heshima na usijue asilani,kitendo cha kukubali msaada wa lifts kutoka kwa staff mwenzie halafu analetwa hadi kwako hizo ni dharau,hata kama usafiri wake umeharibika na kuamua kupeleka gereji,basi mke achukue Bajaj, Uber,taxi na namna nyingine ya usafiri siyo kuletwa mpaka getini kwaki na jitu hulijui halafu uaminishe ni rafiki yake wanaheshimiana,halafu ana usafiri wa gharama kuliko wewe haijakaa poa


NB: hakuna mkamilifu chini ya jua,ndoa ni uvumilivu na subira nje ya hapo unaweza kuwa single miaka yako yote mpaka Mungu atakapokupenda zaidi
 
Back
Top Bottom