Mke hata kama ana kipato, ni haki yake kisheria kutunzwa na mume wake

Mke hata kama ana kipato, ni haki yake kisheria kutunzwa na mume wake

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Mke kuwa na uwezo kifedha haimpi jukumu la kumtunza mume na familia.

Je, unajua kwamba mke kuwa na kipato kikubwa kuliko mume wake hakumaanishi moja kwa moja kuwa amechukua jukumu la kisheria la kumtunza mume na familia? Kwa mujibu wa Kifungu cha 63(a) cha Sheria ya Ndoa, Sura ya 29, mume ana wajibu wa kumtunza mke wake kwa kumpatia mahitaji muhimu ya maisha kulingana na uwezo wake.

Kwa upande mwingine, Kifungu cha 63(b) kinaweka wajibu kwa mke kumtunza mume wake pale ambapo mume hawezi kujipatia riziki kutokana na ulemavu wa mwili au akili, na mke ana uwezo wa kufanya hivyo. Hivyo, mke kuwa na kazi, biashara, mshahara mkubwa au mali nyingi hakumwondolei mume wajibu wake wa kisheria wa matunzo.

Hata hivyo, sheria haimzuii mke kuchangia mahitaji ya familia kwa hiari, na masuala ya matunzo ya watoto yana wajibu wake tofauti chini ya sheria. Kumbuka: Mchango wa hiari wa mke katika familia si sawa na wajibu wa kisheria wa kumtunza mume.

Tukimaliza kuyatafakari haya tuendelee kutafakari na utekwaji wa Twaha Mwaipaya wakuu😀🤔 🤔

 
Hakuna kitu kama hiko! Labda kama unaamini vitabu vya alifu elelaulela au vya abunuasi!
 
Kama tafsiri ya kutunzwa si kwa mujibu wa kipato cha mke, ni kwa mujibu wa kipato cha mume swali ni Je, ni mwanamke wa Dunia ipi ambae ataacha kutembelea V8 analolimudu ili atembelee vits ambayo mumewe anaimudu? Au ataacha piza anayoimudu ili ashindie kande anazozimudu mumewe? Au ataacha wigi analolimudu ili anyoe sababu mumewe anamudu kumnyoa?
 
Mbona ni rahisi sana kuitumia hela ya mwanamke!
Mimi sipati shida ya kukopa hela yake, ikipita miezi 3 sijamkopa anashangaaga "kulikoni!",ananikopesha kwa lazima.
Vitu vingi vinavyo muhusu amezoea mimi ndiye mnunuaji, hela yake haina matumizi makubwa.

Kumbuka:
Ili mke akuamini hakikisha umemtengeneza amekuwa rafiki yako.
Urafiki wa mke na mme hakuna hela ya siri.
 
Hizi kelele utazisikia sana wale ambao wote wanajiweza ila uchumi wa kati wengi wanasaidia sana majukumu ya familia. Ni uzoefu wangu tu binafsi, sijafanya utafiti wowote.
 
Tuseme sawa sasa Je pesa ya mwanamke ni ya kazi gani katika familia?
 
Ila wanume bana, kuna dada mmoja kila siku analalamika, wanafanya kazi ofisi moja na mmewe ila mwanaume pesa zake anaficha anachochangia ni kodi ya nyumba tu, chakula, ada za watoto na malipo ya msaidizi wa kazi hatoi hata sumni! Juzi juzi kakopa ela kaenda nunua gari kabaki na kama 10m na akazificha ndani ila hatoi senti kwaajili ya familia sijui shida inatokea wapi!
 
Sheria Ina makengeza,haiwezekani mume mwenye mshahara mdogo kuliko mkewe atunze watoto na mume wakati si mke aliyetoa mahari.Kwene mimbari waliahidi kuwa wamoja ktk shida na raha
 
Shankupe uzuri wanja,sijui kwanini nikiona wanawake dizain hiyo wakiwa wanazungumza mambo siriaz ya kimaisha nawaona kama kipande cha tofali!
 
Back
Top Bottom