Baada ya msg kuwa delivered,
ushauri wangu wa ukweli ni kuwa:
1. mnapoingia kwenye ndoa muwe makini na kuangalia streghts za personalities zenu, na muwe tayari kuishi nazo. Mie sipendi kuona mtu anaishi na mkewe au mumewe huku anaogopa kuleta baadhi ya hoja mezani. Hio si ndoa ni ndoano, na lazima mmoja huyo atakuwa mnyonge na atatia huruma sana hata kwa ndugu na jamaa zake. ajitahidi kumatch up na arguments (hoja) za mkewe, aje na hoja mezani.
Ndoa za kiafrika wote tunaelewa ni za kiukoo zaidi kuliko mtu mmoja mmoja.
2. Kwa huyo jamaa yako bila kuwa wazi baba na mama, lazima kuna mambo mengi sana yametokea hapo nyuma, sie wanawake mara nyingi huwa tunaunganisha matukio mengi madogo madogo na kuyatafakari kwa ujumla wake, kuna habari hatuwezi kuijua hapa.
2. Ajiweke kwa ajili ya mke wake, bila kujidharaulisha, na abainishe wazi majukumu ya kulea ndugu,
KWA KIFUPI ATAMBUE MAANA YA KUITWA BABA, si sifa wa la cheo ni MAJUKUMU. Awe tayari kwanza kuwa BABA WA NYUMBA YAKE ndio ataweza kuwa msaada wa watu wengine.
hili ni tatizo kubwa sana kuliko tunavyodhania.
Personalities za wanaume kwa miaka ya karibuni mimi huwa naona kama wanaanza kukubali kuwaachia wanawake kuprovide security ya familia, hii itatucost, wote wanawake na wanaume.
Kuna mwalimu wangu alikuwa anasisitiza sana wanafunzi wa kiume wasome sana, wasikubali kupitwa na wasichana, alikuwa naogopa sana kuwa watakuja kudharauliwa baadae, mie kil amara huwa nakumbuka na kuzidi kuona ukweli wa maneno yake mengi kama haya:
- we mtoto wa kuime usikubali kudharauliwa,
- usiache familia yako isikutegemee, hakikisha unawatunza
- mwanaume anatakiwa awe radhi hata kukesha ili kulinda familia yake
- mtoto wa kiume halii mbele ya mtoto wa kike
- mwanaume anatakiwe awe jasiri wakati wote
- jibebeshe jukumu la kutunza familia yako kwa heshima
- usikubali mwanamke akulishe atakudharau au utajidharau
- mwanaume huwezi kusamehewa kwa kukosa uelekeo na msimamo wa maisha yako
nk nk