Mke hataki ndugu wa mume:Msaada please.

Mbona mnakuza mambo, Issue ni mke hataki ndugu za mme na limejionyesha wazi wazi baada ya ndugu yake kuja na hakuongea chochote..

hahaha!sawa crash lkn je,,amewahi kuongea nae mara ngapi juu ya hilo kabla ya kumtimua?
 
Duh Haika lah!

Tribaphobia! - right?
kwa kiasi, fulani.
pia phobia ya dini!!
kwanini useme eti hawa si waswahili tu!!! au si unajua tena wakristu au waislamu!! au
Eti wahaya, wangoni, wazaramo, wasukuma, mtu anaambiwa kafanya ishu fulani kw akuwa yeye ni kabila au dini fulani.
habari nzima inapoteza uzito wake!

mimi huwa naamini kuna wakati ndoa inafika mahali lazima ivunjike hapo ni wakati wahusika wote wawili wanapokuwa hawako radhi kubadilika ili kusikilizana tena kama awali. kama hawa inawezekana wameshafikia point of no return.
 
Kwa ndugu yake mbona hakujadili na bado hakuongea chochote....kifupi jamaa anatakiwa asimamie maamzi yake kama kicho cha familia na akileta msimamo wake wa kuto wataka ndugu za mme amtimue....

Hiyo alikuwa anafahamu sana kuwa ndugu yake anatakiwa kuja but kwa kumheshimu mume wake alimuomba huyo ndugu mwenye mtoto amuombe mume kama mkuu wa familia na hilo pia mume alitakiwa kulifikisha mezani but kwa kichwa chake cha mfume dume akona yeye ni final say. Sasa
 
Kwa ndugu yake mbona hakujadili na bado hakuongea chochote....kifupi jamaa anatakiwa asimamie maamzi yake kama kicho cha familia na akileta msimamo wake wa kuto wataka ndugu za mme amtimue....

Amtimue? vipi kama hapo wanapoishi ni kwa mwanamke?
 
Pole sana mama,
lakini ni kweli wachaga walio wengi wamekuwa na tabia ya kutokutaka kukaa na ndugu za mme lakini linapokuja swala la ndugu wa zake haongei na tena utapaswa kuwapeleka shule kwa garama mme...ninamifano ya kutosha
 
pole dada kwa kuguswa na ukabila ,msamehe ila anahitaji ushauri kuna watu wamekuwa na stereo type hizi,mimimmke wangu ni mmeru huwa napata shida kuwa umeoa wanaofanan na wachaga ila ninavyo fahamu ubaya /ukatili upo kwa mtu
 
tatizo ni kutoshirikishwa amuombe msamaha tatizo wanaume neno samahani ni la kichina kwao hawalitamki kabisa . alipaswa kushauriana na mke wake hasa ukizingatia suala la malezi ni nyeti na kama kweli mtoto ni tukutu atawaharibu na wao wangeshauriana waone namna wangeweza kumlea .
duh na kwa bi dada huyo asiwe kama mwanamgambo wa taliban apunguze msimamo imeshakuwa ameletwa amlee kama mwanaye kwani angekuwa mtukutu asingemlea .
ila kama hataki kuelewa japo mm ni mwanamke lakini nasema apigwe talaka yake alale mbele
 
Hili ni tatizo kubwa kwa wanawake wengi sana, labda linahitaji utafiti kujua chanzo ni nini. Wengi hawapendi kabisa ndugu wa kiume. Ila kuntimua mke sio sahihi sana, kwani kosa moja haliachi mke.
 
hahaha!sawa crash lkn je,,amewahi kuongea nae mara ngapi juu ya hilo kabla ya kumtimua?
ukisoma mada utaelewa kuwa ni tatizo la siku nyingi na mwanamke amekuwa akisisitiza hamtaki yule mtoto yatima kisa hakushirikishwa kibusa kama hakushirikishwa kwenye swala kama hilo angemweleza mme wake asiwe anafanya maamzi kama hayo na siyo kumtaka aondolewe yule mtoto...aendewapi sasa huyu yatima...
 
tatzo jamaa anafanya maamuz bila kumshrikisha mkewe na ndo hapo tatzo linapotokea mwambie aache ukiritimba au umimi anaish na mkewe hvyo itakuwa flesh kama akimshrkisha mkewe kwanza ni hlo 2uu mm ndo ninalaliona japokuwa huyo mkewe nae anatatzo la kuchukia ndugu wa mume wake ila huwa wepesi kuelewa kama akiwashrkisha vzur sawa man
 
mie nadhani ndoa yenu haihang kwenye balance..huyo mwanamke anataka yeye ndio achukue nafasi ya huyo mwanaume na kuiendesha familia..
mie nakushauri kama wewe ndio 'provider' wa familia yenu then lazima u man-up na kuwa na final say!kuwa aggresive kidogo kny maamuzi na matendo yako usimruhusu akakuendesha...
kama wewe na mkeo wote ni provider wa familia yenu then jaribu kumshirikisha mkeo katika maamuzi yoyote yale...

cha kufanya kuwa na courage,mface mkeo na umwambie wazi kuwa tabia yake ya kugomba kuhusu huyo mtoto yatima na kuacha ndugu yake HUIPENDI,na asipojirekebisha utafanya maamuzi mazito ya kumtimua!:coffee:
 
Kuweni na akili kama nyoka na wajanja kama huwa.
Kwanza mpendwa mtoa mada kama umetaja kabila la huyu dada ili tutoe ushauri
kwa kuangalia na hilo, haujawa sahihi, labda ungetuambia na kabila la huyo baba.

Mwanaume ni kichwa cha nyumba ni kweli,
Tumeambia tuwatii waume zetu kweli, lakini katika mambo mema.

Mwanaume huyu asifanye maamuzi tu kwa sababu yeye ni wanaume hapana,
Aishi na mke wake kwa akili. Amshirikishe katika hali ya upendo, heshima na adabu.
Aaache mfumo dume wa kijinga. Kwa ajili ya ustawi wa ndoa yake, familia yake na ndugu zake.

Inavyoonekana wewe na jamaa wengine na mume mwenyewe mnaona kasoro kwa huyo zinatokana na kabila,
hamwezi kumaliza tatizo kwa mtazamo huo. Mtazameni yeye kama yeye, mwambie azungumze na mke wake,
waelewane wao wawili kwanza halafu watafikia mwafaka wa jinsi ya kumlea huyo mtoto.

Wakumbuke kwamba kumlea huyo mtoto ni wajibu wao wote, na Mungu atawabariki, hata kama asingekuwa
ndugu yao. (Mungu ni baba wa yatima, hata wasipomlea wao kwa kiburi chao, Mungu atainua watu kwa ajili yake)

Hapa wakubali kuwa wanyenyekevu waache kiburi na ukoloni, wajue tunaishi kwa neema,
Huyo baba ajitambue anakosea wapi ashuke na huyo mama ajitambue anakosea wapi ajishushe pia,
Kwa sabau hapo watu wanaishi kwa kiburi na ndo maana huyo baba kamkubali huyo ndugu wa mwanamke kwa kiburi,
ili aone mama atasema nini, na huyo mama nae kwa kiburi akanyamaza.

Kiburi ni tabia ya shetani. Kawaambie wote wawili waache kiburi.
Wakae wayamalize, maisha yaendelee,
Waambie wanajua je ju ya watoto wao. Je wanauhakika wataishi mpaka watoto wao waweze kujitegemea??
Mbona wanashindani katika mambo yasiyo na maana. ASK THEM DO THEY KNOW ABOUT THEIR TOMORROW??
 

Atafute shule ya bdng sio lazima iwe ya watoto yatima, na mtoto akifunga shule akae nae siku chache ampeleke kutembea kwa ndugu wengine mpaka atakapokua mkubwa na anauwezo wa kujitetea ndo awe anakaanae akifunga shule. Ila kwa kiasi flani mama huyo hafai.
 

Kuchukia ndugu mara nyingi hua inatokana na malezi alolelewa, kama ameishi akiona mamaake au baba anabagua ndungu wa upande mmoja mara nyingi atafuata hivyo. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, haitokei tu from no where.
 

Acha ligi wewe, kataja kabila tu hakumaanisha wanawake wote wakichaga, pengine asingetaja watu wangemuuliza chakwanza, huyo mama ni kabila gani.
 

Haika nimekubaliana na ushauri wako. Hata mm yalinikuta kwa mtoto wangu wa kujifunzia na kesi ilienda mpaka ukweni,haikusaidia nilionekana simsikilizi mke mke wangu japo siyo kweli. Nisingeweza kumuondoa mtoto wangu wa kumzaa kisa mke wangu hampendi. Na wakati anaolewa alijua na kuwa nina mtoto. I stood up with my decision ya kukaa na mtoto wangu. Nilipopata transfer ya kazi haikuwa rahisi kuondoka na familia mara moja. Guess what happen nilipoondoka. Mtoto alisafirishwa kwa dada yangu faster, ilibidi niingie gharama ya kutafuta shule ya boarding ambayo nayo kutokana na umbali hela zilichakachuliwa na mtoto kupelekwa kijshule ambacho siku nimeenda likizo nilitamani kulia. Thanks God nipo na mke wangu na watoto wangu wote.Though najua kuna ugumu furani wa yeye kukaa na huyu mtoto but nina msimamo kwa watoto wote bila upendeleo. Sasa nikitaja kabila najua utanichapa acha niishie hapo. Ila ukweli kuna shida sana kwa akina dada kupendelea upande mmoja japo siyo wote.
 

Hapana jamaa hakutaja kwa nia mbaya, im sure asingetaja swali la kwanza angeulizwa huyo mwanamke ni kabila gani. Sidhani kama inaweza kumkasirisha mtu hee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…