.......Hili jambo la kubadili jina baada ya kuolewa kwa sisi wadada ni issue kubwa sana siku hizi, wadada wengi hatupendi kubadili majina yetu.........hata mie mwenyewe nilikuwa nakataa kubadili jina langu, maana vyeti vyangu vya shule vyote vipo kwa jina la baba yangu, halafu leo tena nibadili niliona kama haitaleta maana.
Baada ya Mr kulalamika sana kwa nini sibadili jina, niliamua kubadili tu ili nimridhishe.......hivyo natumia majina yangu kama ilivyokuwa yaani jina la ukoo wangu halafu mwishoni ndio naongeza jina la kwake.
Hii kitu haina umuhimu sana, ila kwa kuwa ndoa ni makubaliano ya watu wawili, na kama mwanaume anataka utumie jina lake, mie naona bora tu utumie ili kulinda amani/ masikilizano yenu ya ndoa.......ukitumia jina la mr wako wala hupungukiwi chochote.