nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,379
ukisusa tu,mi naliuza kabisa tuone.
Brother mke ni muhimu nakubali lakini kumwonya achukue tahadhari ndio imekuwa taabu. nimeupata ushauri wako nashukuruSamahani brother, kweni kati ya gari na mkeo kipi ni muhimu sana? Naona kama gari ni "material thing" ambayo inachakaa na unaweza kununua na kuibadili upendavyo. Mke ni kitu cha tofauti kabisa, ni mwenzi wa Maisha na faraja ya moyo wako. Ni mama wa watoto wako na pia ndiyo aliyebeba heshima ya familia yako.Ningekuwa mimi ni wewe nisingemkasirikia hivyo. Ningemuuliza kwa upole kutafuta namna ya kumsaidia. Na mwishowe ningemnunulia gari yake mwenyewe aligonge atakavyo.Brother uko kwenye ndoa, Ndoa ni kitu cha tofauti. Thing wisely!
Jikaze mnunulie Benz.......vibaka wanaziogopa ile mbaya.....au landrover tule tutaa twake nani ataiba?
Brother mke ni muhimu nakubali lakini kumwonya achukue tahadhari ndio imekuwa taabu. nimeupata ushauri wako nashukuru
Yap! hapo umenena kutokana na uzoefu!!!kaka mwanamke huwezi kumwelewa hata siku moja! hata umfanyie lipi anapofanikiwa akikutana na ma shosti kwenye biashara zao lzm wambadirishe tabia tuu. utaona tu anakuwa against wewe! nimeona wengi na ilishanikuta. nilishawahi ulizwa umefuata nini hapa wakati hiyo biashara nimegharamia mie 100 percent. nikaja gundua kuna rafiki yake anamjaza ujinga aisee ilikuwa hell nikafunga biashara. baada ya 3yrs akaja gundua yule shosti hakuwa mtu mzuri hakupenda tuwe na ile bizness alikuwa akiongea vibaya kwa watu kwamba wstafunga tu kibiashara chao. iliniuma sana lkn sasa kajifunza
sina tabia ya kusimanga lakini pia napenda aonyeshe kuguswa na tatizo. angalau ajaribu kushughulika na akishidwa namsaidia. lakini kitu kama hicho kinatokea yeye kimya tu inakuwa vigumu kunyamaza . kibinadamu unakwazika na kujiuliza vipi kwa mwenzangu hili si tatizo?Unaogopaeee??Kama kweli unajua hujawahi kumsema vibaya kuhusu hiyo gari kaa chini ongea nae yaishe....Na kama una zile tabia za kusimanga....oooh wewe mzembe.....hujui bei ya gari.....unafanya mchezo na pesa.....ili hali ilitokea bahati mbaya basi amekuchoka ujue amekuchoka na yuko mbioni kujinunulia la kwake mwenyewe! -mwombe yaishe maisha yaendelee
huko ni mpaka kwa order, kila jioni anaumwa kichwa, mara kachoka mara hili mara lile.Jee tendo la ndoa anakupa?kama anakupa basi wewe usiliwazie,kama hakupi kasusa huyo mwanamke ana tabia mbaya anataka kuwa level na wewe ktk familia
Wakuu, naomba ushauri katika mkwamo huu!Nilimpa mke wangu gari atumie kwa ajili ya shughuli zake za biashara ya duka la nguo. Kwa kwenda na kurudi nyumbani na kwa ajili ya kufuatilia mabo ya biashara yake. vile vile kwa shughuli za nyumbani kama kupeleka watoto hospitali n.k. Mimi pia nina usafiri wangu. Mwezi jana aliibiwa side mirror na taa moja ya mbele pale Kariakoo. Akaniarifu na baada ya kuona hana juhudi ya kurudishia huku akiendelea kuendesha gari "chongo" , niliamua kutumia pesa zangu kufanya replacement. Wiki mbili zilizopita nimekuta tena taa moja hakuna. Kumuuliza ikawa zogo. Anasema nisimuulize kitu yeye atarudishia. nikasubiri ikawa kama mwanzo. Baadaye nikaamua tena kununua taa nyingine na nikamwonya kuwa sitaweza kuwa nanunua taa naye anaendelea kutochukua tahadharina kuwa mwangalifu. Heeh! kumbe nimechafua hali ya hewa! Mwanamke wiki mbili hizi hatumii gari anakwenda kazini kwake kwa usafiri nisioujua. Juzi akanitumia sms akasema " sihitaji gari lako masimango yamezidi" Nishaurini wataalam,
a good joke ila huwa sina mkono mwepesi lakini pia sijui kukaa na kitu moyoni. labda huko ni kubwabwaja. lakini kwa msimamo wako ungekuwa naye ungenunua mengi kweli ( take that Joke as well)NyaniMzee unalo nimempatia usafiri wa uhakika tena usiokuwa na masimango.In fact nimemhakikishia asiwe na hofu hata akiibiwa gari nitampatia lingine wewe taa tu unabwabwaja bwahaaaa ahaaaa!.Joke mkuu wangu usije mtwanga shemeji yetu makonde.
Nyumba kubwa dada yangu, nafikiri hili neno kuolewa,haya mambo ya kutolewa mahari yanatucost sana. Sidhani kama wanaume zetu walio wengi wanaelewa kuwa hata sie tu watu wazima! Utakuta mtu anakugombeza utafikiri mtoto wa darasa la kwanza! maneno kama we mjinga, kichaa, mpuuzi tena mbele ya watoto au mtu baki. kusema ukweli inauma. Halafu the same people wanapiga kelele juu ya kutokuua self-esteem ya mtu bila kutambua wanachokifanya kwa wenzi wao.Mke aonywi kaka anaelekezwa. Mpe ushauri wa jinsi gani anaweza kuepuka hilo tatizo lisijitokeze na usimuonye kwani unakuwa umemchukulia kama mtoto.
kuwa mwangalifu kwa ya kuchukua tahadhari unapo park gari, sio kuliangalia Mkuu.