Mke kazira kutumia gari: Ushauri please

Mke kazira kutumia gari: Ushauri please

Samahani brother, kweni kati ya gari na mkeo kipi ni muhimu sana? Naona kama gari ni "material thing" ambayo inachakaa na unaweza kununua na kuibadili upendavyo. Mke ni kitu cha tofauti kabisa, ni mwenzi wa Maisha na faraja ya moyo wako. Ni mama wa watoto wako na pia ndiyo aliyebeba heshima ya familia yako.Ningekuwa mimi ni wewe nisingemkasirikia hivyo. Ningemuuliza kwa upole kutafuta namna ya kumsaidia. Na mwishowe ningemnunulia gari yake mwenyewe aligonge atakavyo.Brother uko kwenye ndoa, Ndoa ni kitu cha tofauti. Thing wisely!
Brother mke ni muhimu nakubali lakini kumwonya achukue tahadhari ndio imekuwa taabu. nimeupata ushauri wako nashukuru
 
Huyo ni mtu mzima na naamin hata yeye hapendi kinachotokea km umeamua kumpa basi mwache huru nalo,na ukiamua kumsaidia kutengeneza au kureplace kitu basi fanya na usimwambie kitu yeye anaelewa sio mtoto,itafika mahali atakuwa anaona haipendezi ww kila wakati unareplace na atakuwa anafanya hivyo mwenyewe hata kabla ww hujamfanyia au hujajua kilichotokea,kwa namna yoyote hayo ni masimango japo ww hukusudii kumsimanga.
 
Mke aonywi kaka anaelekezwa. Mpe ushauri wa jinsi gani anaweza kuepuka hilo tatizo lisijitokeze na usimuonye kwani unakuwa umemchukulia kama mtoto.

Brother mke ni muhimu nakubali lakini kumwonya achukue tahadhari ndio imekuwa taabu. nimeupata ushauri wako nashukuru
 
kaka mwanamke huwezi kumwelewa hata siku moja! hata umfanyie lipi anapofanikiwa akikutana na ma shosti kwenye biashara zao lzm wambadirishe tabia tuu. utaona tu anakuwa against wewe! nimeona wengi na ilishanikuta. nilishawahi ulizwa umefuata nini hapa wakati hiyo biashara nimegharamia mie 100 percent. nikaja gundua kuna rafiki yake anamjaza ujinga aisee ilikuwa hell nikafunga biashara. baada ya 3yrs akaja gundua yule shosti hakuwa mtu mzuri hakupenda tuwe na ile bizness alikuwa akiongea vibaya kwa watu kwamba wstafunga tu kibiashara chao. iliniuma sana lkn sasa kajifunza
 
Yap! hapo umenena kutokana na uzoefu!!!
 
Unaogopaeee??

Kama kweli unajua hujawahi kumsema vibaya kuhusu hiyo gari kaa chini ongea nae yaishe....

Na kama una zile tabia za kusimanga....oooh wewe mzembe.....hujui bei ya gari.....unafanya mchezo na pesa.....ili hali ilitokea bahati mbaya basi amekuchoka ujue amekuchoka na yuko mbioni kujinunulia la kwake mwenyewe! -mwombe yaishe maisha yaendelee
 
Unaogopaeee??Kama kweli unajua hujawahi kumsema vibaya kuhusu hiyo gari kaa chini ongea nae yaishe....Na kama una zile tabia za kusimanga....oooh wewe mzembe.....hujui bei ya gari.....unafanya mchezo na pesa.....ili hali ilitokea bahati mbaya basi amekuchoka ujue amekuchoka na yuko mbioni kujinunulia la kwake mwenyewe! -mwombe yaishe maisha yaendelee
sina tabia ya kusimanga lakini pia napenda aonyeshe kuguswa na tatizo. angalau ajaribu kushughulika na akishidwa namsaidia. lakini kitu kama hicho kinatokea yeye kimya tu inakuwa vigumu kunyamaza . kibinadamu unakwazika na kujiuliza vipi kwa mwenzangu hili si tatizo?
 
Jee tendo la ndoa anakupa?kama anakupa basi wewe usiliwazie,kama hakupi kasusa huyo mwanamke ana tabia mbaya anataka kuwa level na wewe ktk familia
 
Nilichokuja kugundua kwa muda nilokaa hapa JF wanaume wanapenda kudanganya wenzao; utasikia ooh mimi mke wangu wala anibabaishi akinuna namwacha anune; ooh wanawake siyo wa kuendekeza. Kwa hiyo mnaoomba ushauri mchanganye na akili zenu. Hao wengine wanawambia hivyo kumbe wengine makwao wanapigishwa mpaka deki. Kila mwanaume anatabia ya kujionyesha kidume au jeuri akiwa na wanaume wenzie akifika kwa wife anafyata mkia.

Mtasambaratisha ndoa zenu mkifata ushauri wa kuchangamsha genge.
 
Jee tendo la ndoa anakupa?kama anakupa basi wewe usiliwazie,kama hakupi kasusa huyo mwanamke ana tabia mbaya anataka kuwa level na wewe ktk familia
huko ni mpaka kwa order, kila jioni anaumwa kichwa, mara kachoka mara hili mara lile.
 
NyaniMzee unalo nimempatia usafiri wa uhakika tena usiokuwa na masimango.In fact nimemhakikishia asiwe na hofu hata akiibiwa gari nitampatia lingine wewe taa tu unabwabwaja bwahaaaa ahaaaa!.Joke mkuu wangu usije mtwanga shemeji yetu makonde.

Wakuu, naomba ushauri katika mkwamo huu!Nilimpa mke wangu gari atumie kwa ajili ya shughuli zake za biashara ya duka la nguo. Kwa kwenda na kurudi nyumbani na kwa ajili ya kufuatilia mabo ya biashara yake. vile vile kwa shughuli za nyumbani kama kupeleka watoto hospitali n.k. Mimi pia nina usafiri wangu. Mwezi jana aliibiwa side mirror na taa moja ya mbele pale Kariakoo. Akaniarifu na baada ya kuona hana juhudi ya kurudishia huku akiendelea kuendesha gari "chongo" , niliamua kutumia pesa zangu kufanya replacement. Wiki mbili zilizopita nimekuta tena taa moja hakuna. Kumuuliza ikawa zogo. Anasema nisimuulize kitu yeye atarudishia. nikasubiri ikawa kama mwanzo. Baadaye nikaamua tena kununua taa nyingine na nikamwonya kuwa sitaweza kuwa nanunua taa naye anaendelea kutochukua tahadharina kuwa mwangalifu. Heeh! kumbe nimechafua hali ya hewa! Mwanamke wiki mbili hizi hatumii gari anakwenda kazini kwake kwa usafiri nisioujua. Juzi akanitumia sms akasema " sihitaji gari lako masimango yamezidi" Nishaurini wataalam,
 
NyaniMzee unalo nimempatia usafiri wa uhakika tena usiokuwa na masimango.In fact nimemhakikishia asiwe na hofu hata akiibiwa gari nitampatia lingine wewe taa tu unabwabwaja bwahaaaa ahaaaa!.Joke mkuu wangu usije mtwanga shemeji yetu makonde.
a good joke ila huwa sina mkono mwepesi lakini pia sijui kukaa na kitu moyoni. labda huko ni kubwabwaja. lakini kwa msimamo wako ungekuwa naye ungenunua mengi kweli ( take that Joke as well)
 
Mke aonywi kaka anaelekezwa. Mpe ushauri wa jinsi gani anaweza kuepuka hilo tatizo lisijitokeze na usimuonye kwani unakuwa umemchukulia kama mtoto.
Nyumba kubwa dada yangu, nafikiri hili neno kuolewa,haya mambo ya kutolewa mahari yanatucost sana. Sidhani kama wanaume zetu walio wengi wanaelewa kuwa hata sie tu watu wazima! Utakuta mtu anakugombeza utafikiri mtoto wa darasa la kwanza! maneno kama we mjinga, kichaa, mpuuzi tena mbele ya watoto au mtu baki. kusema ukweli inauma. Halafu the same people wanapiga kelele juu ya kutokuua self-esteem ya mtu bila kutambua wanachokifanya kwa wenzi wao.

Kwa mwanamke ambaye unamtreat kama mtoto unategemea afanye nini kama si kususa kama mtoto? Ndio silaha pekee alonayo maana kukupiga hawezi!
 
Huyo ni mke au hawara?! umesema alikutumia sms inamaana hamuishi pamoja?
na kama mnaishi pa1 ulipomuuliza alikujibu nini?
muongozo ndipo nione namna ya kukusaidia.
 
Back
Top Bottom