Mke kubadili jina la ukoo baada ya kuolewa!

Kubadili ni vyema tu hakuna madhara inategemea unapendaje mie nilibadili zamani na sina matatizo
 
nakwambia sibadili hata kama la Obama nini hao uliowaja,labda tu niwe nataka unilipie deni hapo ntabadili.

Duuh! Kumbe bado wapo wa kununuliwa kwa BEI POA?!!

haya hii beijing sijui hatimayake nini kwahiyo kwa sababu ya kumjua ukubwani aiwezi kukusababisha utumie jina lake labda awe ana kulipia ada au mkopo siyo nzuri na wala siyo utu sasa where is the true love

Hao wanaodai kulipiwa madeni achana nao, wameamua kuleta mzaha tu coz hata point zao zipo kimzaha-mzaha
Na kama wanamaanisha kweli basi ujue hao ndo wananunuliwa popote na yeyote
 
Ni mila na tamaduni kwani mwanamke anapo olewa huhukuliwa amesha kuwa moja ya ukoo wa mwanaume ndiyo maana baadhi ya makabila yalikuwa hayawasomeshi wanawake kwa kuogopa kuwa wafaidisha waoaji na kuna makabila mwanamke akisha olewa hata kuzikwa hatozikwa nyumbani kwa kwao ila atazikwa nyumbani kwa mmewe...
 
WanaJF,

Nawatakia maandalizi mema ya V-Day. Naamini kila siku inatkiwa iwe ya kivalentine.

Ninatatizwa na suala tajwa hapo juu - Mke kubadili jina la ukoo(surname) baada ya kuolewa na kuchukua uko wa mumewe.

Kumekuwa na mabadiliko kwenye suala hili ...

1. wanawake wengine hawabadili kabisa yaani wanabaki na majina yao ya ukoo kama kabla hawajaolewa
2. wanawake wengine wanabadili kwa kuungisha majina yote mawili. mfano Mr. K. Ali ana mchumbia Miss. M. John baada ya kuolewa Mrs. L . John-Ali.
3. Wengine wanaachana na majina yao, kwa mfano wa 2. atakuwa anaitwa Mrs. M . Ali

1. Je kuna umuhimu gani wakubadili au kutobadili?
2. Madhara yake ni nini?
3. Historia yake ilianza lini na wapi?

Asanteni

Inategemea Mkuu
Nia ya mwanamke kutumia majina ya mume wake ni moja kati ya njia za kujenga na kumuongezea heshima mwanamke ambae ni mke wa mtu, tofauti na mwanamke ambaye hajaolewa. Ndio maana unaona wanawake wenye heshima zao wanaitwa Mama Michelle Obama, Mama Maria Nyerere n.k. ambapo maana yake nyingine ni kwamba mwanamke aliyeolewa ndio amechukua nafasi ya mama mzazi wa mwanaume kumlea huyo mwanaume aliyeolewa nae. Kwahiyo kwa asili ya binadamu popote pale duniani mwanamke ni mlezi wa mwanaume.
Ndio maana tunakuja na msemo unaosema HAKUNA KAMA MAMA

Kama mwanamke ana vyeti, passport, au mali zozote ambazo zina majina yake kabla hajaolewa hayo yatabaki hivyo hivyo, wala hakuna haja ya kuyabadilisha coz yeye mwanaume hajaoa hadi vyeti, passport au mali anazomiliki mwanamke. Nje na utambulisho ambao mwanamke atalazimika kutumia vyeti, passport na hati nyinginezo, mwanamke ni keshima kwake kujitambulisha Mrs Mnyanya kama kaolewa na Manyanya, iwe kazin, au kwa watu mbalimbali
Na pia hakuna tatizo lolote kubadili majina sema basi tu kuna baadhi ya vijana wa sasa wanamtazamo wa UMIMI zaidi au pengine hawajui mwanzo wa kitu husika
Nawakilisha
 
Kama ni suala la heshima,hata kuoa nakupa heshima kwamba mimi ni mume wa fulani,basi tumia jina langu pia,heshima hailetwi na upande mmoja,pili kama nachukua nafasi ya mama yako kukulea we huoni nastahili kupewa hiyo heshima ya wewe kutumia jina langu?
Mtu aamue mwenyewe bwana,kuna wanaume wake zao hawataki kufahamika ni wake zao,umetoa mfano wa watu wenye heshima,je majambazi sugu,wauaji,malaya wa kupindukia!!!!!
 
Mumeo kama mpenzi wako akiomba ubadili jina kwa nini umkatalie? Je una sababu zipi za kumwelewesha?

heee! Kumbe huwa mnaomba tubadili majina? Nilifikiri wanawake wenyewe ndio wanaamua.
Kubadili huko ni hadi kwenye vyeti au?
 
CPU heshima haipo kwenye jina!Kama mume ni mtu wa ajabu ajabu kubebana na jina lake kutashusha heshima!Na kama mke ni kituko hata abebane na jina la Papa bado atabaki kua kituko tu!
 
Ninachujua ukiolewa unahama kutoka familia yenu kwenda familia ya mume. Ukiugua unatibiwa na hata ukifa unazikwa hukohuko. Ktk hili kuongea jina la ukoo ulioenda is not an option.

Unapotambilishwa utaitwa Mrs. Unamalizia jina la ukoo wa mwanaume. Lakini kuna wale wabishi hata kama ameolewa na mumu yupo anapendelea kuitwa Ms na wengi wao ni feminist.
 
Kama ni suala la heshima, hata kuoa nakupa heshima kwamba mimi ni mume wa fulani, basi tumia jina langu pia, heshima hailetwi na upande mmoja, pili kama nachukua nafasi ya mama yako kukulea we huoni nastahili kupewa hiyo heshima ya wewe kutumia jina langu?
Mtu aamue mwenyewe bwana, kuna wanaume wake zao hawataki kufahamika ni wake zao, umetoa mfano wa watu wenye heshima, je majambazi sugu, wauaji, malaya wa kupindukia!!!!!

My dia better read between lines!
Hapa sipambanishi heshima za mwanaume na mwanamke. Mwanamke na mwanaume kamwe hawawezi kupata heshima kwa njia sawasawa kwa kila kitu, kila mmoja ananjia yake ya kupata heshima yake. Hutakiwi kuwa na mawazo pambanishi na mwanaume kwa kila jambo.

Hapo kwenye red, nitajie mtu ambaye anatumia jina la mama ake mzazi kama Surname??!!
Hapo kwenye blue inaonyesha wazi hujaelewa nilichoandika.
Mimi nimeanza kwa kusema NI MOJA YA NJIA ZA KUMPA HESHIMA MWANAMKE, hayo ya uhalifu uliyoyataja ni tabia ya mtu mwenyewe na wala sio kwamba ukiolewa na mwanaume basi hadi tabia zake zinakuoa. Heshima ya ndoa haipaswi kuchanganywa na tabia za mtu binafsi.
Ila kama wewe huoni sawa kutumia jina la mwanaume basi ni wewe umejiamulia hivyo, mimi sishinikizi wala silazimishi mtu kufanya hivyo bali naelezea kama utaratibu tuliojiwekea sisi wenyewe binadamu
 
CPU heshima haipo kwenye jina!Kama mume ni mtu wa ajabu ajabu kubebana na jina lake kutashusha heshima!Na kama mke ni kituko hata abebane na jina la Papa bado atabaki kua kituko tu!

Jamani someni btn lines
Sijasema heshima iko ktk jina pekee
Na isitoshe msichanganye heshima ya ndoa na tabia ya mtu mwenyewe. Kama tabia zenu ni chafu basi ni chafu tu, lakin heshima ya kwamba mmefunga ndoa au mmeungana haitochafuliwa. Binadamu kuwa wamoja ni heshima
 
Hilo neno ZENU ingekua YA MTU ungekua umetumia uungwana!
 
Ninachujua ukiolewa unahama kutoka familia yenu kwenda familia ya mume. Ukiugua unatibiwa na hata ukifa unazikwa hukohuko. Ktk hili kuongea jina la ukoo ulioenda is not an option.

Unapotambilishwa utaitwa Mrs. Unamalizia jina la ukoo wa mwanaume. Lakini kuna wale wabishi hata kama ameolewa na mumu yupo anapendelea kuitwa Ms na wengi wao ni feminist.

Ahsante kwa maelezo m-badala.
Umenisaidia kujua watu wabishi wanatambuliwaje
 
Mkuu sidhani kama kuna faida au hasara inategemea na preference lakini takupa mifano miwili...
Mfano mwanamke Dr. ambaye kafanya kazi kwa muda mrefu hilo Jina ndio trade mark yake.., sasa akibadilisha akishaolewa italeta confusion.

Mfano wa pili Tina Turner Turner lilikuwa jina la Mume wake ambaye walikorofishana na wakaachana lakini Tina ilibidi abaki na hilo jina sababu ndio lilikuwa jina lake la biashara ambalo ndio identity yake..

kwahiyo in short it just depends, unaangalia pia kutakuwa na effects zipi ukibadilisha Jina.

Its all about identity Mfano nikisema Hilary (angekuwa surname yake sio Clinton) ni vigumu kujua mtu unaemuongelea Hilary gani.., Je ni yule muuza maandazi ?...... Hapana ni yule aliyegombea Uraisi.... Yupi ?, Hilary Clinton aha ahaaaa kumbe..., ninamjua.. Hope you get my point
 
!Nadhani kukubali kuolewa inatosha kutuunganisha!Jina langu ntabaki nalo kama atakavyobaki na lake!

Lizzy nilipo oa nilimuomba mwenzangu abadili jina akagoma, nimuacha wala sikumlazimisha. Bahati nzuri nikapata kazi nje ya nchi akatakiwa aombe ruhusa ya kazini kwao ili aje anitembelee. Aliambiwa hujaolewa na kama umeolewa kwa nini unatumia jina hili? kama unataka ruhusa basi fanya utaratibu wa kubadili jina. Ilibidi aombe kubadilisha jina. Akapewa ruhusa. Alipofika huku ilibidi nimuombee health insurance akaambiwa utafuata jina la mumeo hata kama kwenye passport yako unatumia la baba yako maana ndiye anakatwa kwenye mshahara wake. Pia kazini kwangu nilipowasilisha document zake za kumuongeza kama dependant wangu walikataa kusajili jina lake. Ikabidi tutumie la kwangu ndiyo mambo yaende sawa kwa ujumla ulikuwa sumbufu moja kwa moja. Yeye mwenyewe alikili kuwa alilazimisha kitu bila kujua madhala yake. Kwa Ushauri tuu LIZZY jaribu kuwa mpole.
 
Duuuh
Zinga la mfano.
Ila nimegundua kuna baadhi ya watu wanataka kuelewa tu kwanin unatumia majina ya mwanaume KWA KUJIFANYA WABISHI
Ila mkuu nje na masuala ya kazi, unaona ni sawa mwanamke akatae kutumia jina la mwanaume??
Mi naona kukataa kwao kumekaa ki-uharakati au ki-ubishi zaidi kuliko ki-ustaarabu au ki-sababu za kueleweka
 
Mkuu I doubt kama marriage certificate ingeshindwa kukamilisha hayo hapo juu... There is no Law forcing someone to use a certain surname...
 
CPU na Voice of reason, Mimi sikuyajua hayo mpaka yaliponikuta. Na ilianzia kwenye Passport ndipo nilipo mwambia tumia jina langu akagoma na form nilijaza mwenyewe. Kwa busara siwezi anza kuweka jina langu bila kumshirikisha. Passport ilienda through na kuludi na jina lake. Ngoma ilikuwa kazini kwake, huku nchi ya watu na kazini kwangu waligoma. Na tena walikuwa wananishangaa kwa nini atumie jina lake kama kaolewa na wewe? vyeti vyote viliwasilishwa lakini walisema atatumia jina lako.
 
Mkuu unless yupo kwenye nchi za kiarabu which am not sure na sheria zao.., lakini majority ya nchi you cant force mtu kutumia jina fulani.. thats why nimetoa mfano wa Dr. kwenye post #34 kwamba huyu dada atakuwa amejenga jina lake kwa muda mrefu kwahiyo kubadilisha litakuwa na effect kwa kazi yake...

Think about this Leo ukimuoa Whitney Houston utataka abadilishe Jina aitwe Whitney Wakumwitu... huoni kwamba hii itamuaffect kwenye biashara yake?
 
Duuuh
Zinga la mfano.
Ila nimegundua kuna baadhi ya watu wanataka kuelewa tu kwanin unatumia majina ya mwanaume KWA KUJIFANYA WABISHI
Ila mkuu nje na masuala ya kazi, unaona ni sawa mwanamke akatae kutumia jina la mwanaume??
Mi naona kukataa kwao kumekaa ki-uharakati au ki-ubishi zaidi kuliko ki-ustaarabu au ki-sababu za kueleweka

Sio lazima....yote ni uamuzi wa mlengwa!!Iwe kwasababu za maana kwa mtu binafsi na za kijinga kwako au bila sababu at all yote ni uamuzi wa mtu.Alafu jaribu kuelewa tofauti.....mtu anaweza asibadili jina lake officially ila bado akajulikana kwa watu kama Mrs au Mama fulani hapo hiyo heshima unayoingelea wewe inakuwepo na inazidi kuwepo!!Kubadili kwenye passport hata nani atajua kwamba hili ni lako au sio lako???Muhimu ni kwa watu wanaokufahamu!!!!Alafu kubadili jina or not hakuleti tofauti yoyote kwenye ndoa....besides huwezi kumuoa mwalimu M akabadili kua mwalimu A....lile ni jina ambalo mtu anafahamika nalo...amelitengenezea heshima aliyo nayo na limezoeleka..... ndoa haiwezi kunifanya niache asili yangu yote!!!
 
Back
Top Bottom