Mke kuficha hati ya kiwanja/nyumba

Mke kuficha hati ya kiwanja/nyumba

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Wananzengo salamu kwenu.

Kuna jambo nakaa nalifikiria sipati jibu na sijui mwenzangu anawaza nini na ana nia gani.

Nilikuatana na huyu mwanamke mwaka 2011 nikiwa chuo na Yeye yupo tu kitaa baada ya muda akafanikiwa kupata kazi tukaendelea kuishi na kupata watoto hadi mwaka jana tulipofunga ndoa ya kiserikali maana tumetofautiana imani na hakuna Kati yetu aliye tayari kumfuata mwenzake.

Kimsingi huyu mwanamke alinunua kiwanja baada ya kukopa hela then akaanza ujenzi na mimi nikaweka hela yangu kidogo ninayopata na nilichukulia hii nyumba ni mali ya familia kwa maana tuna watoto watatu.

Sasa hivi karibuni mwenzangu kaichukua ile hati ya kiwanja na sijui kaipeleka wapi,actually imeandikwa jina lake Mimi nipo kama shahidi.

Ndoa yetu kwa sasa imekua ya migogoro sana natunaishi kwa mazoea tu na isitoshe tunaishi mikoa tofauti japo ya jirani.

Sasa kitu kinachonishangaza ni huyu mwanamke kuficha hati ya kiwanja Ili hali tumeamua kufanya hii mali iwe ya familia ina maana watoto sasa Yeye anapoficha hiyo hati likija la kutokea mi nitajua hiyo hati ipo wapi!!? Kama kitu tumeamua kiwe cha familia sioni haja ya kuanza kuficha document muhimu kama hati.

Niliwahi kumuuliza ile hati ipo wapi mbona tangu tumetoka kugonga mhuri kwa mwenyekiti siioni humu ndani ananipiga kiswahili tu.

Mimi naishi kwenye hii nyumba na yeye yupo mkoa jirani kikazi yupo pamoja na watoto.

Je huyu mwanamke yupo sawa kweli kuficha hiyo hati!!? Ili hali tumefunga ndoa na tuna watoto tayari. Sijui Nia yake nini nahitaji ushauri niishi nae vipi huyu mtu manake anaonekana ana ubinafsi mkubwa sana.
 
Kimsingi huyu mwanamke alinunua kiwanja baada ya kukopa hela then akaanza ujenzi na mimi nikaweka hela yangu kidogo ninayopata na nilichukulia hii nyumba ni mali ya familia kwa maana tuna watoto watatu

Sasa hivi karibuni mwenzangu kaichukua ile hati ya kiwanja na sijui kaipeleka wapi,actually imeandikwa jina lake Mimi nipo kama shahidi
Pole mkuu ila bibie hii ni Mali yake hakuna ulazima wewe kujua iko wapi muhimu unaishi kwenye hiyo nyumba tafuta kiwanja ujenge na wewe
 
Tafta pesa ununue kiwanja chako
Asante sana mkuu, hakika nashangaa mwanaume kabisa analalamikia mali za mke wake. Labda tuseme bado mvulana lakini kama ameshakua mwanaume, aamke anawe uso akatafute hela aache kulalamika ...huo muda wa kulalamika angefikiria jambo la kupata hela na angesogea hatua moja mbele.

Note: Mkuu mtoa mada, funguka muda unaenda speed sana.
 
Siwezi jenga nyumba katika kiwanja ambacho hakina jina langu labda kwa wazazi wangu tu. Mke kama ana kiwanja aidha abadile kiwe na majina yetu wote au apambane na hali yake kukijenga.

Mke sio ndugu, undugu unaunganishwa na damu. Mke uunganishwa kwa hati ya kiapo
 
Tafuta hela yako, Nunua uwanja jenga nyumba yako, Maisha ni Amani.
 
Yeye anapoficha hiyo hati likija la kutokea mi nitajua hiyo hati ipo wapi!!?

hapa tu nimekuquote ..maana yake mwananmke wako ana akili kuliko wewe ashajua unampigia timing afe au uumwe ili uwe mrithi wa kiwanja.

shida sio mkeo shida ni wewe mwanaume, mwanaume umekua kama mwanamke, kusimpathize hali ya kifamilia ili kumiliki mali za mkeo na kisa umeweka visenti kidgo, hapo ulimuongezea tu.

ushauri wangu: sooon utapigwa kibuti na hutoamini, mkeo anataka mwanaume mpampanaji.. tafuta hata eneo la shamba kwenye miji isiochangamka lakini yenye maono ya kuchangamka baadae ..weka mifugo huko weekend peleka familia angalau heshima ije..huitwi jina la baba bure bure..lazima upambane.
 
Siku nyingine upige picha na kuscan hiyo hati nyingine utakayoipata ili uweze kuitunza kwa softcopy, hata kama mchepuko ataificha original(hard copy) wewe utakuwa na softcopy yake.
 
Mali ya mwanamke ni mwanamke na mali ya mwanaume ni ya familia cha msingi tafuta kiwanja chako kajenge.

Hapo ndipo utaelewa wanawake hata kila wakitakacho hawakielewi, kutwa kulilia 50/50.
 
Mkeo kakuona kichwani hamna kitu, pia una mambo mengi hujatulia so kaficha hati kujihami na hapo kakutoa moyoni mda wowote utapigwa matukio mpaka ushangae
 
Siwezi jenga nyumba katika kiwanja ambacho hakina jina langu labda kwa wazazi wangu tu. Mke kama ana kiwanja aidha abadile kiwe na majina yetu wote au apambane na hali yake kukijenga.

Mke sio ndugu, undugu unaunganishwa na damu. Mke uunganishwa kwa hati ya kiapo
Kwa sasa najilaumu sana kuweka hela yangu kwenye ujenzi manake nimechangia kwa kiasi flani pesa yangu bora hata ningeenda tu kufanyia mambo mengine niache apambane nayo peke ake
 
Kwa sasa najilaumu sana kuweka hela yangu kwenye ujenzi manake nimechangia kwa kiasi flani pesa yangu bora hata ningeenda tu kufanyia mambo mengine niache apambane nayo peke ake
Hujachelewa kaanze ujenzi mwingine tena nyumba kali zaidi. Ingawa mnajisumbua tu, mali zote zilizopatikana ndani ya ndoa ni mali ya wanandoa kisheria no matter majina yanasomekaje
 
Back
Top Bottom