Mke mjamzito, nataka kukata bima NHIF ushauri

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
368
Reaction score
556
Wakuu heshima yenu

Nataka kumkatia mke wangu bima ya NHIF,naomba anaejua utaratibu na gharama zake anijuze,hasa hizi ambazo wanasema ni reviewed

Nafanya hivyo kwa sababu ni mjamzito,lakini pia namna ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya ambazo ni wazi atazihitaji sana siku za mbeleni

Napokea ushauri...
 
Very intelligent husband hongera sana mkuu
 
Naomba kuuliza hivi taratibu za kulipa ni kwa pamoja au mtu unaweza kulipa awamu kwa awamu mana naona pesa ni nyingi hasa kwa sisi wa kipato Cha chini
Unapewa control number ya amount yote, inalipwa yote kwa pamoja. Na kupata huduma ni baada ya siku 30
 
Kata mapema mpenzi, maana ukikata wakati anakaribia kujifungua itakusumbua, Bima ukikata haianzi hapohapo kupata huduma, unasubir kwa siku kadhaa ambazo ni kuanzia 30 na kuendelea, kwa maelezo zaidi fika ofc za NHIF zilizopo karibu nawe, au tembelea tovuti yao www.nhif.or.tz kwa maelezo zaidi na utapata mawasiliano yao hapo. Waambie nataka kukata bima sababu inaeleweka usiwaambie kwa sababu mke wangu mjamzito. Kata mapema kuepuka usumbufu na kero plus karaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…