Mke mlevi na mpenda starehe!



mmh, gfsonwin this is a very interesting position, especially coming from a lady...
 
well said mkuu....; tunaoa ili, among other things, tupate furaha, faraja, tujenge familia, tusaidiane kwenye mikikimikiki ya maisha n.k but ndoa nyingine ni kujitafutia ugonjwa wa moyo tu

Wanawake wa siku hizi wengi wao wanaangalia kama una elimu, kazi nzuri, gari mbili tatu, nyumba nk, wanasahau kuwa mali yaweza kuisha, elimu yaweza kutokusaidia, kesho unaamka unakuta umepofuka au umepata ulemavu. Je kwa wakati huo ni wanawake wangapi wako tayari kuishi na manaume kwa amani bila kumsimanga? Kumbuka hakuna jambo linalouma kama mtu unaweza kumpa kila kitu hata mama yako haumpatii, unampa first priority then anakuja kukugeuka! Wanawake hawa tuwaangaliage tu, wazuri usoni ila mioyo yao wanaijua wao na mpenzi wao nyoka!
 
Mh mfumo jiko ukoje mkuu?

Mwanamke anakuchapa kibao ukichelewa kurudi then mwanaume hutakiwi kumrudishia eti unatakiwa kupiga magoti na kusema 'baby am sori'. Ukichelewa siku ingine anakuambia ulale sebuleni yeye anajivinjari kwa bed uliyojipinda kununua kwa pesa ya mkopo! HUO NI MFANO WA MFUMO JIKE AMBAO WANAWAKE WENGI WANAUTETEA KWA KISINGIZIO CHA WAZUNGU! Imagine mwanamke anaenda bar, pub, club anarudi amelewa chakari wamemshikilia unadhani ana usalama huyo? Male friends? To hell,mie kwangu atatapika pombe yote shenz taip, na atakoma aisee! Duniani sio sehemu ya haki, na its not a place for the innocents to live, its a GUNTOWN like Don Coleone said!
 
mmh, gfsonwin this is a very interesting position, especially coming from a lady...
cartura why is it interesting? its true a man has to be a man and with all due respects as head of house. ukiona mwanaume sentensi zako hazisomeki kama ni za baba nyumbani kwako jiangalie vizuri sana. lazima tofauti kati ya mama na baba as kichwa cha nyumba iwepo na usiwe kichwa tu kisicho na macho. si unajua ni kichwani pekee kwenye organ 5 za fahamu? so watch out.
 
Last edited by a moderator:
Mke mweeema, anatoka kwa Bwana................................

Well said Fixed..wanaume wengi huoa sura na shepu nzuri badala ya kuchunguza tabia ya binti, sasa matokeo yake ndio hayo.. in a long-run kitakachoipa furaha na thamani ndoa yako ni tabia njema tu! tabia ikiwa mbaya hata shepu iwe nzuri vipi hutaiona, jamani wanaume mnaotaka kuoa mshirikisheni Mungu la sivyo mtaingia mlango wa kutoke. Aisee nimesikitishwa na hii habari hasa kitendo cha kumwacha mtoto wa miaka miwili na kwenda kunywa pombe.. ampeleke kuombewa labda ana mapepo
 

Good news i may call it ni kwamba binti amekula BAN usiku huu, natoka kwa mshkaji, kamuomba mama yake aje kukaa na mjukuu, bidada amemuvuzishwa. Imeniuma na imenisikitisha kuona wanandoa wamefikia stage hiyo kila nikimuangalia mtoto naumia kama mwanangu vile. Nimepewa jukumu la kupeleka petition ya divorce ili wagawane mali na mambo ya custody of the child na mwanamke asepe zake. The guy seems a bit releaved hata tumechoma samaki kwake na ndio nimeondoka, kiukweli aliyonieleza ni mengi zaidi, yani jamaa ana kifua aisee. Kumbe ameshawahi kumfuma mkewe na njemba akawa halali na mkewe kitanda kimoja. Leo ndo ananionyesha chumbani kwake kulivyo na partition, dah, jamani ndoa hizi. Ila wamezinguana mpaka jamaa kamnyang'anya kila kitu mpaka mahakama itakapotna tamko although wao ni wakatoliki kwa hiyo tunaanza na kusikiliza baraza wanasemaje pamoja walishapelekewa hiyo kesi na wakaisuluhisha.
 
Kama mwanamama kakataa kuwasikiliza hata wazazi wake basi hata akikalishwa chini mara kadhaa na mumewe hawezi sikia. Jamaa atumie janja ya nyani ajaribu kumtia mke wake jambajamba za kuachana aone what gone be her reaction.
 
.......dahh, another broken marriage, single parenthood and 'lost' opportunities....

Kizazi 'kilicholaaniwa!'...kua uyaone.
 

huyo mke itakuwa kapinda........
Namsikitikia hajui wanaume wanapenda wanawake walioolewa maana hawana gharama......... Ameharibu ndoa yake kwa tamaa ya muda mfupi.....
 
Reactions: Sal

hapo ndiyo utagundua kwamba, kwa baadhi yetu, hata vile viapo vya ndoa huwa ni usanii mtupu
 
katika mambo ambayo huchangia uvunjaji wa ndoa ni dharau na kutumia kivuli cha watu wengine katika kumaliza au kufanikisha tamaa zako
 
Mpe pole sana Na kama kichwa cha family akae chini na mkewe amwambie ni vitu gani hapendelei na kama mwanamama yuko tayari kuacha waendelee na ndoa kama hayuko tayari basi amweleze yuko tayari kutoa talaka .
Akili inaweza kuingia kichwani na akabadilika .

namshangaa huyo mama kwa nini aliolewa
 
Maswali gani tena haya mkuu? Si umesoma hapo kuwa ametafuta suluhu sehemu mbalimbali.

Nimesoma sana Bondpost, labda hujaelewa swali langu.
Hizo tabia za huyo mke zilibadilika ghafla?
 
Last edited by a moderator:

FL1 wamama wengi tu waliolewa wanapenda starehe, tunakutana nao sana tu sema hawa hawafanyi wanaume zao wakiwepo wanakuwa na kaunafiki flani hivi ka kujifanya wema mbele za macho ya waume zao, ila mme akiondoka na yeye ni kula bata tu,tena kwa hawa wanaume wanaosafiri safiri au wanaofanya kazi nje ya nchi pole zao, mama hakuna part anayoikosa
 

Umesema ukweli mtupu, mie mwenyewe nakumbana nao hao na wanavishawishi mashetani wale! Mara umeletewa viatu toka singapore, mara mkanda toka UK, mara unaombwa umuendeshe kwenda kigamboni ghafla anasema mpitie sunrise kula! Mara aseme your eyes are so catchy! Mara ooh eyebrows zako ni nzuri we kijana! SHINDWA WE MAMA NA UKOME! Kwenda na maukimwi yako ya uzeeni. Dunia imekwisha, hakuna imani, si wanawake wala si wanaume!
 
huyo mke itakuwa kapinda........
Namsikitikia hajui wanaume wanapenda wanawake walioolewa maana hawana gharama......... Ameharibu ndoa yake kwa tamaa ya muda mfupi.....

Mkataa pema..... Hayo maneno ndo yanamfaa, haijawahi kufikirika kuwa mshkaji anaweza kufikia huko kwani mara zote amekuwa akimshauri mkewe kwa upendo, hata jana hajathubutu kumgusa hata kofi, mke kajifanya anaomba msamaha mpaka akaanza ku-misbehave kutaka mali na mtoto. Kwa sasa anaruhusiwa kuja kumuona mtoto mchana wote kuanzia saa 12 asubuhi mpaka12 jion aondoke akalewe na friends wake alale huko huko. Mtoto amepata bibi inatosha at least akue kwanza. Kuna wanaume wanapata shida sana sababu ya wanawake. Imagine at the age of 35 uanze kutafuta wa kuoa, si ndo mwanzo huyo unaemuoa anataka kuzaa then upate mtoto mwingine at the age of 40!
 

hapo kwenye kabila la wapenda pombe ndipo sijapapenda kwani
atu wote wanaopenda pombe hawahusiani na hilo kabila na ingekua
hivyo baa zote zingejegwa huku migombani sahihisha hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…