Michango mingi imenivutia.Napenda kuongezea kuwa ili ndoa isimame au ifanikiwe kuna bare minimums zinazotakikana bila kujali pesa au usomi ambao nao una nafasi/athari zake:
1. Mmekutana wapi - wengi hupuuza sana hii lakini ina nafasi yake maana itaamua huko mbele ya safari kutakuwa vipi. Mmekutana kwenye mazingira yenye kutoonyesha uhalisia kisha mkaamua kuoana basi ni tabu na shida tupu kwa vile mtakuja kugundua mengi ambayo hamkuyatarajia na ugomvi utakuwa hauishi
2. Mna interests za kufanana? k.m mmoja anapenda kujiendeleza mwingine hapendi anapenda starehe zaidi.Hata kama usomi upo ni tatizo maana matumizi ya rasilimali yatahitaji maamuzi magumu na assuming kuwa mama ndio ana pesa zaidi au msomi zaidi baba hatapenda kusikiliza ushauri au maamuzi ya mkewe maana anajiona yeye ndio kichwa lazima asikilizwe.
3. Heshima- Kama wanandoa hawaheshimiani au dharau imetawala, basi usomi unakuwa kama mwiba kwenye uhusiano.Haijalishi ni mwanamke au mwanaume.
4. Uelewa wa pamoja kuhusu kuingia katika ndoa - wengi husukumwa kuingia kwenye ndoa bila hata kujua wanajiingiza kwenye majukumu makubwa yenye kutaka commitment kubwa pia.Wengi ndoa ni fashion au ni tamaa zaidi ya kutaka kuwa pamoja bila kujua mapenzi kama mapenzi yana maisha mafupi kabla uhalisia haujaingia.Usomi huweza kujenga kiburi cha kukimbia majukumu au kutokutaka kusahihishwa pale mtu anapokosea. Ingetarajiwa usomi usaidie watu kupima kama kweli wanaingia kwenye ndoa wakiwa well informed au wanaingia tu kama fashion.Bahati mbaya sana wasomi wengi ndio wa kwanza kuingia kwenye ndoa wakiwa ignorant kuliko wasiosoma.Wasiosoma utakuta wanaingia kwenye ndoa wakijua hasa nini wanakifuata, heshima inakuwepo, nk. Usomi + pesa = jeuri, dharau, kujiamini kwa kipumbavu, kutokujali nk.
Cha msingi ili ndoa isimame wanandoa wanatakiwa wawe na yafuatayo:
Uvumilivu, unyenyekevu, staha, Heshima, kumcha Mungu,na kujua kuwa ndoa si lele mama - ni msalaba na siyo fungate!