Mke mwema njoo, unahitajika!

Mke mwema njoo, unahitajika!

mh kufunga hapo.
Utaanza taratibu angalau mara moja baada ya miezi miwili, kisha mara moja kila mwezi. Utazoea tu. Badae utaona siyo jambo gumu maana utakuwa na Roho wa Mungu ndani yako. Usiogope dada, siyo ngumu kiviile. Nipo simple sana. Ila Mungu ni nambari wani kwangu. Vipi Upo tayari?
 
Hapo kwenye kuacha kibarua cha kudumu Mmmmh...

Usijali mkuu utapata
 
Kama Kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza.!

Umri: 28 yrs, ME.
Kazi: Ninazo.
Elimu: Inatosheleza.
Religion: Christian
Economy status: Middle class, siyo tajiri wala maskini.

SIFA NYINGINEZO
Not conservative, mcheshi, mpole, mtulivu, Upendo wa kweli upo(hutajutia)

SIFA ZA MWENZA.

MKristo, Mcha Mungu, Mvumilivu, Mstahimilivu na kama hujaokoka yaani kumkiri Mungu kwa kumaanisha na siyo kumkiri kwa mdomo tu wakati moyoni hakuna Mungu, ujiandae kisaikolojia kupata Wokovu hapo mbeleni kabla ya kufunga pingu.! (Hiki ni kigezo muhimu zaidi).

Umri usiozidi miaka 28.

Elimu angalau kuanzia kidato cha NNE ili iwe rahisi kufundishika katika masuala muhimu tutakayokubaliana.

Usiwe na mtazamo wa kupenda kuajiriwa, ujiandae Kisaikolojia kusimamia Biashara, yaani kuwa Mjasiriamali.

Usiwe na ajira ya kudumu, na kama unayo, basi uwe tayari kuvunja Mkataba ili uwe msimamiaji wa Biashara zetu wenyewe hapo mbeleni tutakapooana.

Ukiwa na Vinasaba vya wazawa wa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga au Tabora, is an added advantage. Japokuwa hiki siyo kigezo muhimu sana.!

Usiwe mshirikina, tafadhali sana, uwe Mcha Mungu wa Kweli.

Uwe unajielewa, ujiandae kuwa katika Familia ya Kuomba na Kufunga regularly.

Ujiandae kuishi maisha halisi, siyo kama yale ya Bongo Movie.

Kwetu ni kijijini siyo mjini, jiandae kutembelewa na kupata wageni wa kutosha tu kutoka kijijini.

Kama roho wa Mungu atakuwa amekugusa, basi nitumie PM. Kama siyo member wa JF na hivyo huwezi kutuma PM na una interests za kweli, basi jisajili uwe member maana haizidi dakika 5 kujisajili na kisha utasubiri kidogo Moods wakikuthibitisha utakuwa na uwezo wa kutuma PM .

NB: 1)Najua kuna watakao sema kama napenda Mcha Mungu kwa nini nisiende Kanisani, ila naamini kuwa hata kupitia Jukwaa hili kama ni Mapenzi ya Mungu anaweza patikana Mtu sahihi pia maana hata hapa pia ukiondoa wachache wasio serious, kuna Binadamu wema wenye nia njema.

2)Kama itakuwa ni mapenzi ya Mungu, tutadumu kwenye urafiki na Uchumba kwa Mwaka mmoja, kisha Mwakani mwishoni tunafunga pingu.

Usione aibu wala kulishwa maneno kuwa Mme/ Mke hapatikani kupitia mitandao. Maisha ni mpango wa Mungu. Sivyo Wanadamu wanavyofikiri.

Tafadhali sana, kama una nia ovu usijaribu kujihangaisha kwangu. Utapata shida. Sijaribiwi.!
Nafikir vigezo vyako vinatisha et kama anakaz ajiandae kuacha kaz asimamie biashara labda mwenye vyet feki ataacha kaz, pia naona unakaxia ukabila na bila shaka utakua msukuma, watakuja wasukuma wenzako, pia kumwachisha MTU kaz asimamie biashara cku biashara ikifa itakuweje, bora ungesema elimu ya darasa la saba ajue kusoma nakuandika kila ulete mrejesho pia
 
Nafikir vigezo vyako vinatisha et kama anakaz ajiandae kuacha kaz asimamie biashara labda mwenye vyet feki ataacha kaz, pia naona unakaxia ukabila na bila shaka utakua msukuma, watakuja wasukuma wenzako, pia kumwachisha MTU kaz asimamie biashara cku biashara ikifa itakuweje, bora ungesema elimu ya darasa la saba ajue kusoma nakuandika kila ulete mrejesho pia
Ahsante kwa maoni yako.! Jambo jema ni kuwa , kila mtu yupo huru kutoa maoni yake. Ilimradi heshima na utu vimezingatiwa.!
 
Hapo kwenye kuacha kibarua cha kudumu Mmmmh...

Usijali mkuu utapata
Haswaa, tena ni muhimu zaidi. Masuala ya ajira za kudumu eti Mme anaishi Kagera na Mke anaishi Mbeya kwa sababu ya kujali ajira. Hii siyo haki ya Ndoa. Ndoa ni furaha na Amani. Kazi ni sehemu tu ya kukamilisha maisha. Kazi inaweza kuwa ya kujiajiri au ya kuajiriwa. Kuwa na Fikra ya kwamba kazi ni zile za kaujiriwa tu huko pia siyo kuwa huru Kifkira, ni aina nyingine ya Utumwa uliojificha ....
 
kila la kheri mkuu ila kama umekaza sana vyuma ..yani na hali hii mtu unataka awe tayari kuacha kazi?
 
kila la kheri mkuu ila kama umekaza sana vyuma ..yani na hali hii mtu unataka awe tayari kuacha kazi?
Mkuu hii ni kwa sababu ya changamoto nilizoziona katika Wanandoa Walio ajiriwa. Yaani unakuta Mme anaishi Mtwara na Mke anaishi Mwanza. Wanatembeleana mara moja kila baada ya miezi kadhaa. Yaani ni karaha badala ya Raha. Maisha gani sasa haya ya Ndoa.? Muhimu ni kuwa, kama kuna business ambayo itakuwepo na Mungu kaijalia ipo vizuri, then Maisha yataenda kwa kudra za Mwenyezi Mungu na si Kudra za Mwajiri.
 
Wako wanaoweza kuhimili na kufunga kwa huo mwaka mmoja kabla ya ndoa hadi wakawa wananena kwa lugha na kulia machozi kanisan. Baada ya ndoa anarudi kwenye u-yeye mwenyewe
BTW kila la kheri kijana
 
Kama namwona fulani vile
Mwambie tu kijana ndo huyo
Ila ninavyokujua kwa maombi yako ya kufunga kavu tatu kwa mume huyu mtafungua kanisa sasa
hahahahahaaaaaaaa...
 
Wako wanaoweza kuhimili na kufunga kwa huo mwaka mmoja kabla ya ndoa hadi wakawa wananena kwa lugha na kulia machozi kanisan. Baada ya ndoa anarudi kwenye u-yeye mwenyewe
BTW kila la kheri kijana
Mungu haruhusu jaribu la kukushinda..
 
Kama namwona fulani vile
Mwambie tu kijana ndo huyo
Ila ninavyokujua kwa maombi yako ya kufunga kavu tatu kwa mume huyu mtafungua kanisa sasa
hahahahahaaaaaaaa...
Ha ha haaa, Mkuu..... Sasa ndo itakuwa njema zaidi. Maana tukianzisha hadi Kanisa it means tunakuwa tunatimiza Kusudi la Mungu. Na Wokovu unakuwa umedhihirisha nguvu zake......
 
Back
Top Bottom