Mke Mwizi!!!

Mke Mwizi!!!

Huko mbali...ye amwibie tu vitu akimuuliza anamwambia nimerudishia ule mfuko wa cement uliochukua juzi!

Akiiba hivyo hataumia, dawa ni kuiba kinachomuuma, akimuuliza, amwambie na yeye aache kumuibia ndo na yeye ataacha kuiba nyumba ndogo.
Balanced story.
 
Nahisi kumuibia mume ni sawa umejiibia mwenyewe, amwambie ukweli kuwa hapendezwi na tabia yake ya uizi na akiendelea mtaachana halafu asikilizie
 
Hapana, usimdhataki kwa wazee wala kumpeleka polisi!

Huyo ni wako wa maisha, si ndio? Kaeni chini mjiulize tatizo liko wapi na mtafuta ufumbuzi wa pamoja!
 
Jamani watoto wakifuata tabia ya mama hatari mtaani.
Huyu hana nia ya ndoa alikuja kuvuna. Akimaliza anaanza mbele
 
Ndugu yangu amekuja kuomba ushauri, mke wake ni mwizi, anamwibia pesa kila kukicha. Nguo zake pia huibiwa na mama watoto huyo.
Kibaya zaidi kilichomsikitisha ndugu yangu ni kuibiwa kwa mifuko ya saruji na mabati waliyotaka kuyapeleka saiti.
Mke huyo kila upotevu unapotikea, akiulizwa hajibu kitu zaidi ya kulia.
Jamaa anajiuliza amuache, awajulishe wazazi, ama ampeleke kwa wana saikoloji?
Tumshauri huyu mwenzetu nini afanye

Kama anaiba mpaka mifuko ya saruji ambane aseme anapeleka wapi inawezekana anajenga mahali huyo bila mwenzake kujua :dance:
 
Hebu mwekee mtego kwanza ili u-prove kama ni yeye ndiye anaiba. Ukimkamata anaiba kaa naye na umuulize kwanini anaiba huenda utaweza kumsaidia
 
Tabia haina dawa waungwana. Kama mtu akifumaniwa ana zini anaachwa, wizi pia inawezekana kwani hiyo pia ni amri ya mungu anavunja. Kumuibia mumeo nikama mkono wa kushoto uuibie mkono wa kulia, mwanamke gani hapendi maendeleo yake, ataendelea hivyo na ipo siku ataleta majambazi. Ikibidi amtimue tu hana huruma wala msaada nae.
 
Back
Top Bottom