Mke na mume wakiachana hugawana mali zote! Je madeni ya mume yanaruhusiwa kugawanywa ?

Mke na mume wakiachana hugawana mali zote! Je madeni ya mume yanaruhusiwa kugawanywa ?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,315
Reaction score
13,269
Hili ni swali kwa wana JF wote!

Mume na mke wakiowana ikitokea wameachana mali hugawanywa sawa kwa mke na mume, swali je kama madeni yalihusika ktk utengenezaji mali yanaruhusiwa kugawanywa kwa mke na mume pia?

Naomba nielimishwe
 
Madeni hayagawanywi.

Kama mlikuwa na biashara za pamoja, na kama biashara hiyo ni mali ya ndoa, madeni yanalipwa kwanza ndio mnagawana. Mali inauzwa kwa utaratibu wa mahakama (Mnada) na mdeni akalipwa. Benki huwa zinahusishwa katika hiyo michakato, mali ikiuzwa benki inachukua chake, kinachobaki mnapewa ndio chenu.

Mdai huwa anarifiwa juu ya amri ya mahakama kupiga mnada mali/biashara ambazo zinahusu talaka. Kutalikiana kwenu sio excuse ya kushindwa kulipa madeni, kuchelewesha au kuhamisha madeni ya watu/taasisi zinaowadai.

Kama ni biashara zenu zinadaiwa madeni, au zinalipa madeni (kama ya benki ya muda maalum), itasubiriwa mmalize madeni ndio mgawane mali/biashara hizo. Talaka huwa zinaathiri biashara na biashara inaweza kufa, hivyo mahakama itaangalia pia madeni yanalipwaje.

Kama inatokea, mmoja wenu alichukua mkopo kwa dhamana ya moja ya nyumba ya ndoa (kwa makubaliano yenu wote). Ikitokea mnatalikiana, mwenye deni anaweza kuomba atoe fedha nusu ya thamani ya ile nyumba aliyochukulia deni na kumpa mwingine, yeye akaendelea kulipa deni na akikomboa deni, nyumba inabaki ya kwake mwenyewe.

Pia mahakama inaweza kuangalia kama mali inayotaka kugawanywa haiathiri ulipwaji wa deni. Mfano; mmekopea nyumba yenu kuendesha biashara X. Nyumba hiyo haiwezi kugawanywa maana ina deni lililokopwa kuendesha biashara yenu na hati wenda ipo kwa mdai. Hapo mahakama itaangalia pia deni linalipwaje. Inaweza amuru kwanza deni lilipwe na mgao ufuate.

Mahakama inaweza kuamua kwamba biashara/mali hiyo ibaki kwa mwenye deni kati yenu, ila itatolewa mali au biashara au fedha yenye thamani nusu kumlipa mwingine akafie mbele.

Zipo talaka ambazo mahakama huwa inawasikiliza nyie mnakubaliana vipi, juu ya mali na madeni yenu.

NOTE: Lazima madeni yawe na ridhaa ya wanandoa (Spouse consent). Sio ukope bila kumshirikisha mke/mumeo ukitegemea utaangaliwa. Madeni yanayoangaliwa ni yale yenye ridhaa na lazima yawe kwa mali ya ndoa. Sio mali binafsi (mwanandoa anaweza kuwa na mali binafsi).
 
Back
Top Bottom