TANZIA Mke wa Augustine Lyatonga Mrema afariki dunia

TANZIA Mke wa Augustine Lyatonga Mrema afariki dunia

Bi Rose Augustino Mrema amefariki kwa maradhi ya moyo usiku wa jana katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa,

Hadi anatutoka, Rose Mrema alikuwa ni mjumbe wa Halmashauri kuu na kamati kuu ya TLP Taifa,

Chama na Taifa tumepoteza mtu muhimu sana katika Ustawi wake,

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam,

Ratiba zote mtazipata hapa,

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina Lake lihimidiwe daima,Tuendelee kumwombea pumziko la milele,

Amen,

IMG-20210917-WA0015.jpg
 
Rose Mrema ambae ni Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustino Mrema amefariki katika hospitali ya muhimbili Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.

“Aliugua gafla baada ya kupata mshtuko wa moyo tukampeleka Hospitali ya Muhimbili, Madaktari wanatumiambia mishipa mitatu iliziba kwa muda mrefu” ——— Mrema.

Source Millard Ayo
 
Poleni sana wafiwa na wanachama wote wa TLP
 
Pumzika salama mama yetu kipenzi 😭
Mungu akupe pumziko la milele,
 
R.I.P mama. Pole kwa familia nzima ya mzee wetu Augustine .L. Mrema.
 
Back
Top Bottom