TANZIA Mke wa Balozi Mstaafu Christopher Celestine LIUNDI, Bibi Rahma Simbaliundi, amefariji jana jioni jijini Dar es Salaam

TANZIA Mke wa Balozi Mstaafu Christopher Celestine LIUNDI, Bibi Rahma Simbaliundi, amefariji jana jioni jijini Dar es Salaam

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
MKE wa Balozi Mstaafu, Balozi Christopher Celestine LIUNDI, Bibi Rahma Simbaliundi, amefariji jana jioni jijini Dar es Salaam.

Mama Liundi amefariki akipata matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampasi kuu ya Mlimani.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo hii, tarehe 24/01/21 saa 7 mchana, katika makaburi ya Wangazija, Mtaa wa Bibi Titi Mohammed, Mkabala na Maktaba Kuu ya Taifa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Msikiti wa Al Maamur ulioko Upanga, jijini Dar es Salaam, ambako atasaliwa kabla ya mazishi.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
 
MKE wa Balozi Mstaafu, Balozi Christopher Celestine LIUNDI, Bibi Rahma Simbaliundi, amefariji jana jioni jijini Dar es Salaam...

Apumzike kwa amani.

Ila awamu hii kazi ipo.
 
Pumziko La Amani apate.

Wote walifuata imani moja au kila mmoja alibaki na yake...maana inaonyesha kama walikuwa imani tofauti.
 
Pumziko La Amani apate.

Wote walifuata imani moja au kila mmoja alibaki na yake...maana inaonyesha kama walikuwa imani tofauti.
... kilichowaunganisha sio imani bali "ndoa". Mmoja akishaondoka ndoa nayo imekwenda zake.
 
Huyu mama niliwahi kuishi naye maeneo ya keko zamani kidogo karibia na Hostel moja ya wanafunzi wa shule ya Jitegemee inaitwa BIG BROTHER
 
Siku hizi tanzia ni nyingi sana ila hutoambiwa sababu ya vifo![emoji124][emoji124][emoji124]Chukueni tahadhari ndugu zangu!
Sawa. Ingawa tunacho hofia wengi wetu, ni kutangulia. Siku ya mwisho ikifika, wote tutakufa tu.

Mpaka wale wenye 'chura' nao watakufa tu. Wapenda chura wote, nao ikifika siku yao ya mwisho watakufa tu!!!
 
Tuendelee kunawa kwa maji tiririka, hakikisha uko 1.5M toka mtu wa karibu yako. Paka sanitizer mara kwa mara na usisafiri au kwenda kwenye maeneo yenye msongamano kama hakuna ulazima.

Au nasema uongo ndugu zanguni?
johnthebaptist
 
Back
Top Bottom