Mke wa dereva bodaboda: Wanipe mume wangu hata kama atakuwa amekufa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ni zaidi ya siku 20 zimepita tangu dereva bodaboda anayefahamika kwa jina la Deogratius Shirima (34) mkazi wa kata ya Korongoni wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, kudaiwa ametoweka katika mazingira ya utata huku pikipiki aliyokuwa akitumia kukutwa nyumbani kwa Askari Polisi mkoani humo.

Mke wa Deogratius akizungumza na GADI TV akiwa nyumbani kwake wilayani humo, amesema pikipiki hiyo ilibainika kuwa ipo nyumbani kwa Askari Polisi anayetajwa kwa jina moja la Rama, baada ya mmiliki wa pikipiki hiyo kufanya kitendo cha ‘ku-track’.

Your browser is not able to display this video.
 
Swali, huyo askari ni mwana CCM au? Inabidi akamatwe mara moja kabla hajajiua.
 
Hatari sana hii.

Usalama wa raia na mali zao imekuwa tofauti.
 
Nchi imekuwa na mambo ya ajabu,huyo polisi bado yuko
Kazini

Ova
 
Askari polisi,wanaotembea na kusurura na land Rover pick up na land cruiser nyeusi kule Moshi mjini,hawajali,ni wauaji, na watekaji WA raia.
Isitoshe,ndio wachoraji wa njia za kusafirisha madawa ya kulevia kutokea Kenya
 
Kuna askari mwenye cheo hapo polisi central Moshi mjini, mzaliwa wa singida,ambaye ni mweupe,mnene, amefanya KAZI kituoni hapo zaidi ya miaka 20, bila uhamisho.

Ni mshirika mkubwa wa mtandao wa mauaji ,madawa ya kulevia na wizi
 
Askari polisi,wanaotembea na kusurura na land Rover pick up na land cruiser nyeusi kule Moshi mjini,hawajali,ni wauaji, na watekaji WA raia.
Isitoshe,ndio wachoraji wa njia za kusafirisha madawa ya kulevia kutokea Kenya
Acha tu jamaa yangu kuna yule alikuwa ana bonge la mkono miaka ile kwenye cruiser nyeupe. Bado yupo au amekufa? Msenge yule ni mafia kwa kupoka fedha na kipigo hajali. Ila Mungu yupo natumai atakuwa ameshamlipa.
 
Wananchi wa Tanzania hivi brain zetu zina mutation gani. Ati mama samia aliangalie suala hili . We have a problem somehow ila hatujui tuu.
 
Ni muda Sasa wa wasiojulikana kuanza kujulikana .. Pastor Mtalemwa voice.
 
juzi napiga story na askari mmoja ananiambia yeye alimpa baba yake kuhusu mambo matatu ambayo ni kujiepusha na kuua, kwenda jera na kutenda haki.....sidhani kama askari wote haya wanayajua
 
Mfumo wa police ya sasa, ni ya enzi za ukoloni. Itoshe sasa na kama taifa tuone mabadiriko kuwa ni ya lazima.
 
Tayari washampoteza huyo, hapo pikipiki walikuwa wanabadili usajili irudi kijiweni.

Bila mkubwa kuingilia kati ushahidi utapotezwa na kesi kuzungushwa + vitisho vya kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…