Mke Wa Dr. Salaa Josephine Alonga Na JF

Status
Not open for further replies.
kukosea kunukuu kifungu cha bibilia umeona kosa kubwa sana ambalo hawezi kulifanya,ila kuvunja kiapo cha ndoa halali iliyofungwa kanisani kwa mkristo safi kama yeye kwako its ok
ukipenda sana chongo unaona kengeza
 
Hata ukisikia ukweli wa ndoa yake wewe itakusaidia nini na mke wako.
 
heri JK kuliko mbaka demokrasia na mtu aliyeshindwa kutimiza kiapo na muumba wake leo anazuga ataweza kutimiza ya binadamu
======

Hii ni sawa na kusema, heri kubaka binti yako kuliko kuiba mke wa mtu!? Screwed logic!
 
Ulitaka Slaa akuoe wewe au unabinti anataka mme mlete mimi nataka wa pili, unajifanya uko serious kujua ndoa za watu wakati yako inakushinda acha unazi wako.
 
Bi Josephine, kama kweli ni wewe na haya ndiyo maelezo yako basi naona kama umechanganyikiwa...maana unatuzonga tu hapa.
Kwanza nataka nikupe ushauri wa bure, JF siyo jukwaa sahihi kwa wewe kujisafisha, maana siyo hapa ulipochafuliwa. Harufu ya uvundo wa kashfa zako wanazijuwa Watanzania karibu wote na wao hawajaanza kuzipata kutoka JF.

Nakushauri urudi huko ulikochafuliwa ukajisafishe, usipumbazwe na JF, ukisikia kuwa ni jukwaa la chadema na huyo unaedai "mumeo" anaabudiwa hapa,ukadhani ndiyo inatosha kujisafishia!!!
Bi Josephine, mimi ninashaka na kauli zako, umeshindwa kusema hasa kama madai ya Mahimbo ni kweli ama uwongo, umebaki kusema 'anatumiwa'.

Yeye anadai kuwa wewe bado ni mke wake halali na ushahidi katoka, mahala mlipofunga ndoa na mtu mchungaji aliyekufungisheni. Wewe unadai umeachika, hujasema lini umeachika, chombo kipi kimevunja ndoa yenu? Sheria za ndoa za nchi hii zinajuulikana, kuanzia za kimila, kidini na kiserikali, na zote hizo zina utaratibu wake wa kufungwa na kuvunjwa. Hebu twambie hiyo yako wewe imefungwa kwa utaratibu upi na imevunjwa kwa utaratibu upi?

kwa maana, kama umeondoka tu kwa mumeo na bila ya talaka, ujuwe ume desert ndoa yako, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Sijakufahamu unaposema kuwa Dr. Slaa ni "mumeo" wakati yeye amesema kuwa wewe ni mchumba wake, ni vitu tofauti, unawezaje kuwa mchumba wakati huo huo uwe mke wa mtu?

Unawezaje kuishi na mtu ambaye hajakuowa, halafu wewe unasema mumeo? au niwe sijuwi tafsiri ya "mchumba" na "mke", maana mimi ni mtu wa pwani!

Bi Josephine, unapodai kuwa Mahimbo ametumiwa, sijuwi unamaanisha nini, wewe hujasema kuwa si mke wa mtu, yeye kasema wewe ni mkewe, ukumbuke upo karibu na mtu ambaye watanzania wanataka kumpa dhamana ya kuwaongoza, linapokuja jambo kama hili, watu watataka kujuwa vipi kiongozi wao mtarajiwa yupo katika dialemma kama hii.

Au hujuwi kuwa mambo ya ndoa yanaweza kuangusha serikali? si unakumbuka sakata la Clinton na Monica Lewinsky? halmanusra bunge limshitaki rais, kwa maana serikali yake ingeanguka!
Bi Josephine, upo njia panda na nishaona unahangaika sasa, nakushauri tafuta ulipojikwaa na siyo ulipoangukia.
 
Hata ukisikia ukweli wa ndoa yake wewe itakusaidia nini na mke wako.
ili tujue kama ni muadilifu au muhuni anarukia tu wake za watu, asije kurukia na mali za uma tukimpa nchi
 

======

Kamwambie Lipumba atuonyeshe mke wake.
 
Ulitaka Slaa akuoe wewe au unabinti anataka mme mlete mimi nataka wa pili, unajifanya uko serious kujua ndoa za watu wakati yako inakushinda acha unazi wako.
na kwa majibu hayo mtaishia kusema haiwezekani karatasi za kura zimefojiwa, ukipiga chadema kura inahamia ccm
 

Join date August 2010
 
Asante sana ICHONDI kwa angalizo hilo inawezekama kweli hii post imepandikizwa na huyo si Josephine tunayemjua, maana watawala wana mbinu nyingi. So kuanzia sasa nitakuwa makini sana.

Pia angalizo jingine mleta hoja nimeanza kuwa na wasi wasi naye toka aanze kujitokeza kutuletea vitu live hapa, sihoji kwa nini analeta vitu live lakini kuna baadhi ya mabandiko yake ukiyafuatilia yanawalakini, jaribuni kufuatilia mabandiko yake. Isije kuwa tumeingia kwenye gari tofauti, kuna watu walikuja na mbinu hiyo tukawaamini ili iwe rahisi kututeka lakini wakakuta JF hawadanganyiki.
 

Kanyafu Nkanwa; unavyosema siyo vyema. Kama wewe uko kwenye ndoa,utakuwa unajua matatizo yaliyoko kwenye ndoa. wako watanzania wengi katika ndoa ambao hawaelewani kwa sababu ambazo wameshindwa kuzitatua, badala ya kufanya maamuzi, wanaanza kwenda kwa nyumba ndogoz badala ya kumaliza tatizo au kuachana. Kama Josephina aliachana na huyo ambaye walikuwa hawaelewani na kuamua kuungana na yule ambaye moyo wake umemtuma kuwa anamfaa, mimi nampongeza.

Hilo Gazeti ambalo liliandika kama linajali maisha ya viongozi mbona hawaandika maisha ya Jk na hizo "several small houses" MAWANI
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…