Natumai umenukuu hayo uliyoyaandika kutokana na yale yaliyoandikwa kwenye "Habari Leo" na "CHANGAMOTO". Mojawapo ya Amri Kumi za Mwenyezi Mungu (ambazo ni kwa watu wote) ni ile amri inayosema "Usimshuhudie jirani yako uongo".
Mfumo wetu wa jinsi ya kutenda haki unawataka anayeshtaki na anayeshtakiwa wapewe haki sawa. Kwa Mhariri wa gazeti kuandika tuhuma za upande mmoja, sio tu kwamba anakuwa hajatenda haki, lakini anakuwa amekiuka maadili ya uandishi wa habari.
Unadai kwamba mama Josephine "amewaacha watoto nyumbani na kwenda kujirusha na Slaa kule Mtongani", hebu tukuulize: ULIKUWAPO? UNA UHAKIKA?
Habari za kusikia, au kusoma kwenye gazeti, kamwe haziwezi kuwa ushahidi unaokubalika mahakamani. Zinaitwa "hearsay evidence", yaani, "ushahidi wa kufikirika".
Kabla hujahukumu, tafuta ushahidi usiopingika, usiwe MSHABIKI! Ushabiki utakuponza, kama ulivyowaponza wana-CCM wengi.
Hizi ni njama za CCM - kuwatafuta mamluki - kumchafua Slaa. HAWAMCHAFUI, bali, WANAMJENGA! Kama si kweli wanafanya hivyo, hakukuwa na sababu ya KUGAWA BURE nchi nzima kijarida cha CHANGAMOTO, tena baada ya kuchapisha nakala 45,000, wakati kijarida kile kinachapishwa si zaidi ya nakala 5,000 kwa wiki!
Mungu Ibariki Tanzania! Tuepushe na mafisadi hawa!
-> Mwana wa Haki