Mke wa Jose Chameleone ashuhudia mmewe akitandikwa mabanzi na P-funk majani Kampala

venchwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2016
Posts
1,677
Reaction score
1,596
habarini zenu wajameni
kwa wale wanaofuatilia mziki wa bongo fleva, na wa afrika mashariki kwa ujumla matumaini yangu ni kwamba mnamjua mtayarishaji wa beats maarufu kwa jina p-majani kinywele kimoja,

Mwaka 2005 na 2006 alitayarisha mlio wa mziki ambao ulitumika kwa wimbo wa mwanamziki nguli Joseph Haule maarufu kwa jina Professor J, wimbo kwa jina unaitwa nikusaidieje,

Jose chameleone kwa ujanja ujanja akasema akaiba beat ile na kutumia kwenye mziki wake wa bombo crat, ambayo ilifanya vyema nchini uganda,

Baada ya mwenye mali kugundua kuwa kaibiwa, akawasiliana na chameleone. na majibu ya chameleone ikawa kama anaomba msamaha fulani hivi na akaahidi kulipa dola za kimarekani 2400, miaka ikakatika miwili bila kulipa , majani akakaa kimya kwa kujua kwamba basi ngoja asamehe,

Mwaka 2008 nchini kenya kulikuwapo na programu ya kutumia miito ya simu ya ala zinazoendana na beats au milio ya mziki iliyotengenezwa na wasanii mbali mbali au watayarishaji , MTN ilishirikiana na kampuni ya nje ya uganda waka lounge hiyo program kenya, ule mwito wa beat ya nikusaidieje ukatumika kwenye ring tone , na wakalipa dollar 12,000 Jose akaenda akiwahi akachukua hiyo hela, jambo ambalo limemkwaza sana bwana p-funk akamtext chameleone akakaa kimya

hatua alizochukua majani ni kwenda KOSOTA, wakamzungusha akaenda uganda kudai kwenye chama cha wanamziki na utayarishaji wa filamu, wakamzungusha saana, akaamua kuachana nayo,

mwaka huu 2017 march marekani kuna watayarishaji wa filamu , katikla filamu moja wakaomba kutumia beat ya P-funk majani ya nikusaidieje lakin wakataka kwanza wawasiliane na muhusika wa mziki, confusion ikaja pale nani wamuone either Chameleon wa bombocrat, au Profesa J wa nikusaidieje,

baada ya chameleone kujua kuna dili ilo akapanda ndege akaenda USA, akakutana nao wakasaini mkataba wa maisha atalipwa milele kutokana na mauzo ya filamu ile na wakampa advance 50,000 USD, kama advance payment, Yaan milion 120 za Tanzania

Mbabe Majani baada ya kujua hayo akaenda direct kampala kupata go ahead , akapata vibali vyote akaenda USA kushitaki ,taratibu ziko za kisheria ambazo kafuata, kaambiwa kuwa concert mawakili mpaka kwanza awe na USD 20,000 ili kesi yake kusimamiwa,

Chameleone alivyosikia hayo akampigia majani akasema nataka nikuwekee ile dolla 2000 tuliyokubaliana mwanzo ili tusifike mbali, majani akasema nitakutafta,

Wiki hii wamekutana kampala , akamkabidhi kwanza vibao vya kutosha mke akataka kuingilia kati majani akamshika nywele naye mke akaponyoka akakimbia,
si mara ya kwanza kwa chameleone kuwatapeli watu ni tabia yake na ana conflict na ndugu zake na wasanii wa uganda


kesi ya madai majani kafanikiwa kuifungua marekani na wanaendelea na utaratibu


uzuri wamekubali kumlipa hao wa hollywood watayarishaji wa movie, na wamesema kumwendea jose chameleone kurefund hela yao na kuchange mkataba

malalamiko ya majani p funk NA VIDEO ILIYOTUMIA MZIKI HUO CHINI IPO NI 1.52 MINUTES WHATCH IT

 
Hapo majani ana haki kabisa na biti ya nyimbo zote mbili na ringtones na huko kwenye movie. Ila naona jamaa ni mbabe sana, ngoja nitamlengesha kwa wale jamaa wa ununio wampe discipline😀😀
 
P. Funk kweli mtemi.. ugenini ila anakutia vibao ... hapo ameonesha tofauti kubwa sana na watanzania wa kawaida... ile tabia yetu ya kusema namwachia Mungu inatufanya wageni watuone mazuzu
 
P. Funk kweli mtemi.. ugenini ila anakutia vibao ... hapo ameonesha tofauti kubwa sana na watanzania wa kawaida... ile tabia yetu ya kusema namwachia Mungu inatufanya wageni watuone mazuzu
HAHAHA KAGAWA MABANZI NA WALE WALIOTAYARISHA ILE MOVIE WAMEAHIDI KUMLIPA NA KUMUENDEA CHAMELEONE
 
Ila.kweli huu upumbavu aliofanya camelion ni haufai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…