Mke wa Kombo alivyosimulia jinsi Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana na juhudi zilizofanyika kumtafuta Julai 2, 2024

Nimesikitika sana.....Na shemeji sasa aachane na hayo manguo ya rangi za kijanikijani
 
Watanzania mna matatizo gani? Kila siku ni ''ifike mahali''. Ifike mahali gani? Hivi unadhani wanafanya haya bila Samia kujua? Ni lini umeshasikia wahusika wakikamatwa au hata juhudi za kuwafuatilia zikifanyika?
Rais hajui mengi sanaa, you have no idea how much she doesn't know.

Na hivi vyombo vya ulinzi na usalama anaviogopa kwa kiasi fulani. Mwanzoni alipojaribu ku push reforms wakaibuka panya road na majambazi wanaotumia silaha, ikabidi anywee na kuwaacha wanendelee kuwapiga risasi na kusema "mtuhumiwa alijirusha toka kwenye gari akafariki". unadhani ile ilikuwa coincidence??
 
Wazo bora sana hili. Uwe ni uamuzi wa kuliokoa taifa.
 
Rais anajua
Rais anajua yote ndugu yangu...hajajigeuza chura kiziwi hivihivi....ni kwamba anasikia kelele na malalamiko yote
 
Watanzania mna matatizo gani? Kila siku ni ''ifike mahali''. Ifike mahali gani? Hivi unadhani wanafanya haya bila Samia kujua? Ni lini umeshasikia wahusika wakikamatwa au hata juhudi za kuwafuatilia zikifanyika?
Tuna matatizo ya ajabu sana kama nchi, sijui kwa nini!
Kuna kitu hakiko sawa. Hebu fuatilia tu hata baadhi ya maoni yanayo andikwa humu. Yanatia shaka sana kama akili zetu zipo sawasawa.
 
Kwa nini usimpeleke Samia mwenyewe huko akafundishwe namna ya uongozi bora?
Matatizo yote yanaanzia kwenye ngazi hiyo kutelemka chini.
Unakwenda kufundisha polisi, unawaleta kwenye mfumo ulio oza halafu utegemee watafanya kazi nzuri?
 
Unajitahidi sana kutetea ujinga, sijui unafaidika nao vipi!

Huu ndio ushauri ambao ungempa Samia kama angekuteua uwe mshauri wake?
 
Huu ndio upumbavu wanao fanyiwa waTanzania. Huyu alijuwa alipo huyo mateka, na siyo ajabu alitekwa kwa amri yake DC.

Ushenzi huu lazima ukomeshwe.
NIna wazo kama lako mimi mashaka kwa Msando DC,wote waliokengeuka CHADEMA wanajifanya wanajua mbinu za kuinyong'onyeza eti...Amini huyo kijana atakuwa ni tishio kwa CCM na mtetezi wa watu na jamii inamkubali na pengine ametia nia hata ya kugombea udiwani
 
Unajitahidi sana kutetea ujinga, sijui unafaidika nao vipi!

Huu ndio ushauri ambao ungempa Samia kama angekuteua uwe mshauri wake
Uhalisia wa mambo huwa hauiwi "mzuri" na wenye kuwaridhisha wote.

Wakuu wa taasisi tu wanashindwa kujua kila linaloendelea kwenye taasisi zao, sembuse rais wa nchi nzima.
 
Kwa nini usimpeleke Samia mwenyewe huko akafundishwe namna ya uongozi bora?
Matatizo yote yanaanzia kwenye ngazi hiyo kutelemka chini.
Unakwenda kufundisha polisi, unawaleta kwenye mfumo ulio oza halafu utegemee watafanya kazi nzuri?
Is your suggestion realistic?? Hali iliyopo ndio hii, uipende au uichukie lakini ndio uhalisia wenyewe, unapotaka kushauri jambo lolote lazima suluhu yako iwe na uhalisia. Kinyume chake utakuwa unaongea mambo ya kufikiria.
 
Mbona kuna matukio mengi na yeye amekaa kimya? Hivi yule aliyetaka kulisha fisi na mamba mwili wa binadamu kule Katavi amechukuliwa hatua gani? Alisema alipelekwa Oysterbay polisi, na akaja mhuni mwenye jezi ya simba kumhoji!
Mpaka uthibitisho wa maneno ya mtekwaji beyond reasonable doubt. Aliyetekwa naye haaminiki sana kwenye maelezo.
 
Utekaji umefanywa na vyombo ambavyo Raisi anaviongoza. Kwa sababu hiyo Raisi anastahili lawama. Kama Raisi hajahusika, na hataki kulaumiwa, basi anapaswa kuwafuta kazi waliohusika.
Kwenye Awamu ya 5 mambo watu wengi waliathirika kwa maamuzi ya kukurupuka kwa vile Magufuli alikuwa anafukuza watu bila kufuata sheria. Na Mahakamani kuna kesi nyingi ambazo waliofukuzwa wanadai fidia.

Tuache rule of law itamalaki. Atuhumu mtu wa kwanza, achunguze mwingine then mamlaka ya nidhamu ichhukue hatua baada ya ripoti ya uchunguzi
 
Ila jana au Leo amelisifia jeshi la polisi Eti linafanya kaci nzuri sana na Kwamba nchi imetulia eti.
Kama unataka kujua whether Jeshi la Polisi linafanya kazi au halifanyi kazi, pata taswira ingekuwaje bila Jeshi la Polisi.

Hapa Mwenge makutano ya Sam Nujoma Rd na Ali Hassan Mwinyi Road/ Bagamoyo Road kusipokuwa na Traffic tu Wilaya za Ubungo na Kinondoni zinasimama. Na hao ni Traffic Police tu

Tukio moja ambalo bado tunasubiri ripoti haliwezi kuharibu kazi pevu ya Polisi
 
Sasa tumeshajua chura kiziwi, kauli yake hiyo. Yeye ananyamaza, kazi wamepewa polisiccm kumalizana na wananchi. Aibu yenu, kumkamata mwananchi, kumuweka mahabusu siku 29 bila kumpeleka Mahakamani.


Mnamfanyia nini siku zote hizo? Mngemuua mngesema mko naye? Kazi yenu ni kulinda raia na mali zao. Mmegeuka genge la utekaji, kumfurahisha mtu mmoja, hizo damu na utesaji ziwe juu yenu na vizazi vyenu.
 
Tukio kama la kutekwa huyo jamaa unahitaji uchunguzi kweli? Raisi anastahili lawama kwa matukio hayo kwasababu yanafanywa na vyombo vya dola anavyo viongoza. Na majuzi tu Rais alipokea ripoti ya tume ya haki jinai halafu vyombo vyake bado kinaendelea na utekaji.
 
Daaaa! Suala lipo kwenye uchunguzi wa polisi? Polisi imekiri kumshikilia. Polisi wanachunguza Nini hapo?Je huo ni ukamataji Gani? My country 😭 hakika majambazi ni wengi
Kwa siku 29????
 
Asingekubali kufuatana na huyo mhuni aliyemwambia akaona nyaraka. Angemvurumusha na kumwambia kama aende zake akadai hizo fedha, japo wangeweza kumfuata tena kwa njia nyingine.
Abduction Squads have several Techniques for Abduction of their Targets. It's an extremely difficult to detect an Abduction attempt unless you get tipped by good Samaritans.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…