Mke wa Kombo alivyosimulia jinsi Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana na juhudi zilizofanyika kumtafuta Julai 2, 2024

Mke wa Kombo alivyosimulia jinsi Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana na juhudi zilizofanyika kumtafuta Julai 2, 2024

Tuliopitwa na tukio hili pitia hapa ambapo mke alisimulia kupitia gazeti la Mwananchi mume wake Kombo alivyotekwa na watu wasiyojulikana - Jumanne Julai 2, 2024

====

Handeni. “Niliamka asubuhi nikaanza kufanya usafi, akaja mtu mmoja akawa anazunguka hapa nyumbani kwetu, tukasalimiana, akaniuliza “huu msingi (wa nyumba) anayepandisha ni nani”? Nikajibu mama na mume wangu wanajenga hapa, akataka kuniuliza maswali zaidi, nikamwambia anisubiri nimuite mhusika.

“Nikaingia ndani nikamwambia mume wangu kuna mtu yupo nje nimemuona anazungukazunguka hapa nyumbani, ila simfahamu lakini anaulizia msingi unaojengwa ni wa nani, kamsikilize. Ndipo mume wangu akatoka nje na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kuongea naye.”

View attachment 3042253
Mke wa Kada wa CHADEMA Kombo Mbwana, Mariam Rajabu

Ndivyo Mariam Rajabu (20) anavyoanza kusimulia jinsi alivyoshuhudia mumewe, Kombo Mbwana, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akichukuliwa na watu wasiojulikana Jumamosi Juni, 15, 2024 akiwa nyumbani kwake, Kijiji cha Komsala, Kata ya Kwamatuku, Handeni Mkoa wa Tanga.

Anasema baada ya kumweleza alichokuwa anahoji mtu huyo, Mbwana alitoka kwenda kumsikiliza.

Mariamu anasema katika mazungumzo yao, alimsikia mtu huyo akimwambia mumewe kuwa eneo hilo ameuziwa yeye tayari na ni shamba la ekari tatu, kama atahitaji kuona nyaraka, waende kwenye gari lililokuwa limeegeshwa jirani na nyumba yao akazione.

“Basi wakaondoka kuelekea kwenye gari huku wakionyeshana eneo na alipoingia tu kwenye gari, nilishtuka kuona gari hilo linaondoka kwa kasi. Ndiyo mpaka leo sijamuona tena mume wangu na sijui chochote kumuhusu yeye na hakuna mawasiliano,” anasimulia Mariam mwenye mtoto mmoja.

Pia soma: Polisi yakiri kumshikilia Kada wa CHADEMA Kombo aliyedaiwa kutoweka kwa siku 29!

Anasema bado anajiuliza nini kimempata mumewe na sababu ya kuchukuliwa kwake.

“Hivi sasa naishi kwa shida sana, yeye ndiyo nilikuwa namtegemea kwa kila kitu,” anasema dada huyo.

View attachment 3042259
Kombo Mbwana

Anasema licha ya kuwa ya shemeji yake kumsaidia mahitaji madogo madogo, bado hali si nzuri, kuna siku hulazimika kupata milo miwili tu asubuhi na jioni kwa kuwa chakula hakitoshi.

“Naiomba Serikali imtafute mume wangu wapi alipo nijue, nina mtoto mdogo ambaye anahitaji huduma nyingi na baba yake, ndiyo alikuwa kila kitu,” amesema Mariamu.

Kombo Mbwana mkazi wa kijiji cha Komsala kata ya Kwamatuku wilaya ya Handeni ambae ni kada wa Chadema anayedaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana tangu Juni 15,2024.

Akizungumzia hilo, Mark Sango (20) mdogo wake Mbwana pia ameiomba Serikali kuongeza nguvu ya kumtafuta yake yake.

“Hatujui hawa watekaji wanania gani, je ndugu yetu bado mzima au kuna kitu wamemfanya, familia nzima hatuna amani,” amesema Sango.

Amesema licha ya kuendelea kumsaidia shemeji yake kupata mahitaji muhimu, hali si nzuri kwa sababu hana kipato.

"Baada ya kaka kuchukuliwa majukumu yake tunayabeba na sisi, licha ya kwamba sina uwezo wa kuyabeba kama kaka mwenyewe, lakini inanibidi nipambane, tuna mtoto mdogo hapa, lazima nimsaide shemeji,” anasema Sango.

Hakuna shamba lililouzwa

Akisimulia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Komsala, Joseph Minango amesema hana taarifa kama shamba la Mbwana limeuzwa kama ilivyodaiwa na mtu aliyeondoka naye.

“Ninachofahamu mimi na ofisi yangu, eneo hilo ni mali ya Mbwana, labda kama kuna mauziano yalifanyika zamani kabla ya mimi sijaingia madarakani. Lakini cha kujiuliza kwa nini wameondoka naye na hajarudi mpaka sasa,” amehoji Minango.

Amesema wao kama serikali ya kijiji wanaendelea kufuatilia kwa karibu tukio hilo ambalo tayari lilisharipotiwa kwa Jeshi la Polisi.

Awali akielezea tukio hilo, katibu wa Chadema Jimbo la Handeni Mjini, Kombo Matulu alisema wamefuatilia sehemu mbalimbali lakini hawajapata majibu yupo wapi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando amesema tukio hilo lipo kwenye uchunguzi chini ya Jeshi la Polisi na amewaomba wanafamilia na wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikilishughulikia.

“Serikali haijawahi kushindwa jambo, nawaomba tuwe watlivu,” amesema Msando.

Vilio vya watu kutoweka na kutekwa vimeendelea kuibua hofu na wasiwasi nchini, huku wadau wakiinyooshea kidole Serikali kwa kushindwa kuvikomesha.

Kwa mujibu wa wadau hao wa kada mbalimbali, pia vipo viashiria vya ushiriki vyombo vya dola, ikidaiwa baadhi ya watekaji wanapomchukua mtu hudai wao ni askari, madai ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni ameyakanusha akisema ni uhalifu kama mwingine.

Duh. Yaani wasiojulika wapo mpaka vijijini ...... Halafu juzi nimesikia Maza kasema anafanyia kazi maoni ya Tume ya Maadili sijui. If it's true basi aongeze kasi ..... Il;a kwa jinsi anavyoyakalia kimya haya matekaji, inawezekana yeye ni mfaidia wa haya.
 
Abduction Squads have several Techniques for Abduction of their Targets. It's an extremely difficult to detect an Abduction attempt unless you get tipped by good Samaritans.
Ni kweli kabisa. Ila kwa hali ya kawaida mtu hawezi kuja nyumbani kwangu aniambia eti kuna mtu amemuuzia nyumba yangu hivyo niende naye akanionyeshe. Hata kama hana nia ya utekaji lakini ni lazima nitamtoa nduki.
 
Tambua tu kwamba Kuna mbinu nyingi sana zinatumika katika Operesheni za Utekaji-nyara.
Je, vipi katika Operesheni ya Utekaji akitumiwa Kiongozi wako wa Serikali ya Mtaa ambaye unamfahamu vizuri au akitumiwa ndugu yako wa damu wa karibu sana naye utaweza kumtoa nduki??????
 
Hujanipa hata kidogo. Najua sana kuna mbinu nyingi za utekaji wala sihitaji kuambiwa. Unaweza hata kupigwa kikumbo kwenye mtaa ulio busy ukaingizwa kwenye gari kwa haraka na watu wasijue. Sasa tuachane na suala la utekaji kabisa. Wewe umekaa nyumbani kwako halafu anakuja mtu anaanza kuulizia ulizia kuhusu nyumba au kiwanja ulichojenga na ambacho unajua ni chako. Anakwambia kuwa kuna mtu amemuuzia, kama huamini twende kwenye lile gari pale nikakuonyeshe hati. Hivi kweli mtu wa aina hii unaweza kumsikiliza na kwenda naye? Mmi kwangu ni big no na tena nitamtimua vibaya sana. Nitamwambia nenda kaleta aliyekuuzia na nitakuwa mkali sana unless kama hicho kiwanja sina uhakika kama ni changu.
 
Uhalisia wa mambo huwa hauiwi "mzuri" na wenye kuwaridhisha wote.

Wakuu wa taasisi tu wanashindwa kujua kila linaloendelea kwenye taasisi zao, sembuse rais wa nchi nzima.
Wewe kweli ni uchwara....unafikiri ni yupi mtu sahihi wa kubebeshwa lawama juu ya mambo haya????!Tuambie basi....
 
Uhalisia wa mambo huwa hauiwi "mzuri" na wenye kuwaridhisha wote.

Wakuu wa taasisi tu wanashindwa kujua kila linaloendelea kwenye taasisi zao, sembuse rais wa nchi nzima.
Nina mashaka kama unaelewa unacho kiandika hapa!

Pamoja na kwamba hilo la "...rais, au wakuu wa taasisi.." kushindwa kujua kinachotokea ni hoja mbovu kabisa; lakini unajifanya hujui sababu za kuwepo na hali mbovu hiyo katika maeneo hayo.
 
Is your suggestion realistic?? Hali iliyopo ndio hii, uipende au uichukie lakini ndio uhalisia wenyewe, unapotaka kushauri jambo lolote lazima suluhu yako iwe na uhalisia. Kinyume chake utakuwa unaongea mambo ya kufikiria.
LOOooooh!

Kwa hiyo waTanzania wapende au wasipende, ni lazima wakubali hali hiyo mbovu?
Wewe upo kwenye ngazi tofauti sana ya uelewa wa haya mambo!

Hata hivyo, mkuu 'Mzalendo...' naona tuliache hili, maana sioni jinsi tunavyoweza kukubaliana kati yetu juu yake.
 
Wewe kweli ni uchwara....unafikiri ni yupi mtu sahihi wa kubebeshwa lawama juu ya mambo haya????!Tuambie basi....
Mtu sahihi wa kubebeshwa lawama kwa madhila kama haya ni Wananchi wenyewe kutokana na wao kuzubaa na kukubali kuwa wajinga na/au waoga wa kudai au Kupigania haki zao za msingi ikiwemo na kudai Katiba nzuri ya nchi yao.
Kumbuka: "Haki huwa haitolewi kama zawadi na mtu mdhalimu, ni lazima ipiganiwe na wale watu wanaodhulumiwa."
Martin Luther King Jr.
 
Ni kweli kabisa. Ila kwa hali ya kawaida mtu hawezi kuja nyumbani kwangu aniambia eti kuna mtu amemuuzia nyumba yangu hivyo niende naye akanionyeshe. Hata kama hana nia ya utekaji lakini ni lazima nitamtoa nduki.
Huyo kijana msimlaumu alikuwa hajawahi kutekwa. Polisi walijaribu kumteka Mdude Chadema, akiwa tayari ni mzoefu, akawashtukia akiwalengesha eneo lenye mkusanyiko wa watu na akapiga mayowe. Polisi ikabidi wawe wapole.
 
Mtu sahihi wa kubebeshwa lawama kwa madhila kama haya ni Wananchi wenyewe kutokana na wao kuzubaa na kukubali kuwa wajinga na/au waoga wa kudai au Kupigania haki zao za msingi ikiwemo na kudai Katiba nzuri ya nchi yao.
Kumbuka: "Haki huwa haitolewi kama zawadi na mtu mdhalimu, ni lazima ipiganiwe na wale watu wanaodhulumiwa."
Martin Luther King Jr.
Wewe unaliweza hilo? Tuanzie hapo
 
Huyo kijana msimlaumu alikuwa hajawahi kutekwa. Polisi walijaribu kumteka Mdude Chadema, akiwa tayari ni mzoefu, akawashtukia akiwalengesha eneo lenye mkusanyiko wa watu na akapiga mayowe. Polisi ikabidi wawe wapole.
Mkuu sijamlamu hata kidogo. Nilikuwa nasema upole usizidi sana. Kutekwa wangeweza kumteka hata kwa njia nyingine lakini kwa hali ya kawaida mtu akija kuuliza uliza mambo ya nyumba yako na kusema ameuziwa sehemu huyo ni wa kufukuza kama mbwa.
 
Back
Top Bottom