Elections 2010 Mke wa Madaraka Nyerere Kugombea Ubunge CHADEMA - Jimbo la Kwimba

Elections 2010 Mke wa Madaraka Nyerere Kugombea Ubunge CHADEMA - Jimbo la Kwimba

Sakila hagombei tena amejikatia tamaa!

Leo nilikuwa nazumgumza na Mama Leticia akaniambia kuwa yeye anatamani sana huyo mhindi apite ndio atakuwa mwepesi zaidi kwake, anadai kama angeweza kufanya kampeni ili apitishwe ndani ya chama chao angefanya hivyo.. Inasemekana huyo mhindi anamougopa Leticia..Lets wait and see!

By the way mmeniudhi kuniletea sredi yangu huku ingawa ni ndio mahali pake. Watu hawaji huku hivyo ujumbe haufiki kwa wengi..Watu bado hatujalizoea jukwaa hili labda kwa kuwa wakati wake rasmi bado!

Na hiyo ndiyo Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ya kweli.....huu sio wakati wa kutanguliza hofu ya fedha za mtu...ni wakati wa kusimama na kutetea unachoamini.

bravo mama letisia nakutakia mafanikio mema katika uchaguzi huu....usiende kwa waganga mwamini MUNGU atakufanikisha ( ni ushauri tu)

Mix with yours
 
Sidhani kama ana imani na ushirikina.
 
Familia ya Hayati Mwl Nyerere inaanza kujiengua kidogo kidogo CCM. Hii ni ishara ya nini?
 
Haya bana umeshinda wewe ila huyu mama anajiamni kuliko unavyodhani..

Inawezekana anajiamini kuliko ninavyodhani, lakini tukimuweka kwenye ultimate test ya kujiamini anashindwa.

Ultimate test ya kujiamini ni kuweza kusema "mimi nina uhakika ndiye chaguo bora kabisa, mleteni mtu yeyote tushindane naye nitamuangusha". Hii ndiyo lugha ya washindi wanaojiamini.

Mtu akishaanza kusema "Napenda fulani apite, kwa sababu atakuwa mpinzani dhaifu na mimi nitapata afadhali" anaanza kuonekana hajashinda ile ultimate test ya kujiamini.
 
Yawezekana ni kweli hawataki kubebwa au wanakimbilia masilahi. Maana enzi zile mmoja wa familia hii anagombea ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi kule Arusha, mama yake alikuwa anamsaidia kupiga debe.
Hata hivyo familia hii inaijua vizuri CCM maana ilipikwa na kupakuliwa kwao. Sasa wanaona inaliwa na wengine.
 
Inawezekana anajiamini kuliko ninavyodhani, lakini tukimuweka kwenye ultimate test ya kujiamini anashindwa.

Ultimate test ya kujiamini ni kuweza kusema "mimi nina uhakika ndiye chaguo bora kabisa, mleteni mtu yeyote tushindane naye nitamuangusha". Hii ndiyo lugha ya washindi wanaojiamini.

Mtu akishaanza kusema "Napenda fulani apite, kwa sababu atakuwa mpinzani dhaifu na mimi nitapata afadhali" anaanza kuonekana hajashinda ile ultimate test ya kujiamini.

Umeshinda wewe,you might be right kwa mtazamo wako...
 
Wakuu habari!

CHADEMA imeendelea kujiongezea hazina ya wanawake wazuri wanaowania majimbo kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge mwezi Oktoba mwaka huu.

Kati ya wanawake hao mmoja wao ni Leticia Nyerere mke wa Madaraka Nyerere mtoto wa hayati Mwl Nyerere.

Mama huyu Leticia Nyerere anatarajia kuondoa hodhi ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kwa kipindi cha miaka yote ya mfumo wa vyama vingi imekuwa ikitawala katika Jimbo hilo la Kwimba mkoani Mwanza bila mabadiliko yoyote ya kiuchumi na kijamii na maendeleo kwa ujumla.

Asante sana najua watajitokeza wengi kama yeye Mungu amulike Tanzania tupate viongozi bora
 
Leticia Nyerere sio makini, ni kweli alimkimbia Madaraka, kaenda Marekani nako kafulia kakimbia karudi kuomba Ubunge CHADEMA, kwa kutumia jina la Nyerere, mhhh...Kwimba haijavaa miwani ya Mbao, akishindwa labda atakimbia kumuomba msamaha Madaraka, sababu anapenda vitu vizuri bila kuhangaika, anataka Mhindi apite ili awe Mbunge....anyway, ni haki yake lakini......???
 
This is where JF leads the pack,no ifs no buts every aspect,negativity and positivity is laid bare-if its the Leticia i know then the opposition in tanzania has a gigantic way to go'
 
Leticia Nyerere sio makini, ni kweli alimkimbia Madaraka, kaenda Marekani nako kafulia kakimbia karudi kuomba Ubunge CHADEMA, kwa kutumia jina la Nyerere, mhhh...Kwimba haijavaa miwani ya Mbao, akishindwa labda atakimbia kumuomba msamaha Madaraka, sababu anapenda vitu vizuri bila kuhangaika, anataka Mhindi apite ili awe Mbunge....anyway, ni haki yake lakini......???

Sijui kuhusu umakini,

Mimi nilishasema mtu mwenye confidence na uwezo wake hawezi kusema anataka fulani awe mshindani wake kwa sababu itakuwa kazi rahisi kumshinda, hii ni kauli ya mtu mwenye mashaka na uwezo wake.
 
19144_100229920007453_100000613353513_3411_1109588_n.jpg

Mkwe wa Nyerere aiandama CCM

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na Maregesi Paul, Mbeya

LETICIA Nyerere ambaye alikuwa mke wa mtoto wa Hayati Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere, ameanza rasmi kampeni za kukibomoa Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akiwataka wananchi wajiunge na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Leticia alianza kampeni hizo jana kwa kuhutubia wananchi katika Jimbo la Mbeya Vijijini.

Alihutubia wananchi wa vijiji vya Idunda na Galijembe na kueleza ni kwa nini alijiunga na CHADEMA na kuachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokuwa akikiunga mkono kwa muda mrefu.

Akihutubia mikutano ya hadhara katika vijiji hivyo vilivyoko Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa nyakati tofauti jana, Leticia alisema amejiunga Chadema kwa vile anaamini ndicho chama kinacholenga kuwakomboa Watanzania.

"Mimi CCM naifahamu sana huenda kuliko Watanzania wengi wanaoiunga mkono ingawa haiwasaidii kwa namna yoyote.

"CCM ilikuwa na sifa enzi za Mwalimu Nyerere, lakini baada ya mzee huyo kipenzi cha Watanzania kututoka duniani, chama hicho kimepoteza mwelekeo na matokeo yake ndiyo maisha magumu na vitendo vya ufisadi tunavyovishuhudia kila kona ya nchi,” alisema Leticia.

Katika maelezo yake, Leticia alitumia muda mwingi kuwashawishi wanawake kujiunga na CHADEMA kwa vile kitendo cha kuendelea kuishabikia CCM kitawafanya waendelee kufariki kila wanapopata ujauzito na wakati wa kujifungua.

Leticia ambaye kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani, alisema baada ya kujiunga na chama hicho cha upinzani hivi karibuni, amejiona huru zaidi kwa vile sasa ana uwezo wa kuikosoa CCM ikiwa ni pamoja na kuwashawishi Watanzania wengine waachane na chama hicho tawala. Leticia alijiunga na Chadema hivi karibuni mjini Ngundu wilayani Kwimba, Mkoa wa Mwanza, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Kabwe Zitto kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji huo wakati alipokuwa katika ziara ya Operesheni Sangara kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mbali na Leticia, mwingine aliyejiunga CHADEMA hivi karibuni akitokea katika familia ya Mwalimu Nyerere ni Vicent Nyerere ambaye ni mtoto wa kaka yake Mwalimu Nyerere.
[/FONT]​

Gazeti la Mtanzania
 
"Mimi CCM naifahamu sana huenda kuliko Watanzania wengi wanaoiunga mkono ingawa haiwasaidii kwa namna yoyote". Alisema Leticia.

[/QUOTE]
Nilisema wengi wanaoshabikia CCM ni wale wanaoambulia kofia na tisheti lakini wanaoifahamu CCM vizuri hawafanyi hivyo, nikasema tena usione watu tunashabikia vyama vya upinzani ukadhani hatuijui milango ya CCM inawezekama kabisa tunaifaidi CCM kuliko wewe unayeambulia kofia. Hebu jiulize ni watanzania wangapi wanafaidika na matunda ya CCM kuliko Leticia.
 
Leticia Nyerere sio makini, ni kweli alimkimbia Madaraka, kaenda Marekani nako kafulia kakimbia karudi kuomba Ubunge CHADEMA, kwa kutumia jina la Nyerere, mhhh...Kwimba haijavaa miwani ya Mbao, akishindwa labda atakimbia kumuomba msamaha Madaraka, sababu anapenda vitu vizuri bila kuhangaika, anataka Mhindi apite ili awe Mbunge....anyway, ni haki yake lakini......???

Kama alimkimbia,alimtembea sisi hayatuhusu,yanayotuhusu hapa ni kuwa anagombea ubunge jimbo la Kwimba.Kura ndio zitaamua kama anafaa ama la!
 
Nilisema wengi wanaoshabikia CCM ni wale wanaoambulia kofia na tisheti lakini wanaoifahamu CCM vizuri hawafanyi hivyo, nikasema tena usione watu tunashabikia vyama vya upinzani ukadhani hatuijui milango ya CCM inawezekama kabisa tunaifaidi CCM kuliko wewe unayeambulia kofia. Hebu jiulize ni watanzania wangapi wanafaidika na matunda ya CCM kuliko Leticia.

Nakubaliana na wewe,umejibu vyema sana.
 
Back
Top Bottom