GE2025 Mke wa Mzee wa Vijisenti, Andrew Chenge, aongoza Kura za maoni Viti Maalum Simiyu

GE2025 Mke wa Mzee wa Vijisenti, Andrew Chenge, aongoza Kura za maoni Viti Maalum Simiyu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Tina Chenge mke wa Mzee wa Vijisent, Andrew Chenge, ameibuka kinara katika kura za maoni za kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalumu mkoa wa Simiyu, baada ya kupata kura 631 kati ya kura halali 1,029 zilizopigwa.

IMG-20250731-WA0087.jpg
Kura hizo zilipigwa katika Mkutano Maalumu wa UWT mkoa wa Simiyu uliowakutanisha wajumbe 1,053, ambapo waliopiga kura walikuwa 1,034, kura 5 zikiwa zimeharibika.

Katika matokeo hayo, wagombea wengine walioshika nafasi za juu ni,Ester Midimu aliyepata kura 500,Caritas Machupa kura 312,Minza Mjika kura 292,Rosemary Ng’hwani kura 186.

Wengine ni pamoja na Limi Kilalo kura 60,Jane Masanja kura 50 na Grace Balele kura 34.

IMG-20250731-WA0090.jpg
 
Back
Top Bottom