Naomba kujua kama ina ukweli wowote hii.
- Tunachokijua
- Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa Barua inayosambaa Mtandaoni ikidaiwa kuandikwa na Dkt. Fatma Maganga, mke wa Hayati Job Ndugai Si ya Kweli
Pamoja na mambo mengine, barua hiyo imeelezea kuwa Dkt. Fatma amejiuzulu nafasi ya Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) ili kutokuendelea kutumikia mfumo ulioamua kufumbia macho Heshima kwa mmoja wa Viongozi wake wakuu waliotangulia kwa kutokupeperusha nusu mlingoti Bendera, pamoja na Chama Chake cha Mapinduzi kuendelea na Ratiba, Sherehe na Mikutano yake kama kawaida
Aidha, yapo mapungufu kadhaa kwenye barua hiyo ikiwemo kukosewa kwa Jina la Mhusika, ambapo badala ya Maganga limeandikwa Mgagna.
Soma Pia: Mke wa marehemu Ndugai akanusha vikali barua inayosambaa mitandaoni ikidai amejiuzulu nafasi ya katibu Tawala Singida