Mke wa rafiki yangu anasumbuliwa na mumu wa mtu

Mke wa rafiki yangu anasumbuliwa na mumu wa mtu

NYUMBA KUBWA, Hiyo nimeikubali mia kwa mia na ninaufunga mjadala.
Amfundishe mkewe kukataa na trick za kutimua watu kama hao..Nachelea kusema huyo mwanamke ni wa aina yake...Kama yeye mwenyewe mtu mzima hajuhi kutimua mtu basi kazi ipo...

Na nataka kuangalia upande wa pili wa shilingi... sawa jamaa hajatulia..ndio...lakini mi navyowajua watu wasiojua kutimua wanaume atakuwa anampa signals ambazo zina read nataka... ndio maana anamfata bila kuchoka.

Nakumbuka those days nikiwa kijana mtu akinifata mara ya kwanza namjibu vizuri tu kuwa asante kwa kunipenda (maana kupendwa ni heri) lakini samahani siko interested. Kesho akinifuata tena akyanani siongei kitu wala kumwangalia simwangalii mwenyewe atajiona chizi harudi tena...Wanaume ukianza kujibishana nao mbona watakushinda... ooh mimi mke wa mtu... ataanza... hata mimi mbona nina mke. Hakuna discussion kuna watu wana 'A' za ku argue. Ni kujifanya bubu na kumfanya watu wamuone chizi anaongea peke yake. Ina work sana.
 
Hivi Nyumba Kubwa,kabla huyo mwanamke hajaolewa alikua anajilindaje?Au alikua anamkubali kila mwanaume?
 
Hello wana JF.
Nina rafiki yangu mmoja ambaye kwa sasa yuko nchi ya jirani anasoma. Amemuacha nyumbani mke wake na watoto wao watatu. Mke wake ni mama wa nyumbani na anashughuli zake za kujiongezea kipato. Ni familia yenye upendo na wote mme na mke wanapendana sana. Tatizo kwa sasa ni jirani yao mmoja, mme wa mtu anayemnyemelea huyo mke wa rafiki yangu. Anakaa standby akichungulia dirishani, mke wa rafiki yangu akienda dukani hilo jamaa linamfuata nyuma na kumtongoza, akielekea sokoni, jamaa hilo linawasha gari haraka lina pretend kumpa lift. Mke wa rafiki yangu a.k.a shemeji hamfichi mme wake anamwambia kila kitu maana anapatikana kwenye simu. Hilo dume limekuwa kero kwa shemeji. Sasa rafiki yangu kaniomba ushauri afanye nini? Nilichomshauri ni ampigie huyo jemba aache kumfuata mke wake maana ana namba yake ya simu. Sasa ninaileta issue hii kwenu wana JF nikiomba maboresho ya nini kifanyike kumstopisha huyo fara.

Ikishindikana huo ushauri uliompa, shemeji yako akafungue kesi kwa Kova!
 
Ndugu yangu hebu achana na hayo mambo kwani huyo ni Shemeji yako, usikute na wewe unamtaka akakukatalia.
Umeshaambiwa ni Mwanamke kamili ana akili zake anajua baya na zuri, mwenzako lift anaifurahia na hawezi mwambia mummewe siku akikanyagwa, hapo lazima na mboga anaachiwa, na Daladala hatapanda kwani Gari ipo
Mimi yamenikuta kuna jirani yangu kamtongoza Mke wangu huu mwaka wa pili, siku Mke wangu anampandishia na mimi nilikuwepo lakini jamaa mpaka leo mate yanamtoka, kila wakikutana jamaa hakomi, mm nimeacha kwa sababu ukimtukana ni aibu ya Mwanamme kwa nini Mwanamke asifanye kazi hiyo mwenyewe?
Acha Mme wake aje mshirikiane kumnasa mgoni wake lakini wewe hata nikikuelekeza ukalinunue TEGO huko KISUMU Nchini KENYA halitafanya kazi mpaka mwenye mali.
 
huyo mwanamke keshaliwa na jamaa hizo zote ni jama za kuku attract na wewe uingie mtegoni. uone mmm mbona jamaa anamfuatilia sana basi dada huyu ni bomba otherwise huwa ni rahisi sana kwa mume/mke kama hayuko interested na mwenzake huwa haiendelei sana anakuwa stopped soon
 
au wewe ndiye ndiye mshitakiwa namba 1 , sasa unatafuata pa kutokea?

Hata mm nina wasiwasi huyu jamaa ndiye mshtakiwa no. moja. turudi kwenye mada, Hivi mwanamke mwenye watoto watatu anatongozwa anashtaki kwa mumewe? shame. huyo mwishowe atamkubali tu na akimkubali atasema? kwanza mpaka mke wa mtu utongozwe ujue hujajiweka kama mke wa mtu ndio maana mtu anapata urahisi kukuingia. Hilo swala amwachie mkewe amkomeshe huyo jamaa na akishindwa bac ahesabu hana mke ana mtoto wa shule.
 
Inaonyesha huyu mwanamke hajui kumkatalia mwanaume! Hivi wanaume wote wanaomtongozaga huwa anamwambie mumewe awakanye? au tangu aolewe huyo ndo mwanaume wa kwanza kumtongoza?

Kifupi ni kwamba huyo mke doesnt have a life
 
Wanawake wanaoshitaki kwa waume zao wapo wengi tu

Lakini unajua ni kwa nini wanafanya hivyo? Wanataka kuwarusha roho waume zao...kwa maneno mengine mkeo akikwambia fulani kanitaka ni kuwa anakwambia mimi bado ninalipa...hata ukiniacha wako wanaonitamani. Ndio maana wanaume walio makini hawawezi kufurahi kuambiwa news kama hizo...wanajua wife anatamba kijanja.


Mimi mume wangu ana wivu sana na sitathubutu kumwambia upuuzi kama huo kwani najua ndio utakuwa mwanzo wa kuvuruga amani nyumbani. Imagine namwambia boss amenitaka...si ntaambiwa nitafute kazi kwingine. Kama adult unatakiwa mabo kama hayo uyamalize mwenyewe.

Hata mm nina wasiwasi huyu jamaa ndiye mshtakiwa no. moja. turudi kwenye mada, Hivi mwanamke mwenye watoto watatu anatongozwa anashtaki kwa mumewe? shame. huyo mwishowe atamkubali tu na akimkubali atasema? kwanza mpaka mke wa mtu utongozwe ujue hujajiweka kama mke wa mtu ndio maana mtu anapata urahisi kukuingia. Hilo swala amwachie mkewe amkomeshe huyo jamaa na akishindwa bac ahesabu hana mke ana mtoto wa shule.
 
Tafuta number ya mke wake kisha mueleze kwamba unaonelea ni busara wewe na yeye mkaingia kwenye mchakato kama ambao mme wake ameuanzisha kwa mkeo. hapa una pretend kama wewe ndio mume wa mke anayewindwa. send lovely sms to her katika wakati ambao unajua jamaa yuko nae.

nadhani utakuwa umepata agent mzuri zaidi wa kulitatua hili swala at the root.
 
inaonekana huyo mwamamke anamlegezea huyo mwanaume, kama tangu mwanzo angeonesha hataki tena kwaukali sidhani kama huyo mwanaume angeendelea kumfatafata. nakama kashafanya yote lakini mwanaume bado anamg`ang`ania basi awambie watu wazima mseme au wamwambie mkewe.
 
Back
Top Bottom