Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump kufanya ziara nchini

mashakani

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2018
Posts
615
Reaction score
990
https://twitter.com/share?text=Mke ...8-4780592-54pfmb/index.html&via=MwananchiNews
mke+pic.jpg

Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump
Kwa ufupi
  • Amesema ziara yake imetokana na kazi ambazo zinafanywa na Shirika la Misaada la Marekani USAID kwa nchi za Afrika na kwamba maeneo ambayo shirika hilo limekuwa likifanyia kazi yamekuwa ni sehemu ya maisha yake.

Washington, Marekani. Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump hatimaye ameweka wazi ratiba ya ziara yake barani Afrika ambapo atatembelea nchi za Ghana, Malawi, Kenya na Misri kuanzia wiki ijayo ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kimataifa akiwa peke yake.
Ziara ya Melania barani Afrika inalenga kuhamasisha ulinzi wa haki za watoto pamoja na mazingira bora ya utoaji elimu kwenye mataifa atakayotembelea.
Melania alisema hayo wakati alipokutana na wake wa marais mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa, na kueleza sababu za kuzitembelea nchi hizo.
Katika taarifa yake Melania amesema ziara yake imetokana na kazi zinazofanywa na Shirika la Misaada la Marekani USAID kwa nchi za Afrika, ambapo amesema maeneo ambayo shirika hilo limekuwa likifanyia kazi yamekuwa ni sehemu ya maisha yake.
Melania alisema anatarajia ziara yake kwenye mataifa hayo kuwa yenye tija hasa wakati huu ambapo mtoto wa kiafrika ameendelea kukabiliwa na changamoto za kielimu, matumizi ya dawa za kulevya, unyanyasaji, usalama katika matumizi ya mtandao, umasikini na magonjwa, akisema katika karne hii watoto hawapaswi kuwa katika mazingira haya.
 
Hivi mke wa "mtu yule" mbona hana habari na mambo kama haya wanayofanya wenzake!?
 
Safi sana mama yetu melaniaaa....njoo uzidi kutumwagiaa neemaa..
 
Wakenya hamuachi vituko jamani
 
Partager un lien sur Twitter
mke+pic.jpg

Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump
Kwa ufupi
  • Amesema ziara yake imetokana na kazi ambazo zinafanywa na Shirika la Misaada la Marekani USAID kwa nchi za Afrika na kwamba maeneo ambayo shirika hilo limekuwa likifanyia kazi yamekuwa ni sehemu ya maisha yake.

Washington, Marekani. Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump hatimaye ameweka wazi ratiba ya ziara yake barani Afrika ambapo atatembelea nchi za Ghana, Malawi, Kenya na Misri kuanzia wiki ijayo ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kimataifa akiwa peke yake.
Ziara ya Melania barani Afrika inalenga kuhamasisha ulinzi wa haki za watoto pamoja na mazingira bora ya utoaji elimu kwenye mataifa atakayotembelea.
Melania alisema hayo wakati alipokutana na wake wa marais mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa, na kueleza sababu za kuzitembelea nchi hizo.
Katika taarifa yake Melania amesema ziara yake imetokana na kazi zinazofanywa na Shirika la Misaada la Marekani USAID kwa nchi za Afrika, ambapo amesema maeneo ambayo shirika hilo limekuwa likifanyia kazi yamekuwa ni sehemu ya maisha yake.
Melania alisema anatarajia ziara yake kwenye mataifa hayo kuwa yenye tija hasa wakati huu ambapo mtoto wa kiafrika ameendelea kukabiliwa na changamoto za kielimu, matumizi ya dawa za kulevya, unyanyasaji, usalama katika matumizi ya mtandao, umasikini na magonjwa, akisema katika karne hii watoto hawapaswi kuwa katika mazingira haya.
Washington, Marekani. Mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump hatimaye ameweka wazi ratiba ya ziara yake barani Afrika ambapo atatembelea nchi za Ghana, Malawi, Kenya na Misri kuanzia wiki ijayo ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kimataifa akiwa peke yake.

Nathani wewe utakuwa Mkenya, maana hao wengine wasingeandika kwa Kiswahili.
 
Atawasaidia nini wakazi wa kibera?
Hizi ni sifa za kijinga na uzamani
 
aisee hawa viongozi wa kutoka ughaibuni huko wanapigana vikumbo kuingia nchini mazeee....tumechoka kuwapokea dahhhh kila siku!! watuache na ss tupumue kdg
 
Back
Top Bottom