Mke wa rais wa Msumbiji avutiwa na huduma za kibingwa hospitali ya Taifa Muhimbili

Mke wa rais wa Msumbiji avutiwa na huduma za kibingwa hospitali ya Taifa Muhimbili

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
MKE WA RAIS WA MSUMBIJI AVUTIWA NA HUDUMA ZA KIBINGWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Gueta Selemane Chapo, ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) za jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Mama Gueta amepongeza ubora wa huduma za kibingwa na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utoaji wa matibabu.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mama Gueta Chapo amepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mohamed Janabi, na kufafanuliwa kuhusu huduma zinazotolewa katika vitengo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kitengo cha Tiba ya Uzazi kwa Njia ya Kisasa (IVF), wodi ya kina mama waliojifungua, na huduma za upasuaji wa moyo kwa watoto na watu wazima zinazotolewa JKCI.

Aidha, akiwa katika wodi ya wanawake waliojifungua, Mheshimiwa Mama Chapo amepata fursa ya kukutana na akina mama waliolazwa, ambapo alitoa zawadi na kusisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora kwa mama na mtoto, akitaja kuwa huo ni msingi muhimu wa maendeleo ya jamii.

Katika Kitengo cha IVF, Mheshimiwa Mama Chapo ameelezwa kwa kina kuhusu huduma zinazotolewa kwa wanawake na wanaume wenye changamoto za uzazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Mama Chapo ameonesha kuvutiwa na mafanikio ya huduma hiyo na kubainisha umuhimu wa kuimarisha huduma kama hizo nchini Msumbiji.

Vilevile, akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Mheshimiwa Mama Chapo amepata maelezo kuhusu huduma za kibingwa za upasuaji na matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima.

Pia ameshuhudia kazi ya madaktari bingwa na kupongeza ubora wa huduma zinazotolewa, pamoja na mchango wa ushirikiano wa kimataifa katika kuboresha huduma hizo.

Katika mazungumzo yake na viongozi wa hospitali hizo, Mheshimiwa Mama Chapo ameeleza kufurahishwa na kiwango cha huduma na teknolojia inayotumika katika MNH na JKCI, huku akisisitiza kuwa uzoefu alioupata utasaidia kuanzisha ushirikiano wa kina kati ya Msumbiji na Tanzania, hususan katika maeneo ya afya ya moyo, huduma za uzazi na matibabu ya kibingwa.

IMG-20250508-WA0164.jpg
IMG-20250508-WA0163.jpg
IMG-20250508-WA0160.jpg
IMG-20250508-WA0162.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250508-WA0167.jpg
    IMG-20250508-WA0167.jpg
    539.3 KB · Views: 36
  • IMG-20250508-WA0168.jpg
    IMG-20250508-WA0168.jpg
    697.2 KB · Views: 42
  • IMG-20250508-WA0150.jpg
    IMG-20250508-WA0150.jpg
    666.7 KB · Views: 32
  • IMG-20250508-WA0158.jpg
    IMG-20250508-WA0158.jpg
    447.4 KB · Views: 34
  • IMG-20250508-WA0156.jpg
    IMG-20250508-WA0156.jpg
    594.9 KB · Views: 36
  • IMG-20250508-WA0161.jpg
    IMG-20250508-WA0161.jpg
    671.5 KB · Views: 33
  • IMG-20250508-WA0145.jpg
    IMG-20250508-WA0145.jpg
    529.2 KB · Views: 37
  • IMG-20250508-WA0157.jpg
    IMG-20250508-WA0157.jpg
    810.2 KB · Views: 32
  • IMG-20250508-WA0159.jpg
    IMG-20250508-WA0159.jpg
    628.5 KB · Views: 32
  • IMG-20250508-WA0165.jpg
    IMG-20250508-WA0165.jpg
    735.2 KB · Views: 35
  • IMG-20250508-WA0169.jpg
    IMG-20250508-WA0169.jpg
    533.1 KB · Views: 32
  • IMG-20250508-WA0166.jpg
    IMG-20250508-WA0166.jpg
    849 KB · Views: 33
  • IMG-20250508-WA0148.jpg
    IMG-20250508-WA0148.jpg
    421.4 KB · Views: 32
Serikali ya Msumbiji imeonesha nia ya kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete( JKCI) kwa kuwatuma wataalamu wake kujifunza namna ya kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wagonjwa ili nchi hiyo iwe na uwezo wa kutoa huduma hizo kwa wananchi.

Ushirikiano mwingine ni wa kuwapeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa katika Taasisi hiyo na kuwatuma wataalam wao kwenda kujifunza namna ya kutoa
huduma za matibabu ya moyo na hiyo ni sehemu ya tiba utalii.
3d67fb97-26ba-4b94-b8e8-f1bdb8d32cde.jpeg

Hayo yamesemwa leo Mei 8, 2025 na Mke wa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Mama Gueta Selemane Chapo alipotembelea taasisi hiyo leo iliyopo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Mhe. Mama Gueta alisema Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inauwezo mkubwa wa kuhudumia wagonjwa wa nje 2,000 na kulaza wagonjwa 100 kwa wiki.

"Hospitali yetu ya Maputo haiwezi kufanya haya yote tunatamani ije ishirikiane na hospitali hii katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo".

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter ******* alisema Mhe. Mama Gueta alikwenda kuona teknolojia ya kisasa ya matibabu ya moyo inayotumika katika taasisi hiyo ikiwemo ya kuwafuatilia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wakiwa
nyumbani kwa kuwekewa shuka maalum la Dozee.

Dkt. ******* alisema kupitia shuka hilo daktari anaona mapigio ya moyo, presha, upumuaji na mambo mbalimbali yanayoendelea kwa mgonjwa
akiwa nyumbani na hivyo kuepusha vifo vya ghafla.

"Ameona watoto waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo kwani taasisi yetu kwa mwaka inafanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa 1,000 kwa njia ya tundu dogo wagonjwa 3,000 kwa mwaka na hii ni namba kubwa na sisi ndio wa kwanza kufanya upasuaji mkubwa barani Afrika", alisema Dkt.
*******.
 
Chuma kwelikweli. Wakatoliki hatunaga kazi mbovu. Naona yupo na Mgombea wetu huko WHO
 
wabongo bhana, cheap sana, kwa hiyo ulitegemea asemeje labda? wewe ualikwe na kupewa heshima zote halafu uombwe cha kusema utasemaje? ulitegemea aseme vinginevyo? btw Mama Maria Nyerere anaendeleaje iliwekwa hapa jf na mdau kwamba ni mgonjwa siku nyingi, mnajua chochote, labda?
 
Na hilo barakoa? Wangemwambia Tanzania hatuamini kuna vitu kama korona!
 
Back
Top Bottom