Mke wa Rais wa Zanzibar akutana na Mke wa Rais wa Msumbiji Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar akutana na Mke wa Rais wa Msumbiji Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Mke wa Rais wa Zanzibar akutana na Mke wa Rais wa Msumbiji Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya ZANZIBAR MAISHA BORA FOUNDATION (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi, amekutana na kuzungumza na Mke wa Rais wa Msumbiji, Mama Gueta Selemane Chapo, aliyetembelea ofisi za ZMBF.

Alipowaili katika Ofisi za Taasisi hiyo Mama Gueta Chapoo alipokelewa na mwenyeji wake Mama Mariam Mwinyi ambaye aliambatana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya ZMBF Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro na Mkurugenzi wa Miradi wa ZMBF, Bw. Joseph Kaphipa.

Ziara hiyo ililenga kujifunza na kuona jitihada zinazofanywa na taasisi ya ZMBF inavyofanya kazi zake katika kuboresha maisha ya wananchi wa Zanzibar.

Katika ziara hiyo Mama Gueta amepongeza jitihada zinazofanywa na ZMBF katika kuboresha Maisha ya Wanawake, Watoto na Vijana baada ya kujionea moja ya shughuli zinazofanywa na Watoto wa kike katika Taasisi hiyo ya ZMBF ikiwemo ya kutengeneza taulo za kike zenye ubora na ambazo zimekuwa zimekuwa msaada mkubwa kwa Watoto wa kike Zanzibar.

Akiongea na mgeni wake Mama Marim Mwinyi amefurahi ugeni huo kuitembelea Taasisi yao na alimweleza namna wanavyo saidia Wazanzibari kuboresha maisha yao hususani kwa wanawake, Watoto na Vijana.

IMG-20250510-WA0070.jpg
IMG-20250510-WA0084.jpg
IMG-20250510-WA0080.jpg
IMG-20250510-WA0043.jpg
IMG-20250510-WA0090.jpg
IMG-20250510-WA0086.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250510-WA0077.jpg
    IMG-20250510-WA0077.jpg
    421 KB · Views: 37
Back
Top Bottom