June 30, 2019
Dar -es-Salaam,Tanzania
Mke wa Bw. Raphael Ongangi, Bi Veronica azungumza na vyombo vya habari jinsi tukio la utekaji wa mumewe lilivyofanyika katika makutano ya barabara maarufu za kitongoji cha Oysterbay, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Tanzania .
Source : millard ayo
Bi. Veronica anaelezea watekaji hao hawakuonesha kutaka au kudai fedha wala kupora gari waliokuamo yenye na mumewe.
Katika tukio hilo Bi. Veronica anasema aliweza kutambua uwepo wa 'mkuu' wa watekaji aliyekuwa anaratibu tukio hilo zima kwa kutoa amri na nini kifanyike.
Na 'mkuu' huyo alikuwa mtu wa mwisho kuondoka eneo aliposhikiliwa Veronica huku kukiwa hakuna uporaji wa simu, fedha wala gari alilokuamo.
Ni wiki moja sasa imepita baada ya tukio hilo la utekaji kutokea, na vyombo vya dola yaani Polisi wa Tanzania wamekuwa karibu kumpatia Veronica maendeleo ya uchunguzi na pia Naibu balozi wa Kenya nchini Tanzania amekuwa akiwapatia usaidizi wa karibu familia hiyo iliyokumbwa na mkasa huo wa kutisha.