Mke wa Raphael Ongangi azungumza utekaji

Mke wa Raphael Ongangi azungumza utekaji

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
June 30, 2019
Dar -es-Salaam,Tanzania

Mke wa Bw. Raphael Ongangi, Bi Veronica azungumza na vyombo vya habari jinsi tukio la utekaji wa mumewe lilivyofanyika katika makutano ya barabara maarufu za kitongoji cha Oysterbay, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Tanzania .

Source : millard ayo
Bi. Veronica anaelezea watekaji hao hawakuonesha kutaka au kudai fedha wala kupora gari waliokuamo yenye na mumewe.

Katika tukio hilo Bi. Veronica anasema aliweza kutambua uwepo wa 'mkuu' wa watekaji aliyekuwa anaratibu tukio hilo zima kwa kutoa amri na nini kifanyike.

Na 'mkuu' huyo alikuwa mtu wa mwisho kuondoka eneo aliposhikiliwa Veronica huku kukiwa hakuna uporaji wa simu, fedha wala gari alilokuamo.

Ni wiki moja sasa imepita baada ya tukio hilo la utekaji kutokea, na vyombo vya dola yaani Polisi wa Tanzania wamekuwa karibu kumpatia Veronica maendeleo ya uchunguzi na pia Naibu balozi wa Kenya nchini Tanzania amekuwa akiwapatia usaidizi wa karibu familia hiyo iliyokumbwa na mkasa huo wa kutisha.
 
July 1, 2019
Dar-es-Salaam, Tanzania

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Mh. Zitto Kabwe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kigoma mjini, Tanzania azungumzia kutekwa kwa rafiki yake Raphael Ongangi.

Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema Raphael Ongangi ni rafiki yake tu na wala hahusiki na masuala yake (Zitto) ya kisiasa hivyo wasiwaumize watu bure na familia zao kwa kuwa tu wanafahamiana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 1, 2019 jijini Dar es Salaam, Zitto amesema masuala ya utekaji yamekuwa yakileta taswira mbaya kwa nchi ya Tanzania.

Aidha ZITTO Amesema Tanzania haipaswi kuwa na taswira Mbaya kwa mataifa mengine hasa nchi jirani ambazo tuna shirikiana nazo katika mambo mbalimbali.

Pia Zitto ameelezea mazingira yalivyokuwa siku ya tuko la kutekwa kwa Raphael.

Raphael Ongagi ambaye ni raia wa Kenya ametimiza siku ya saba tangu alipotekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam, Juni 24, 2019 ambapo Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewataka waliomteka kumwachia akiwa hai.
Source: Global TV online
 
Upande wa pili wa Story ya mwandishi Cyprian Musiba kwa wa Kenya kuhusu kupotea kwa Raphael Ongangi
 
July 2, 2019

Raphael Ongangi apatikana akiwa hai, Mombasa Kenya
1 hours ago

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIA wa Kenya na mfanyabiashara anayeishi nchini Tanzania, Raphael Ongangi aliyekuwa ametekwa nyara, amepatikana akiwa hai jijini Mombasa nchini Kenya
Juni 24, 2019 Ongangi akiwa na mkewe Veronica Nkundya maeneo ya Oysterbey jijini Dar es Salaam alipokua akitoka katika kikao cha wazazi katika shule ya mtoto wao alitekwa na watu wasiojulikana.
Katibu wa Itikadi,Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amethibitisha kupatikana kwa Ongangi ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe.
"Wamemona wakamtupe Ongangi jijini Mombasa tunashukuru yupo hai japo atujui undani wa afya yake ilivyo,'' amesema Ado.
Source : www.azaniapost.com
 
Published on 2 Jul 2019
BREAKING: MFANYABIASHARA RAPHAEL ONGANGI APATIKANA MOMBASA, MKEWE ATHIBITISHA!

Raia wa Kenya, Raphael Ongagi, aliyedaiwa kupotea tangu wiki iliyopita akiwa Tanzania, amepatikana leo Jumanne, Julai 2, 2019, jijini Mombasa nchini Kenya akiwa hai. Mkewe, Veronica Kundya amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram. Veronica ameandika: “Nipo hapa leo nikiwa na furaha kubwa sana sana kuushuhudia UKUU WA MUNGU. My Raphael AMEPATIKANA leo Mombasa na yupo salama, sina taarifa ingine zaidi ya hio ila hio pia INATOSHA sana kwangu.

“Sina mengi ya kusema zaidi ya KUMSHUKURU MUNGU sana sana kwa kuwa yeye ni Mungu wa miujiza maana ametenda Napenda KUWASHUKURU WOTE kwa moyo wangu wote kwa niaba ya familia yangu kwa sala na kujitoa kwenu kwa hali na mali kwenye kipindi hiki kigumu.

“Mimi na familia yangu tutaishi kutangaza ukuu wa Mungu, Mungu azidi kutubariki sisi sote na familia zetu

Source : Global TV online
 
Kwa hiyo alitekewa Kenya au hao watekaji wamepenya mpk Mombasa na kumuachia huko
 
Back
Top Bottom