Mke wa Trump na mke wa Zelensky waungana kupambania amani ya Ukraine

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Moja ya tukio lililogonga vichwa vya habari katika mkutano wa Rais Donald Trump wa Marekani na Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine jijini Washington DC jana Jumatatu ni barua za wake wa marais hao, katika kutafuta amani ya Ukraine na Russia.

Kabla ya mkutano na viongozi wa Ulaya pamoja na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, Keir Starmer Waziri Mkuu Uingereza, Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa, Friedrich Merz, Kansela wa Ujerumani, Zelenskyy alimkabidhi Trump barua hiyo na kumwambia ‘ni ya mkeo Melania sio ya kwako’.

Soma pia: Mkutano wa Trump na Zelensky waisha na sintofahamu

Screenshot 2025-08-19 034939.png

Chanzo: Mwananchi​

Barua hiyo ya mke wa Rais wa Ukraine, Olena Zelenska, inahusu shukurani kwa mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump, kwa hatua yake ya kumkosoa Rais wa Russia, Vladimir Putin.

Melania amekuwa mkosoaji wa wazi wa Putin na wiki iliyopita aliandika barua akimtaka alinde watoto, kufuatia ripoti kwamba angalau watoto 20,000 wamechukuliwa na wanajeshi wa Russia tangu uvamizi wa mwaka 2022. Kwa mujibu wa dazeti la Daily Mail la Uingereza.

Zelenska alishukuru kwa hatua hiyo na kupitia mumewe, Volodymyr Zelenskyy, alikabidhi barua hiyo kwa Rais Trump ili aipate Melania. Katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Zelenskyy ameandika:
“Ninataka kumshukuru Mama wa Taifa wa Marekani, Melania, kwa kulipa kipaumbele suala moja la maumivu na gumu zaidi la vita hivi utekaji wa watoto wa Kiukraine na Russia. Tunathamini huruma yake na barua yake kwa Putin.”
 
View attachment 3446206

Hizo ni propaganda za Wazaliwa wa Ulaya mashariki unajua ndio wanaongoza katika kampeini ya uichukia Urusi, vile vile kumbuka Melania mkewe Trump ni mzaliwa wa Ulaya mashariki iliyo wahi kuwa chini ya USSR, barau hii Melania akumpatia Trump ampelekee Putin kwa bahati mbaya hiyo ni moja wapo ya mipango iliyo sukwa na akina Macron na bila shaka waziri mkuu wa Uingereza lengo lao hasa hawakutaka mkutano baina ya Putin na Trump unafanikiwe ndio wakaja na madai ya kutunga tu kwamba Urusi imeshikilia zaidi ya watoto 2,000 kutokea Nchini Ukraine kusafirishwa kwenda Urusi kinguvu ie bila ya ridhaa yao, walifikiri hilo lingemkasirisha sana Trump na kutoa amri ya kusitisha mkutano/maelewano, kwa bahati nzuri, sina shaka Trump alisha gundua ujanja wa Viongozi wa EU na Uingereza walivyo kuwa wamepania ili mkutano huu usifanikiwe.
 
Back
Top Bottom